Thursday, 3 June 2021

DR CHARESI KASANZU AFUNGUA MILANGO KWA WACHIMBAJI WADOGO

 

Charesi Kasanzu amesema anawakaribisha wachimbaji wadogo ambao wanaoitaji kuwekeza kwenye sekta ya Madini .

Kwani wao gharama zao ni nafuu katika kufanya tafiti za maeneo ya uchimbaji Madini kwa gharama nafuu .pia wanatoa ushauri na Elimu  .

Mafanikio makubwa waliyoyapata wamegundua gesi na Madini amesema haya wiki ya utafiti na ubunifu Chuo Kikuu cha Mlimani.

Habari picha na Ally Thabiti

FLORA STEPHANO AJA NA MUHAROBAINI WA UGONJWA WA KUTETEMEKA


 Muhadhiri Idara ya Zuolojia na Uhifadhi Viumbe poli amesema wamefanya tafiti kwaajili ya kupata tiba ya ugonjwa  wa Kutetemeka

Ivyo utafiti huu utakuja kutatua maradhi ya Kutetemeka na kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Kutetemeka .Flora Stephano Ameipongeza serikali na wadau wengine kwa kutoa mchango wao kwenye mambo ya tafiti na bunifu. 

Habari picha na Ally Thabiti 

AMOSI MAKALA AJA NA MAAGIZO MAZITO


 Mkuu wa Mkoa wa Dsm Amosi Makala ameitaka jiji la Ilala kuwawekea utaratibu nzuri wamachinga kwani kwa sasa vibanda walivyojenga vinaatalisha Usalama wao na Wananchi.

Pia ameaidi kupita kata kwa kata ili kutatua kelo za Wananchi amepojea vilio vya Madiwani wa jiji la Ilala ivyo amesema kelo zote atazifanyia kazi ikiwemo ujenzi wa barabara,zahati ,hospitali.

Swala la Talura atazifanyia kazi Lengo kuondoa mnyukano uliopo na machinjio ya vingunguti yaweze kumaliziwa haraka .

Habari picha na Victoria Stanslaus

Wednesday, 2 June 2021

TRA YAKUTANA NA TCCIA

 Julias Mjenga Afsa Mkuu wa Huduma na Mtoa Elimu kwa Mlipa kodi TRA amesema wamekutana na wafanyabiashara Lengo kupokea changamoto wanazokutana nazo katika Biashara zao.

Hivyo amesema watazifanyia kazi na kuzitilea ufafanuzi kelo zote pia amesema wameandaa vitabu vya Nukta Nundu kwaajili ya wasiio Ona Lengo wawe na uwelewa na Elimu ya ulipaji kodi.

Habari picha na Ally Thabiti


 

NAIBU MEHA WA ILALA APAZA SAUTI


 Sadi Kimji Naibu Meha wa Ilala amewataka Talura kutoa ushirikiano na Madiwani wa Ilala na tanzania kwa ujumla kwani wamekuwa kelo nawasumbufu kwa Madiwani na watanzania . 

Mfano katika ukusanyaji tozo za kuegesha magari ,faini uegeshaji mbaya wa magari .

pia Talura wanajenga Vivuko,Madaraja ,barabara pamoja na Mitaro.ambako utakuta kunakuwaga na mapungufu makubwa na kukosekana kuimarika kwa muda mrefu miundombinu hii .

Hivyo ili kuondokana na mnyukano huu ni vyema Talura kuwa wasikivu na waelewa .

Habari picha na Ally Thabiti   

ACP MAHANGA ATOA NENO ZITO


 Mkurugenzi wa Michezo Jeshi la Polisi Tanzania ACP Jonas Mahanga amesema Jeshi la Polisi linawapongeza silent Ocean kwa kuweza kuwapa vifaa vya michezo lindo hiki kinafanya michezo uendelee na iimalike kwa Jeshi la Polisi.

Habari picha na Ally Thabiti

JESHI LA POLISI KINONDONI LAWATOA LAO NYA WATU


 ACP Ramadhani.H. Kingai Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni  amewataka wanakinondoni kupuuza taarifa za mitandaoni kwani Kinondoni kupo shwari kiusalama na Jeshi lake limejipanga kwaajili ya kukabiliana na vitendo vyovyote vya kialifu.

Mpaka sasa Jeshi la Polisi Kinondoni limedhibiti wizi wa magari na vifaa vya magari pamoja  na kuvunja nyumba za watu .

Kamanda wa Polisi Kinondoni Ramadhani . H. Kingai ametoa rai kwa wanakinondoni wakifanyiwa vitendo vyovyote vya kialifu waende kutoa taarifa Polisi nasio kukimbilia mitandaoni ili kuondoa hofu kwa watu amesema haya ostabei Polisi Kinondoni wakati akiongea na Wanahabari.

Habari picha na Victoria Stanslaus