KAMISHINA WA SKAUTI MKOA WA DAR ES SALAAM
BI.AMINA MAURID
BI.Amina Maurid akiwa katika kongamano la TGNP MTANDAO Mabibo jijini Dar es salaam amewaasa akinamama wote nchini kuwa waangalifu kwa watoto wao. Amesema kuwa akinamama wasiwaache watoto wao bila kuwakagua mara kwa mara na endapo wakiachwa na wadada wa kazi,huyo dada wa kazi apewe haki zake zote ili asipate wazo la kumfanyia vitendo vya ukatili mtoto. Ameongeza pia wazazi wote kwa ujumla wajitahidi kutoa elimu ya kijinsi kwa watoto wao, Bi Amina ameahidi kuwa elimu na mafunzo aliyopata TGNP MTANDAO ataielimisha jamii yote kwa ujumla ili watu wapate elimu ya kumkomboa mtoto katika vitendo vya kiunyanyasaji wa kingonoMWALIMU WA JINSIA SHULE YA MSINGI BUGURUNI
Mwalimu pia ametoa mifano mbalimbali aliyokutana ikiwemo kumfumania binti mdogo wa darasa la tatu akivua nguo za shule hadharani maeneo ya makumbusho stendi na kuvaa nguo za nyumbani ili aingie mtaani na kufanya vitendo viovu. Mwalimu amesema hii ni kutokana wazai kutojali mda wa kurudi mtoto kutoka shule hata akirudi usiku wazazi hawahoji wala kujari tukio hilo. Hivyo amesisitiza uangalifu zaidi uchukuliwe zidi ya watoto ili kuwalinda zidi ya unyanyasaji wa kingono
MDAU NA KIONGOZI WA TGNP MTANDAO MABIBO
Ameongeza pia wazazi waache mazoea, endapo wakimpata mhusika wa tukio la ubakaji au kulawiti waache kushawishiwa na pesa kwan alieathirika na kupata shida ni mtoto. Hivyo wasikubali ile dhana ya kupatania nyumbani kwani kufanya vile ni kumnyanyasa mtoto
HABARI PICHA NA ALLY THABITI
No comments:
Post a Comment