Wednesday, 11 September 2019

BARAZA LA MITIHANI LATOA ONYO KALI WENYE TABIA ZA KUVUJISHA MITIHANI


Dkt. CHARLES E MSONDE
KATIBU MTENDAJI BARAZA LA MITIHANI TANZANIA 

Baraza la mitihani nchini tanzania limetoa wito kwa kamati za Mikoa na Halimashauri/Manispaa/Jiji kuhakikisha kuwa taratibo zote za uendeshaji wa mitihani ya taifa zinazingatiwa ipasavyo. Ni pamoja na kuhakikisha mazingira ya vituo vya mitihani yanakua salama, tulivu na kuzuiya mianya yote inayoweza kusababisha kutokea kwa udanganyifu katika mitihani inayoendelea,mitihani itaanza kesho tarehe 11 na kumalizika tarehe 12. Baraza pia limewataka wasimamizi wote wa mitihani nchini wafanye kazi kwa weledi na uadilifu kwa kuzingatia kanuni za mitihani na miongozo waliyopewa. Baraza limesisitiza kuwa wale wote waliopanga njama za kufanya udanganyifu kipindi cha mitihani watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi na kanuni za utumishi wa umma
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya baraza hilo Dkt Charles E. Msonde amesema kuwa watanzania wote wanapaswa kulinda usalama wa wanafunzi na kuhahakisha hawawaingilii na kuwasumbua kipindi chote cha mitihani yao. Jumla ya wanafunzi 947,221 ndio waliosajiliwa na baraza kwa ajili ya mitihani ya mwaka 2019, Ambapo kati yao wavulana ni 451,235 sawa na asilimia 47.64 na wasichana 495,986 sawa na asilimia 52.36. Baraza pia limetoa idadi ya watahiniwa wenye mahitaji maalum waliosajiliwa kwa ajili ya mitihani hiyo ni 2,678 ikiwa kati yao 81 ni wasioona, 780 wenye uoni hafifu, 628 wenye ulemavu wa kusikia, 325 ni wenye ulemavu wa akili na 864 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwilini. Baraza pia linawaasa wasimamizi wote nchini kuwapa mahitaji yote muhimu watu wenye majitaji maalum kama kuongezewa mda wa dakika 20 kwa kila saa kwa somo la Hisabati na dakika 10 kwa kila saa kwa masomo mengine kama mwongozo wa baraza unavyoelekeza
HABARI PICHA NA ALLY THABITI

No comments:

Post a Comment