Friday, 20 September 2019

WAZIRI ATOA PONGEZI KWA WANAWAKE KWENYE MAHAFALI YA PILI YALIYO ANDALIWA NA ATE


 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akizungumza wakati wa mahafali ya  pili ya programu ya mwanamke Kiongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa wanawake 20 kutoka makampuni mbalimbali wakitunukiwa vyeti vyao 

Akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo, Jenista amesema  ATE wamekuwa na mchango mkubwa katika kujenga uwezo wa rasilimali watu ambao watashiriki kukuza na kuboresha uchumi wa taifa letu na serikali imejipanga vizuri kuhakikisha tunafanya kazi pamoja kwa kuhakikisha kuwa tunawajengea uwezo vijana ili wapate ujuzi wa aina mbali mbali utakaowawezesha kufikia maendeleo endelevu kuelekea Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Amesema, kwa moyo wa dhati kabisa anayo furaha kuwapongeza ATE kwa kufanikiwa kuandaa kwa mara ya pili mfululizo Mkutano wa Mwaka wa Uongozi kwa Wanawake na kuzitaka Taasisi mbalimbali za kibiashara na Wadau mbalimbali nchini kuungana ili kuhakikisha programu hii inakuwa endelevu kwa kuwahamasisha wanawake wengi kushiriki mafunzo haya. 

Pia, ameupongeza uongozi wa ATE ambao wameshirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) pamoja naUN Global Compact Network Tanzania (UNGCN) kwa kuandaa mkutano huu kwa ustadi wa hali ya juu na ninaamini utaleta mafanikio makubwa kwa manufaa ya wanawake wengi wenye ndoto za kuwa viongozi nakupelekea matokeo chanya kwa taifa letu kwa ujumla 


 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Dr Aggrey Mlimuka akizungumzia programu ya mwanamke wa wakati ujao na kuzitaka makampuni kuwafuata pindi wanapohitaji wakurugenzi kwenye mahafali yaliyofanyika Leo Jijini Dar

Mkurugenzu Mtendaji wa ATE Dr Aggrey Mlimuka ameeleza kuwa Kwa kipindi cha toka mwaka jana wamefanikiwa kuanzisha Alumni ya programu ya Mwanamke Kiongozi kwa malengo ya kutengeneza mtandao thabiti wa wanawake ambao Watashirikiana kutimiza malengo yao ya kushika nafasi za juu za uongozi na kuwa Wakurugenzi wa bodi mbalimbali kwa kushirikishana nafasi hizo, kujadiliana mambo mbalimbali ya uongozi, kuchochea uwepo wa sera zinazoshirikisha wanawake katika uongozi na jinsi ya kuandaa wanawake wengine kwa ajili ya uongozi na pia kuwekeana ufadhili pale unapohitajika kwa ajili ya wao kushika nafasi mbalimbali za uongozi. 

Amesema kama Chama cha Waajiri wameandaa na kuhifadhi taarifa zote (data) juu ya wanawake hao waliohitimu toka awamu ya kwanza na kutoa rai kwa makampuni wanachama na wasio wanachama kuwasiliana na nao pindi wanapohitaji wakurugenzi wa bodi kwani programu hii imewajengea uwezo wa kumudu nafasi hizo kwa ufanisi wa hali ya juu.


Zifuatazo ni kampuni mbalimbali ambazo zimeleta wananyakazi wao katika mafunzo haya ni Legal and Human Right Centre ,Equinor Tanzania, Songas Gas Ltd, Social Action Trust Fund (SATF), National Housing Corporation (NHC), Barclays Bank Tanzania, TOL Gases, Grumeti Reserves na wao wenyewe ATE.

 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akikabidhi vyetu kwa baadhi ya wahitimu wa programu ya mwanamke Kiongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa wanawake 20 kutoka makampuni mbalimbali wakitunukiwa vyeti.
 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akikabidhi vyetu kwa baadhi ya wahitimu wa programu ya mwanamke Kiongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa wanawake 20 kutoka makampuni mbalimbali wakitunukiwa vyeti
Habari picha na REUBEN MAUYA .


No comments:

Post a Comment