Friday, 20 September 2019

MWANANCHI JUKWAA LA FIKRA WAMKUNA PROF, JOYCE NDALICHAKO

Waziri wa elimu sayansi na tekinolojia profesa Joyce Ndalichako akizungumza na mamia ya watu walioweza kujitokeza katika jukwaa la fikra lililoandaliwa na mwananchi communications limited lililobeba dhima ya kumuwezesha kijana kupata ujuzi na maarifa mahususi. Jukwaa hilo lilikuwa live kupitia vyombo mbalimbali vya Habari ikiwemo ITV, RADIO ONE pamoja na mtandao ya kijamii. Mwananchi Co limited wamekuwa wakiandaa majukwaa mbalimbali kila Mara hii ni kutoa Fursa kwa vijana kuweza kutoa maoni Yao na masuruhisho kuhusiana na Mada tofauti tofauti. Jukwaa la mwaka huu limekuwa ni latano kuweza kuandaliwa na mwananchi, Lakini viongozi wameweza kukiri kuwa safari hii ni lakihistoria kwani muitikio wa watu ulikua mkubwa mno hadi kufikia wengine kuweza kubaki nje ya ukumbi na kufuatilia kupitia runinga za dharura zilizofungwa maeneo hayo ya ukumbi ya kisenga hall mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Profesa Ndalichako pia amewataka vijana waweze kuiunga mkono kwani serikali imewekeza sana katika elimu, ikiwemo ujenzi wa maabara ya kisasa katika chuo kikuu cha kilimo sokoine Morogoro ili kuwapa ujuzi zaidi wanafunzi katika fani za kilimo. Serikali pia imetenga zaidi ya billion 13tsh katika upanuzi chuo kikuu cha tekinolojia mbeya.
Profesa Ndalichako pia amewashukuru wadau wengine mbalimbali walioweza kujitokeza kwake na kusema wapo tayari kuandaa majukwaa mengine. Kutokana na mda kuwa mchache kulinganisha na wingi wa watu kuliwasukuma wadau kupanga kuandaa jukwaa lingine ili vijana waweze kukutana Tena na kuweza kueleza changamoto zao. Vijana wengi waliweza kukubaliana na kauli ya kuweka utaratibu wa kutumia lugha moja kuanzia Shule za msingi mpaka chuo kikuu. Na isiwepo ya kutumia lugha ya kingereza kwa Shule za private halafu mwisho wa siku wanakutana chuo kikuu wote na mtoto alie tumia lugha ya kiswahili huo ni ubaguzi, hivyo Kama private wanatumia kingereza basi yabidi na Shule za serikali nazo watumie kingereza. Ni maoni ya mdau mmoja aliyejitokeza katika jukwaa la fikra
Mwanafunzi Shule ya secondary Alpha akitoa mawazo yake juu ya kile kinachosababisha matokeo mabovu mashuleni. Amesema kuwa kinachongania sana ni kuwepo kwa walimu wengi ambao hawana uwezo mkubwa wa kufundisha. Akitoa Mfano kuwa zipo Shule zinawachukua wahitimu wa kidato cha Sita ili waje kuwasaidia kufundisha wanafunzi wa kidato cha Sita, hapo huwezi tegemea mwanafunzi kupata matokeo mazuri. Kulingana na kanuni na taratibu zinaelekeza kuwa mwalim wa diploma ukomo wake ni kidato cha pili na mwenye degree ukomo wake ni kidato cha Sita. Sasa unakuta mtu Ana diploma na anafundisha mpaka kidato cha Sita. Hivyo akatoa pendekezo lake kuwa sector ya elimu iweze kuangalia walimu wenye ufaulu mkubwa ndio waweze kuwa walimu ili kupata matokeo chanya
Habari picha na REUBEN MAUYA 




No comments:

Post a Comment