Tuesday, 17 September 2019

KCB BANK YATOA ELIMU NA FURSA YA VIWANGO VYA JUU KWA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WAKATI

NDG, SHOSE KOMBE
MKURUGENZI WAJASIRIAMALI WADOGO NA WAKATI KCB
Bank ya KCB Nchini imetoa elimu na mafunzo kwa wajasiriamali wadogo na wakubwa katika kuchangamkia Fursa mbalimbali zinazotolewa na Bank hiyo na Namna ya kunufaika ukiwa mwanachana wa Bank ya KCB Nchini Tanzania
Akizungumza na waandishi wa Habari mjasiriamali ndugu Ngwalula Fundikila amesema wanachokitoa KCB na kitu kizuri sana ambacho kila Bank inabidi waweze kukiiga kwani wameweza kupata elimu ya vitu mbalimbali
Akitolea Mfano kuwa wajasiriamali wengu huwa hawana nidhamu ya pesa Hivyo kwa elimu wanayopewa na KCB itawasaidia katika mambo mengi sana. Ameongeza kuwa kupitia mikutano hii wataweza kukutana na wafanyabiashara wengine na kuweza kubadilishana mawazo na kupanua biashara zao. Amewataka pia KCB Kwenda mpaka vijijini ili nao waweze kupata mafunzo ya biashara
KCB Bank pia wameenda mbali zaidi na kusema kuwa watahakikisha wajasiriamali wote wadogo na wakati wanapata mafunzo makubwa ikiwemo kwenda China ili kuweza kuona na kujifunza namna ya bidhaa zinavyotengenezwa na kujifunza zaidi
Akizungumza na waandishi mheshimiwa shose kombe mkurugenzi wa wajasiriamali wadogo na wakati KCB amesema kuwa wamepanga utaratibu wa kuwapereka wajasiriamali Nchini China ili waweze kupata Mafunzo mengi zaidi na pia waweze kuagiza bidhaa moja kwa moja kutoka viwandani na kupata faida kubwa. Amewashukuru pia wajasiriamali kwa kuweza kujitokeza kwa wingi na Kuja kupokea mafunzo haya yanayotolewa na KCB
HABARI PICHA NA ALLY THABITI

No comments:

Post a Comment