Friday, 20 September 2019
KAMPUNI YA MAZIWA YA ASAS YAJA NA MIKAKATI MIZITO KUELEKEA KILELE KUHAMASISHA UNYWAJI MAZIWA
Mabalozi wa maziwa ya ASAS Nchini Tanzania wakiongea na waandishi wa Habari kuulezea Uma umuhim wa kunywa maziwa kila siku kwani kufanya hivyo kunakuwezesha kupata Afya nzuri na kukukinga na magonjwa mbalimbali. Wakisisitiza kuelekea siku ya uhamasishaji kunywa maziwa duniani ambako kilele chake kitafanyikia mkoani Iringa Tarehe 24/9/2019 mwaka huu. ASAS wanajivunia sana kwani mpaka sasa wameweza kutoa maziwa zaidi Lita laki Tatu (300,000) kwenye Shule za mikoa ya Iringa, Njombe pamoja na mbeya. Kampuni ya ASAS wamesema kuwa wataendelea kutoa maziwa mashuleni kwa kuwapatia Afya bora wanafunzi wote Nchini ili kuunga juhudi za mh Rais John Pombe Magufuri kwa kutoa elimu na Kama hawana Afya bora hawawezi kusoma kwa bidii
Pia mabalozi mbalimbali wa maziwa hayo pendwa hapa Nchini wakiwemo Maulid kitenge (mtangazaji Efm) Shafii dauda, Haji Manara, Mpoki, Steve Nyerere, Mwarabu Fighter, Dokii(mtangazaji Efm), anko zumo,tabu mtigita, jb na wengineo
Wamezidi kuwashukuru sana kampuni ya ASAS kwa huduma zao bora kwa jamii yetu kwani maziwa hayo yamesheheni vitamini vya kutosha vinavyo hitajika katika mwili wa mwanadamu
Haji Manara pia amesema kuwa kuwepo kwa kampuni ya ASAS Nchini kumefanya baadhi ya vijana Nchini kuweza kupata ajira na kuweza kujikwamua kimaisha na badala yake kpunguza idadi kubwa ya vijana kudhurura mitaani hovyo. Hivyo watajitahidi kwa nguvu zao zote katika kuhamasisha watu kuweza kunywa maziwa katika jamii hasahasa hususani siku ya kilele tarehe 24/9 /2019 mkoani Iringa
Habari picha na REUBEN MAUYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hongera ASAS Kwa jitihada walizofikia
ReplyDelete