Monday, 19 February 2024

WAZIRI NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAAHIDI MAMBO MAZITO ZAO LA MIANZI

Waziri wa Maliasili na Utalii Angera Kailuki amesema mkakati aliouzindua wa zao la mianzi serikali itasimamia na kutekeleza kwa vitendo kwa kutega bajeti ya kutosha ili kutoa elimu kwa jamii namna bora ya kupanda mianzi kwani faida zitakazopatikana ajira, kodi, fedha za kigeni, malisho kwa mifugo na kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. 

Waziri Kailuki ameitaka taasisi ya utafiti kutafiti mbegu bora na ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kupanda zao la mianzi.

Nae kwa upande wake katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dr. Hassan Abbas amesema zao la mianzi litasaidia kuondoa mmomonyoko wa ardhi huku akiahidi mpango kazi na mkakati uliozinduliwa wa kupanda zao la mianzi atasimamia kikamilifu.

Nae kwa Ubapande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema tukipanda mianzi tutabusulu kumomonyoka kw ardhi hekta milioni 5 huku, akisisitiza kuwa zao la mianzi litaleta faida kubwa nchini Tanzania ambako mikoa kumi na nne 14 litapanda zao la mianzi.

Habari na Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment