Friday, 13 September 2019

WALIOJENGA UKUTA WA MADINI YA TANZANITE ARUSHA (MERERANI) WATANGAZIWA NEEMA



           JENERALI VENANCE MABEYO
MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NCHINI TANZANIA
   Mkuu wa majeshi ya ulinzi Nchini Tanzania jenerali Venance Mabeyo amesema vijana wote wa kujenga taifa JKT waliojitolea katika oparesheni ya Kikwete na Magufuri katika kujenga uzio wa ukuta mererani kwa ajili ya kuzuia wizi wa madini ya Tanzanite waweze kujitokeza na vyeti vyao ngome makao makuu ili waingizwe katika mchakato wa JWTZ.
Ameyasema hayo makao makuu ya jeshi na kusisitiza kuwa vijana taklibani eluf mbili na thelathini (2033) waliweza kujitolea kujenga ukuta huo. Hivyo kwa wale ambao hawakuweza kuchaguliwa wapeleke vyeti vyao haraka iwezekanavyo mgulani jijini Dar es Salaam.
Jenerali Venance amesema kuwa Rais Dr John Pombe Magufuri alisema vijana wote waliojitolea waweze kupatiwa ajira. Kuanzia mwaka 2018 jeshi lilikuwa likijitahidi kufanya mchakato na kuwachukuwa baadhi ya vijana. Kwakua hawakuweza kuchukuliwa wote jeshi linatoa wito kwa vijana wote ambao hakupatiwa ajira wajitokeze na vyeti vyao ili jeshi liwakamilishie mchakato mzima na kupatiwa ajira.
Jenerali Mabeyo amekemea pia vijana wenye tabia ya kupiga simu kwa viongozi wa juu na kujaribu kutoa lugha chafu kwa kuwa hawajapatiwa ajira. Amewatoa hofu kuwa idadi yote wanayo na watapatiwa ajira Kama Rais wa nchi alivyoagiza
Jenerali Mabeyo amesisitiza kuwa vijana waachane na zana potofu ya kuwa lazima akifika JKT basi atapata ajira. Jeshi dhumuni lake ni kuwaweka vijana kuwa wakakamavu na wazalendo katika nchi Yao
HABARI PICHA NA ALLY THABITI

Wednesday, 11 September 2019

BARAZA LA MITIHANI LATOA ONYO KALI WENYE TABIA ZA KUVUJISHA MITIHANI


Dkt. CHARLES E MSONDE
KATIBU MTENDAJI BARAZA LA MITIHANI TANZANIA 

Baraza la mitihani nchini tanzania limetoa wito kwa kamati za Mikoa na Halimashauri/Manispaa/Jiji kuhakikisha kuwa taratibo zote za uendeshaji wa mitihani ya taifa zinazingatiwa ipasavyo. Ni pamoja na kuhakikisha mazingira ya vituo vya mitihani yanakua salama, tulivu na kuzuiya mianya yote inayoweza kusababisha kutokea kwa udanganyifu katika mitihani inayoendelea,mitihani itaanza kesho tarehe 11 na kumalizika tarehe 12. Baraza pia limewataka wasimamizi wote wa mitihani nchini wafanye kazi kwa weledi na uadilifu kwa kuzingatia kanuni za mitihani na miongozo waliyopewa. Baraza limesisitiza kuwa wale wote waliopanga njama za kufanya udanganyifu kipindi cha mitihani watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi na kanuni za utumishi wa umma
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya baraza hilo Dkt Charles E. Msonde amesema kuwa watanzania wote wanapaswa kulinda usalama wa wanafunzi na kuhahakisha hawawaingilii na kuwasumbua kipindi chote cha mitihani yao. Jumla ya wanafunzi 947,221 ndio waliosajiliwa na baraza kwa ajili ya mitihani ya mwaka 2019, Ambapo kati yao wavulana ni 451,235 sawa na asilimia 47.64 na wasichana 495,986 sawa na asilimia 52.36. Baraza pia limetoa idadi ya watahiniwa wenye mahitaji maalum waliosajiliwa kwa ajili ya mitihani hiyo ni 2,678 ikiwa kati yao 81 ni wasioona, 780 wenye uoni hafifu, 628 wenye ulemavu wa kusikia, 325 ni wenye ulemavu wa akili na 864 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwilini. Baraza pia linawaasa wasimamizi wote nchini kuwapa mahitaji yote muhimu watu wenye majitaji maalum kama kuongezewa mda wa dakika 20 kwa kila saa kwa somo la Hisabati na dakika 10 kwa kila saa kwa masomo mengine kama mwongozo wa baraza unavyoelekeza
HABARI PICHA NA ALLY THABITI

Monday, 9 September 2019

KATIBU MKUU WA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA PADRI CHARLES KITIMA

Padri CHARLES KITIMA wa jimbo la singida ambae pia ni katibu mpya wa baraza la maaskofu katoloki nchini Tanzania  na aliyewahi kuwa makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Mt Augustine (SAUTI) Mwanza akiongea katika makao makuu ya baraza hilo.
Katibu Padri charles kitima amesema kuwa wanawake wote nchini wajitokeze kwa wingi katika fursa mbalimbali za kisiasa. Ameendelea kusema kuwa mwanamke katika jamii ni nguzo kuu sana hivyo kukaa nyuma kwao katika uongozi mbalimbali ni kurudisha nyuma maendeleo katika taifa letu kwani wanawake wana nguvu na ari ya uongozi ya hali ya juu sana
Padri huyo amesisitiza kuwa vyama vyote nchini viwape kipaumbele wakinamama ili tuweze kupiga hatua katika maendeleo ya kisiasa na sekta nyingine ikiwemo sekta ya uchumi ambayo ndio sekta kuu inayo hitaji watu makini na wanaochukia rushwa na bila kuwa na ubadhirifu
Wakinamama waliojitokeza katika mkutano huo wakifuatilia kwa makini maneno ya Padri Charles kitima na kupewa moyo wa kupambana katika siasa na kujumuika katika vyama mbalimbali vya siasa nchini

Padri Charles kitima ametoa wito huo kwa kinamama wote waliojitokeza ili waweze kutoa elimu nzuri kwenye jamii yetu kuhusiana na maswala ya siasa na kuwa walimu wazuri kwa jamii kwa ujumla. amesisitiza kua mama kwenye jamii ndie mwalimu mkuu wa mafunzo mbalimbali
HABARI PICHA NA ALLY THABITI

CHAMA CHA WANANCHI CUF CHALAANI UKATILI NA MAUAJI YANAYOENDELEA AFRIKA KUSINI



                             ENG, MOHAMEDI NGULANGWA
NAIBU MKURUGENZI WA SERA NA MAMBO YA NJE CHAMA CHA CUF 

Chama cha wananchi CUF kimelaani vikali ukatili na mauaji yanayoendelea nchini Afrika kusini na kudai kuwa kitendo hicho kinajaribu kuligawa bara letu la Afrika na kutuweka katika ubaguzi wa hali ya juu sana. Naibu mkurugenzi wa sera na mambo ya ndani wa chama cha CUF amesema kuwa mwenyekiti mpya wa SADC Mh, Dr JOHN POMBE MAGUFURI aweze kuitisha mkutano wa dharura ili kuzungumzia na kutatua changamoto hizi zinazo likabili bara letu la Afrika.
Ameyasema hayo katika ofisi za chama hicho makao makuu Buguruni jijini Dar es salaam na kukemea vikali unyama huo unaofanywa na watu wa demokrasia ya Afrika ya kusini. Eng, Ngulangwa amesema ili kulinda heshima ya bara letu na kutoleta ubaguzi kati yetu ni lazima kuweza kutatua kwa haraka tatizo hili kabla halijawa kubwa zaidi na kumtaka Raisi wa Tanzania ambae ni mwenyekiti mpya wa SADC kulipa kipaumbele tatizo hili na kulipatia ufumbuzi ili kuendeleza umoja kati yetu waafrika wote kwa ujumla        
HABARI PICHA NA ALLY THABITI        

Saturday, 7 September 2019

CHANGAMOTO YA WOTOTO KUBAKWA NA KULAWITIWA AKINAMAMA WAPEWA MBINU

KAMISHINA WA SKAUTI MKOA WA DAR ES SALAAM
BI.AMINA MAURID
BI.Amina Maurid akiwa katika kongamano la TGNP MTANDAO Mabibo jijini Dar es salaam amewaasa akinamama wote nchini kuwa waangalifu kwa watoto wao. Amesema kuwa akinamama wasiwaache watoto wao bila kuwakagua mara kwa mara na endapo wakiachwa na wadada wa kazi,huyo dada wa kazi apewe haki zake zote ili asipate wazo la kumfanyia vitendo vya ukatili mtoto. Ameongeza pia wazazi wote kwa ujumla wajitahidi kutoa elimu ya kijinsi kwa watoto wao, Bi Amina ameahidi kuwa elimu na mafunzo aliyopata TGNP MTANDAO ataielimisha jamii yote kwa ujumla ili watu wapate elimu ya kumkomboa mtoto katika vitendo vya kiunyanyasaji wa kingono
                                MWALIMU WA JINSIA SHULE YA MSINGI BUGURUNI
Mwalimu pia ametoa mifano mbalimbali aliyokutana ikiwemo kumfumania binti mdogo wa darasa la tatu akivua nguo za shule hadharani maeneo ya makumbusho stendi na kuvaa nguo za nyumbani ili aingie mtaani na kufanya vitendo viovu. Mwalimu amesema hii ni kutokana wazai kutojali mda wa kurudi mtoto kutoka shule hata akirudi usiku wazazi hawahoji wala kujari tukio hilo. Hivyo amesisitiza uangalifu zaidi uchukuliwe zidi ya watoto ili kuwalinda zidi ya unyanyasaji wa kingono
                             MDAU NA KIONGOZI WA TGNP MTANDAO MABIBO
Ameongeza pia wazazi waache mazoea, endapo wakimpata mhusika wa tukio la ubakaji au kulawiti waache kushawishiwa na pesa kwan alieathirika na kupata shida ni mtoto. Hivyo wasikubali ile dhana ya kupatania nyumbani kwani kufanya vile ni kumnyanyasa mtoto
HABARI PICHA NA ALLY THABITI

Friday, 6 September 2019

MKURUGENZI WA TBS AANIKA MAMBO MAZITO

                                         Mkurugenzi wa TBS Dr Ngenya, Athuman Yusuf
Amesema shirika la viwango nchini TBS mafanikio walioyapata ni kujituma zaidi na kutekeleza wito wa mh Rais Dr JOHN POMBE MAGUFURI za kuelekea Tanzania ya viwanda pia ueredi na uadirifu ndio maana wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kazi. Sifa hizi zimetolewa na wafanyabiashara wa chama cha TCI katika Hotel ya serena ambako walipongeza shirika la viwango nchini Tanzania TBS Kwa utendaji wao mzuri
Habari picha na ally thabiti
                                                  MAKAM WA RAIS TCI SHABIRR
Makam wa rais TCI Amesema watajitshidi kutatua changamoto za wanachama wa TCI zinazowakabiri katika biashara zao na watawatafutia fursa za kibiashara ndani na nje ya nchi
Ametoa wito kwa wafanya biashara kujiunga na TCI Ambako mpaka hivi sasa wapo wanachama zaidi ya 400. Amesema haya jijini katika hotel ya serena


                           WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA HON INNOCENT                        

                                                            BASHUNGWA (MP)
Nae waziri wa viwanda na biashara amewapongeza wafanyabiashara wa TCI kwa kufanya biashara zao kwa uwazi, kufuata kanuni, sheria na taratibu za nchi na amewapongeza viongozi wa TCI kwa kuwa wakweli na kuwaunganisha wana TCI na taasisi zingine. waziri INNOCENT BASHUNGWA Amesema changamoto wanazokabiliana nazo wafanyabiashara wa TCI serikali itazifanyia kazi hivyo wasiwe na hofu wala mashaka juu ya serikali ya Dr POMBE MAGUFURI
Habari picha na ally thabiti

SERIKALI INA NIA THABITI KUSHIRIKIANA NA WADAU WA TASNIA YA NAFAKA KUKOMESHA CHANGAMOTO-WAZIRI HASUNGA 


HABARI PICHA NA ALLY THABITI
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano na wafanyabiashara na wasindikaji wa mazao ya nafaka katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano JNICC Jijini Dar es salaam leo tarehe 29 Agosti 2019.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akifungua mkutano na wafanyabiashara na wasindikaji wa mazao ya nafaka katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano JNICC Jijini Dar es salaam leo tarehe 29 Agosti 2019.
 HABARI PICHA NA ALLY THABITI
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumzia fursa zilizopo katika tasnia ya nafaka wakati akifungua mkutano na wafanyabiashara na wasindikaji wa mazao ya nafaka katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano JNICC Jijini Dar es salaam leo tarehe 29 Agosti 2019. 

Na ALLY THABITI, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi madhubuti wa Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ina nia njema kabisa ya kuhakikisha kuwa inashirikiana na wadau wote katika kuhakikisha kuwa tasnia ya nafaka inaendelea na kuondoa changamoto zinazojitokeza.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 29 Agosti 2019 wakati akifungua mkutano na wafanyabiashara na wasindikaji wa mazao ya nafaka katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano JNICC Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa, Serikali peke yake, haiwezi kuziondoa changamoto hizo bila wafanyabiashara, wasindikaji na wasafirishaji kushirikiana na Serikali.

Katika mkutano huo waziri Hasunga amezitaja fursa zilizopo kwenye tasnia ya Nafaka kama ambazo ni pamoja na eneo linalofaa kwa kilimo ambalo linakadiriwa kuwa hekta milioni 44. Kati ya hizo, hekta milioni 29.4 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Eneo hilo, linafaa kwa kilimo cha mazao yote ya biashara na chakula, yakiwemo mazao ya nafaka kama mahindi, mtama, mpunga, ngano na mengineyo.

Fursa nyingine alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati, inajitahidi sana kufikisha umeme vijijini ambako ndiko nafaka zinapatikana. Hadi sasa asilimia 70 ya vijiji nchini, vimepatiwa umeme. Umeme huo unatakiwa utumike pia katika eneo la usindikaji. Hadi sasa, sehemu ndogo ya maghala kwenye usindikaji wa mpunga na mahindi kupitia mashine za kukoboa mpunga na mahindi.

Mhe Hasunga alisema kuwa Kuna baadhi ya maeneo, maghala mazuri yamejengwa  kwa usimamizi wa Serikali ili kuwa na uhifadhi mzuri wa nafaka. Mfano, maghala mengi yaliyojengwa wakati wa BRN bado hayajaweza kutumika ipasavyo.

Alisema Nchi yetu ina ikolojia tofauti tofauti, hali hii inasababisha baadhi ya maeneo kuwa na mvua za kutosha, na maeneo mengine kuwa na uhaba wa mvua. Maeneo yanayopata mvua za kutosha huzalisha chakula cha kutosha pamoja na ziada. Kwa maeneo ambayo yamezalisha ziada, wanayo fursa nzuri ya kupeleka ziada hiyo kwenye maeneo mengine ambayo hayazalishi vizuri.

“Vilevile, nchi yetu imezungukwa na nchi ambazo hazina fursa kubwa ya kilimo kama tuliyonayo. Miongoni mwa nchi hizo ni kama Uganda, Kenya, Congo, Sudan na nyinginezo. Hii ni fursa nyingine ya soko kwani tukizalisha vizuri, uhakika wa soko la nje, ni mkubwa pia” Alikaririwa Mhe Hasunga

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amezitaja mada zitakazojadiliwa katika mkutano huo kuwa ni pamoja na Fursa ya biashara ya mazao ya nafaka katika soko la Afrika na uwezo wa Tanzania kuzalisha nafaka na wafanyabiashara kushiriki kikamilifu, Upotevu wa mazao ya nafaka baada ya mavuno, mkakati wa Taifa wa kudhibiti na matokeo ya utafiti wa hali ya maghala yalivyo hapa nchini, Uongezaji thamani katika mazao na kuboresha mazingira ya biashara ya nafaka na Mfumo wa masoko na uzoefu.

Alisema kuwa mada hizo zitatoa nafasi pia ya kuelewa vizuri tasnia ya nafaka ili kuwa na maazimio ambayo yatajibu changamoto mbalimbali hususani ya upatikanaji wa taarifa na utumiaji vizuri wa fursa zilizopo katika tasnia hiyo.

“Nitoe rai kwa washiriki wote, tusikilize kwa makini, tuwe wawazi, na kwa uhuru tujadili mada hizo kwa mapana na marefu, ili baada ya siku mbili hizi, tutoke na maazimio yatakayojibu changamoto za tasnia hii ya Nafaka” Alisisitiza Mhe Hasunga

Habari picha na ally thabiti