Friday, 20 May 2022

NANGASU WAREMA MKURUGENZI WA MIRADI TAASISI YA WANAWAKE LAKI MOJA KUITANGAZA ROYAL TOUR

 Mkurugenzi wa Miradi ya Maendeleo Kutoka Taasisi ya Wanawake Laki Moja Nangasu Warema na barozi wa Utalii amesema wanamuunga mkono rais Samia Suluhu Hassan kuanziaha Royal Tour.

 kwani itasaidia Kwa kiasi kikubwa Kuongeza idadi ya watalii na wawekezaji kwenye sekta ya Utalii,pia kukuwa Kwa uchumi wa tanzania na kuongezeka Kwa fursa za Ajira Kwa watanzania .

Nangasu Warema amesema Wana mikakati wa kuzunguka nchi nzima kutangaza vivutio vya Utalii wataanza nyanda za Juu Kusini .

Habari na Ally Thabiti

Habari na 

MWENYEKITI WA TAIFA WA TAASISI YA WANAWAKE LAKI MOJA VICKY KAMATA AMUUNGA MKONO RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

 Taasisi ya Wanawake Laki Moja Tanzania Chini ya Mwenyekiti Vicky Kamata wamempongeza rais Samia Suluhu Hassan Kwa Kutoa ruzuku ya fedha kiasi cha bilioni Mia moja kwaajili ya kupunguza ongezeko ya bei ya mafuta, amesema itasaidia Kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mafuta Kwa bei nafuu na itapelekea kupunguwa bei Kwa vitu mbalimbali.

Amesema yeye na Taasisi Yao wanamuunga mkono rais Kwa hatuwa alioifanya.

Habari na Ally Thabiti

Wednesday, 18 May 2022

MAKAMU WA RAIS ATETA NA NIMR

 Dr Philip Mpango Makamu wa Rais Tanzania ameitaka NIMR Kuongeza Kasi kwenye Tafiti wanazozifanya lengo kukabiliana na milipuko ya magonjwa Kwa wakati na ameiagiza NIMR wawe na chanjo zenye kudhibiti magonjwa, pia ameiagiza Tafiti za Dawa za Tiba asili ziwe za kukamilika Kwa wakati na haraka na Matokeo yaonekane lengo tuwe na Dawa za asili  Kwa wingi nchini tanzania.

Makamu wa Rais amesema serikali imejipanga kujenga vituko vya Afya kila Kona ya tanzania kwaajili ya kunusulu vifo Ndio maana imetenga fedha za kutosha kwaajili ya Tafiti mbalimbali. 

Philip Mpango ameipongeza NIMR Kwa Kongamano la 31 la Kisayansi kwani litaibwa mambo mengi ambayo yataleta tija na faida Kwa nchi Yetu ya tanzania.

Habari na Ally Thabiti

CHUO KIKUU SUACHAISHUKURU NIMR KWENYE KONGAMANO LA 31

 Fidelis John Kutoka Chuo Kikuu SUA amemshukuru taasisi ya Utafiti wa Afya NIMR Kwa kufanya Kongamano la 31 kuanzia tarehe 17 na mwisho tarehe 19/2022 kwani Chuo Kikuu SUA kimepata fursa ya kuelimisha watu namna Panya Buku anavyoweza kutambuwa Ugonjwa wa Kifua Kikuu Kwa haraka zaidi .

Fidelis John amesema kupitia Panya Buku Tanzania inaweza  kutibu wagonjwa wa Kifua Kikuu Kwa wakati na haraka tena Kwa gharama nafuu ambako itapelekea pesa nyingi za serikali kuokolewa na vifo vyingi kupunguwa na kutokomeza  Kifua Kikuu.

Fidelis John amesema nchi ya Marawi na Ethiopia Wamechukuwa Panya Buku Kutoka Tanzania kupitia Chuo Kikuu SUA kwaajili ya Kupambana na kutokomeza Kifua Kikuu  kwenye  nchi zao.

Habari na Ally Thabiti


JANICE MAIGE AIPONGEZA NIMR

 Mtafiti wa Ifakara Health Institute Janice Maige amempongeza Taasisi ya Utafiti wa Afya ya Binadamu NIMR Kwa kufanya Kongamano la Kisayansi la 31 kwani itasaidia Kwa kiasi kikubwa kujuwa Mbinu mbalimbali za kuweza kukabiliana na milipuko ya magonjwa na namna ya kupata chanjo ya magonjwa yanayojitokeza nchini Tanzania na Duniani.

Janice Maige amesema Taasisi ya Ifakara Health Institute inafanya TAFITI kwenye upande wa Mareria Mfano Rufiji wamepunguza Mareria Kwa asilimia 34,upande wa Ukimwi na wanatoa elimu na Mafunzo kwenye matumizi ya Lishe Bora .

Habari na Ally Thabiti

TCRA YAISHANGAZA DUNIA

 Mwandisi Kisaka wa TCRA amesema Wameamuwa kukutana na Wanahabari wanaoandika habari za mtandaoni lengo kuwatambuwa na kuthamini mchango wao , na kuwataka wawe wanahandika habari za Miradi na Matukio Tu.

Mwandisi Kisaka Kutoka TCRA amewataka wanahabari wanaoandika habari za mtandaoni wazingatie sheria,kwanini na taratibu za Tanzania na Maadili ya nchi , huku akiwataka wafuate mizania wakati wa kuandika habari zao amesema haya jijini dsm makao makuu ya TCRA Ubungo wakati WA Mafunzo na Wanahabari wanaoandika habari za mtandaoni.

Habari na Ally Thabiti

MWANAHABARI AIPONGEZA TCRA


 Tunu Mwanahabari wa Tanzania Yetu Tv amesema anaipongeza na kuishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kwa kuwapa Mafunzo na kuwajengea uwezo wanahabari wa mtandaoni , Kwani wameweza kuzitambuwa sheria nakanuni za TCRA na kuepukana na hadhabu walizokuwa wanakutana nazo . 

Habari  Picha na Ally Thabiti