Monday, 15 November 2021

FORUM CC YATOA NENO KWA WANAHARAKATI WA TGNP MTANDAO


 Msololo Onditi Program Officer wa FORUM CC amewataka Wanaharakati wote Kuwajenga uwezo watu WA namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, Kwa Lengo la kunusulu vizazi vya sasa na vijavyo.

FORUM CC inaipongeza TGNP MTANDAO Kwa juhudi na jitihada wanazofanya Kwa jamii Kwa kuwapa elimu ya utunzaji wa Mazingira. 

 FORUM CC imetoa Rai Kwa serikali washirikiane na Wanaharakati ili waweze kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi . Kwa kuwapa rasilimali watu,Fedha na kuweka mazingira rafiki na wezeshi Kwa wadau wote Kwa maslai mapana Kwa tanzania .

Habari picha na Ally Thabiti

JOYCE WA TGNP MTANDAO AKITANA NA WANAHARAKATI


 Joyce Kutoka TGNP MTANDAO Amewataka Wanaharakati kuweka nguvu za pamoja ili kutokomeza Mimba za utotoni,Ndoa za utotoni na Utoaji wa mimba Kwa watoto wa kike  na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Pia Joyce wa TGNP MTANDAO ameitaka serikali ya Tanzania kutekeleza makubaliano waliyosaini SADC mwaka 2008 namna ya kutokomeza na kupinga maswala ya ukatili wa kijinsia .

Kwani katika makubaliano hayo tanzania imekuwa nchi ya mwisho katika utekelezaji.

Habari picha  na Ally Thabiti

MWANA HARAKATI JENIFA AHAIDI MAZITO


 Jenifa ni Mwanaharakati amesema Mafunzo aliyoyapata TGNP yamemjengea uwezo mkubwa wa namna ya kuweza kutokomeza mimba za utotoni na maswala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.  

Na mambo yote yanayousu ukatili wa kijinsia yeye atakuwa balozi mzuri,ametoa wito Kwa jamii kuungana na TGNP MTANDAO katika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Habari picha na Ally Thabiti

Tuesday, 9 November 2021

TBA YAJA KIVINGINE


 Tusekelege M. Joune Executive Director wa TBA amesema watu wajitokeze Kwa wingi kwenye Banda la TBA viwanja vyanazi mmoja ili waweze kupata elimu ya kibank na vipeperushi vya Aina mbalimbali bule.

Pia mabank yanatekeleza maagizo na maelekezo ya serikali riba za mikopo kuwa ndogo, TBA imesimamia na kiwango kimekuwa kidogo cha riba   Mkurugenzi wa TBA ameiomba serikali kutatuwa Changamoto zilizopo kwenye mabank . 

 huku akitoa wito Kwa wakopaji kulejesha Fedha Kwa wakati kwenye mabank na waache kukimbilia mahakamani.

Habari picha na Ally Thabiti

MBONI AJA KIBABE


 Katika Kuelekea Maazimisho ya Miaka 60 Tanzania (Tanganyika) Mwanadada MBONI ameamuwa kufanya Tamasha kubwa la Taharabu tena bule tarehe 10/12/2021 ambako kutakuwa na wasanii nguli akiwemo Khadija Kopa.

Habari picha Victoria Stanslaus

ESABERA KAONGA AWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA

 


Mfanya Biashara Kutoka  Mbeya Esabera Kaonga amewataka wanawake kujiunga na taasisi ya MWANAMKE NI TUNU kwani watapata fursa mbalimbali .pia amewataka watu kununuwa bidhaa zake Kwa Mawasiliano zaidi 0714 981 067.

Habari na Victoria Stanslaus

WIZARA YA ELIMU YANUFAIKA NA MABILIONI YA UVIKO 19


 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu amesema Fedha walizopata za UVIKO 19 watatumia katika ujenzi wa madarasa,mabweni na miundombinu  kwenye shule mbalimbali . Pia watanunua vifaa vya kuifunzia na kusomea watu wenye Ulemavu mbalimbali.

Habari picha na Ally Thabiti