Tuesday, 20 February 2024

TANROADS, TBA, NA TEMESA KUKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA EGYPT

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amemshukuru Rais Dkt Samia kwa kuleta wawekezaji kutoka Egypt wa usafirishaji na miundombinu pamoja na wajumbe wake. Waziri Bashungwa amefuraishwa na mradi wa kutoka Cairo kwenda Captaon Afrika ya Kusini ambao njia yake itapita kwenye nchi 9 na Tanzania ikiwemo nchi itakayo nufaika na mradi huu ambao utakamilika ifikapo mwaka 2060 pia amewakaribisha kwenye sekta binafsi kwaajili ya project mbalimbali moja ya fursa ya kupata wawekezaji wa viwango vya juu.

Waziri bashungwa amewaambia Tanroads kutekeleza ahadi ya Rais kuwa na mkakati wa waandisi kuwa sehemu ya kusaidia wakandarasi wa zawa ambako kila kilometa 20 kutakuwa na vijana wawili. Kubadilishana uzoefu wa majenzi na kujifunza amewaomba Temesa kuwa na mitambo ya kisasa kwaajili ya kusaidia Wakandarasi wa ndani hii ndio mikakati ya Rais kuleta ubunifu na kuongeza wigo.

Kipande cha kutoka Zambia unapoingia nchini pale Songwe ni kilometa 1600 ni moja ya barabara ya mikakati Dar es Slaam na Morogoro Tanroads kujenga barabara za Express Morogoro kwenda Dodoma ambako itafungua uchumi na kutengeneza ajira kwa watanzania. 

Nae waziri wa Egypt amewaarika viongozi wa Tanzania kutembelea nchini mwao ili wajionee ujenzi wa Barabara zinavyopendeza . Chakwanza kudizaini njia za kawaida zote wanaweza kuzitengeneza katika ubora pia wanauwezo wa kutengeneza madaraja ya aina zote amewaomba watu wa Tanroads waende wakajionee ubunifu wa hali ya juu. Ujenzi wa barabara za Cement ya kawaida na hata barabara za rami pamoja na njia za juu njia za mwendokasi.

Habari na Victoria Stanslaus

No comments:

Post a Comment