Eng. Kitainda Hamed Michael meneja wa miradi ya Ubia kati ya Serikali na sekta Binafsi TANROADS amesema mwezi wa tatu walitangaza Tenda wamejitokeza China, Uturuki na wengine kampuni zilizorudisha tenda ni kampuni tatu zote kutoka China wanalipia huduma,katika makampuni matatu inahitajika kampuni moja tu. Serikali ikishindwa kutoa huduma wanatumia sekta binafsi kuchangia.
amesema changamoto ipo barabra ya morogoro road kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro wanatumia masaa sita na ajari za kila siku hivyo zitakoma itakapojengwa Barabra ya express, itakuwa barabara ya viwango vya juu na manufaa yake kuokoa mafuata, vipuli vya magari na afya za waendeshaji ambapo itapelekea mwananchi kupata huduma iliyo bora na uchumi kuongezeka.
TANROADS imefungua Tenda ya Barabara kutoka Kibaha hadi Chalinze, Tender inasehemu tatu na watapokea Proposal. katika sekta binafsi wamewekeza 100% katika kuchangia huduma ya barabara, serikali kupata mitaji sekta binafsi ili kujenga barabara hii inasaidia kukuza uchumi wa nchi.
Habari na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment