Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas amemtangaza David Mwenge Nyantora kuwa mshindi wa Super Jackpot ya mechi 13 akiwa amejishindia shilingi 265,780,681. ikiwa ni takribani miezi 11 tangu kumtangaza mshindi wa mwisho wa Supa Jackpot mechi hizihizi 13 ambapo hii ni awamu ya pili kupata mshindi wa Supa Jackpot tangu ianzishwe rasmi.
hili ni jambo la kihistoria kwa kampuni ya kubashri kupata zaidi ya washindi wa Jackpot 10 na kuwatangaza kwa miaka 6 mfululizo. Supa Jackpot ya wiki hii imeweza kutoa washindi wa bonasi jumla ya 8708 huku jumla ya bonasi zilizotolewa ikiwa ni zaidi ya milioni 756.
Naye mshindi alikuwa na haya ya kuongea, Akizungumza katika hafla hiyo maalumu iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, Dar es Salaam, David anasema alianza kucheza na SportPesa mwaka 2018, baada ya kuifahamu kupitia usomaji wa magazeti, amewashauli Watanzania waendelee kucheza na SportPesa.
Naye Mkuu wa kitengo cha Uhusiani na Mawasiliano wa SportPesa Sabrina H. Msuya alimpongeza mshindi na kumhimiza kuwa balozi kwa wengine. Anawakumbusha Watanzania Supa Jackpot ipo na itaendelea kuwepo kutegemeaa na matokeo ya kila wiki. endeleeni kutuamini kama ambavyo, David ametuamini na matokeo ya ushindi mtayapata. amesema haya wakati wa kumtangaza mshindi wa Supa Jackpot David Mwenge Nyantora.
Habari Picha na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment