ENG, JOHANNES MAGANGA
MKURUGENZI WA UPIMAJI NA UGEZI
Shirika la viwango na uthibiti TBS limetoa mafunzo maalum kwa wafanyabiashara wote Nchini. Lengo kuu ni kuwapa elimu ya namna ya kupata vibali vya kielekroniki, ambavyo vitawasaidia sana wafanya biashara kwani vimejumuishwa vitu vingi sana kwa wakati mmoja. Hii pia ni pamoja na kuwapunguzia gharama za kupeleka nyaraka zao ofisini TBS. Mafunzo hayo yametolewa kwa mawakala wa forodha na waagizaji bidhaa.
Mh, GERVAS KAIMU MKURUGENZI UTHIBITI UBORA
Amewatoa hofu waagizaji wa bidhaa na kuwambia kuwa wameweka njia salama za kulipa kodi, ambapo kutakuwa na Aina moja ya kodi kutokana na kuwa na mfumo mpya wa kielekroniki utakaowasaidia sana watu
Pia wamesema kuwa watahakikisha wanawapatia elimu yakutosha mawakala wote Nchini wa forodha na waagizaji wa bidhaa ili waweze kuelewa vizuri namna ya uendeshaji
MH, ABDALLAH MWINYI
KATIBU WA JUMUIYA YA WAFANYA BIASHARA KARIAKOO
MH, Abdallah Mwinyi amewapongeza sana TBS kwa mafunzo mazuri walioyapata kwani yatakua msaada mkubwa sana kwao na manufaa pia. Amepongeza pia kwa juhudi zao binafsi kwa kuwajali na kuwatengenezea mazingira rafiki Kama mfumo mpya waliouanzisha wa kielekroniki
No comments:
Post a Comment