Tuesday, 9 November 2021

TBA YAJA KIVINGINE


 Tusekelege M. Joune Executive Director wa TBA amesema watu wajitokeze Kwa wingi kwenye Banda la TBA viwanja vyanazi mmoja ili waweze kupata elimu ya kibank na vipeperushi vya Aina mbalimbali bule.

Pia mabank yanatekeleza maagizo na maelekezo ya serikali riba za mikopo kuwa ndogo, TBA imesimamia na kiwango kimekuwa kidogo cha riba   Mkurugenzi wa TBA ameiomba serikali kutatuwa Changamoto zilizopo kwenye mabank . 

 huku akitoa wito Kwa wakopaji kulejesha Fedha Kwa wakati kwenye mabank na waache kukimbilia mahakamani.

Habari picha na Ally Thabiti

MBONI AJA KIBABE


 Katika Kuelekea Maazimisho ya Miaka 60 Tanzania (Tanganyika) Mwanadada MBONI ameamuwa kufanya Tamasha kubwa la Taharabu tena bule tarehe 10/12/2021 ambako kutakuwa na wasanii nguli akiwemo Khadija Kopa.

Habari picha Victoria Stanslaus

ESABERA KAONGA AWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA

 


Mfanya Biashara Kutoka  Mbeya Esabera Kaonga amewataka wanawake kujiunga na taasisi ya MWANAMKE NI TUNU kwani watapata fursa mbalimbali .pia amewataka watu kununuwa bidhaa zake Kwa Mawasiliano zaidi 0714 981 067.

Habari na Victoria Stanslaus

WIZARA YA ELIMU YANUFAIKA NA MABILIONI YA UVIKO 19


 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu amesema Fedha walizopata za UVIKO 19 watatumia katika ujenzi wa madarasa,mabweni na miundombinu  kwenye shule mbalimbali . Pia watanunua vifaa vya kuifunzia na kusomea watu wenye Ulemavu mbalimbali.

Habari picha na Ally Thabiti

Saturday, 6 November 2021

TAASISI YA MWANAMKE NI TUNU YAWAKOMBOA WANAWAKE


 Mkurugenzi wa Taasisi ya MWANAMKE NI TUNU Adera amesema Lengo lao ninkuwainuwa wanawake kiuchumi ambako wameweza kuwafikia wanawake zaidi ya elfu moja nchini Tanzania. Pia Wana matawi jijini Mbeya ,kanda ya kaskazini, Mkoani Iringa na Mikoa mingineyo .

Habari picha na Ally Thabiti

TARURA YAJA NA MIKAKATI MIZITO DSM


 Meneja wa Talura Mkoa wa Dsm Bwana Mkinga amesema wamepokea maelekezo ya maboresho ya mfumo wa Ukusanyaji wa tozo za uegeahaji wa magari Kwa njia ya mtandao yaliotolewa na Waziri wa Tamisemi Humi Mwalimu watayafanyia  kazina kutekeleza Kwa vitendo. 

Ikiwemo kutoa elimu ,matumizi ya Lugha nzuri na mengineyo. Pia amesema watu wenye Ulemavu watashirokishwa Kwa kiasi kikubwa .Mkinga ametoa wito Kwa waegesha magari Kwa Dsm kutoa ushirikiano wakati WA utoaji elimu na Baada ya mfumo kurejeshwa tarehe 1/12/2021.

Lengo ni kudhibiti upoteaji wa mapato ya Maegeaho ya magari.

Habari picha na Ally Thabiti

WIZARA YA TAMISEMI YATATUWA KELO YA MFUMO


 Waziri wa Tamisemi Humi Mwalimu amesema Kwa kushirikiana Tarura wametatuwa kelo zilizokuwa zimejitokeza kwenye mfumo wa tozo za kukusanya maeneo  ya Maegeaho ya magari .

Kwani watu walipokuwa wakiegesha magari yao waliweza kubainisha changamoto walizokutana nazo jijini Dsm wakati wa kulipa Kwa njia ya mtandao ...Ikiwemo kupigwa faini ya elfu30,kutopewa taarifa za madeni,kutopewa namba ya malipo,Lugha chafu Kwa watumishi na zinginezo.

Waziri Humi Mwalimu amesema Kwa sasa mteja atatozwa shilingi elfu kumi Kama atachelewa kulipa ndani ya siku 14, Kwa sasa atatozwa shilingi 500 na Kwa siku 2500 Baada ya kuegesha gari.  Pia Waziri ameitaka Talura kutoa elimu Kwa waegesha magari ndani ya siku 21 kwani mfumo huu utaanza tena tarehe 1/12/2021.

Waziri Humi Mwalimu ametoa wito Kwa waegesha magari nchi mzima kutumia mfumo huu Kwa kulipa tozo Kwa njia ya mtandao kwani inasaidia kutokupotea pesa za serikali.kabla ya kutumia mfumo huu Dsm ilikuwa inakusanya milioni25 na Baada ya kutumia mfumo huu imekusanya milioni 40.

Humi Mwalimu ametoa Rai Kwa Talura kutoa asilimia 40 ya Fedha kupelekwa kwenye halmashauri pia kutowachaji tozo ya Maegeaho watu wenye Ulemavu kupitia Sura ya 288.

Habari picha na Ally Thabiti