Sunday, 26 June 2022

DSTV YAJA KIVINGINE


 Mtendaji mkuu wa DSTV LEONARD SHELUKINDO amewataka watu kutoa 9900/= ili kuwangalia vipindi bora vya DSTV.

Habari na Ally Thabith

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ATOA MAAGIZO MATANO

 AMOS MAKALA, amewataka wenyeviti wa serikali za mtaa, watendaji, madiwani na mamea kuhakikisha wanawaondoa wamachinga maeneo yasiyofaa kwa biashara, kusimamia usafi.

Habari kamili na Ally Thabith 

MKURUGENZI WA TANTRADE AKUTANA NA WANAFANYA BIASHARA



 Latifa Mohamed Hamisi, Mkurugenzi mkuu wa TANTRADE amesema maonyesho ya ALBAINI NA SITA (46) ya Sabasaba yatakayofanyika tarehe 28/06/2022 yatakuwa yenye  kufana na mafanikio makubwa ambapo nchi zaidi ya sabini (70) zitashiriki na kwa wafanya biashara watanzania wataonesha bidhaa zao amewataka watu kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya sabasaba kwani kiingilio ni nafuu na miundo mbinu yote imeboreshwa pia kutakuwa na makongamano ya aina mbalimbali lengo kuwatafuia fursa wafanyabiashara wa kitanzania na wageni kutoka nchi za nje kuwaonesha fursa za uwekezaji nchini Tanzania ambako kauli mbiu kwa mwaka huu inasema "Tanzania ni mahali sahihi kwa usalama wa biashara na uwekezaji". Bi. Latifa Amesema haya kwenye semina iliyowakutanisha wafanya biashara watakao shiriki kwenye maonesho ya sabasaba. Maada zilizowasilishwa ni Afya, ambaye aliwasisha Rehema kutoka halmashauri ya Temeke amesisitiza na UVICO 19 ambako chanjo zinapatikana za UVICO 19. Wa pili, Loyce Kibuta, Ameelezea namna ya kujikinga na majanga ya moto na jinsi yakutumia vifaa vya kuzimia moto nawataka watu kupiga namba 114 la jeshi la zima moto kwaajili ya msaada.

Abdallah Seif Abdallah amewataka wafanyabiashara kutoa risiti na wanunuaji wa bidhaa kudai risiti ambaye atatoa risiti atapigwa faini ya shinilingi milioni tatu mpaka milioni nne na nusu na atakae nunua kitu bila kudai risiti atatozwa elfu thelathini mpaka milioni moja na nusu.

Nora wa Tantrade amezungumzia tuzo za banda bora ambazo zitakuwa na category 26 nae SUDI afisa biashara wa Tantrade amezungumzia mfumo wa vibali.

Kwa upande wake Masha amezungumzia kanuni za ushiriki 

Haya ndiyo ambayo yamezungumziwa kwenye semina kati ya Tantrade na washiriki wa maonyesho ya sabasaba.

habari Picha na Ally Thabith

Friday, 24 June 2022

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AIPONGEZA MAKUMBUSHO YA TAIFA

 Godwin Ggondwe amesema Kitendo cha MAKUMBUSHO ya TAIFA ya Kijito nyama  Kwa kufanya tamasha la watoto wenye maitaji maalum ni Jambo zuri  Kwani watu wenye ulemavu Wana haki sawa Amesema wilaya ya kinondoni inawathamini watu wenye ulemavu wote.

Kwa kuwapa elimu na Huduma zinginezo.

Nae Kwa upande wake Afisa elimu wa Makumbusho Wilhimina Josephu amesema ili ni tamasha la 34 amesema wameamuwa kuwakutanisha watoto wenye ulemavu lengo kuonyesha Wana haki Sawa na watoto wengine.

Pia amesema Makumbusho ya Taifa kuna miudombinu rafiki na wezeshi Kwa watu wenye ulemavu,swala la kuandika vipeperushi Kwa nukta nundu wamelibeba watalifanyia kazi.

Mwanafunzi Teresa wa darasa la sita shule ya misingi Kesho la wokovu kwaniaba ya watoto wenye ulemavu wamempongeza Makumbusho ya Taifa Kwa kuwajali na kuwathamini ivyo wameaidi watakuwa mabarozi Kwa Jamii .

Lengo watoto wenye ulemavu wapelekwe shule wakasome .

Habari na Victoria Stanslaus

Wednesday, 15 June 2022

TGNP YAWATAKA WANAHARAKATI KUPAZA SAUTI KWENYE BAJETI YA TILIONI 41.48

Mkurugenzi mtendaji wa TGNP Liliani Liumbi amesema bajeti iliyowasilishwa na Migulu Lameck Nchemba haijazingatia mlengo wa kijinsia hivyo amezitaka hasasi za kiraia nchini Tanzania na wanaharakati kuweka nguvu ya pamoja katika bajeti ijayo lengo izingatie mlengo wa kijinsia. TGNP imepongeza serikali kwa kufuta ada ya kidato cha tano hadi cha sita na kufanya elimu ya msingi mpaka kidato cha sita kuwa bure.

habari Picha na Ally Thabith
 

BAJETI YA TILIONI 41.48 YAWASILISHWA NA WAZIRI WA FEDHA MWIGULU NCHEMBA


Waziri wa fedha na mipango Mwigulu Lameck Nchemba amesema bajeti ya Tilioni 41.48 itakuwa mkombozi kwa watanzania kwani kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita elimu ni BURE, pia mabadiliko ya sheria kumi na tisa zimepitishwa kwenye bajet hii huku sekta ya kilimo, Afya, maji na miundo mbinu mfano barabara zimetengewa fedha za kutosha.

habari picha na Ally Thabith

TAIFA WAZIRI DORITHY GWAJIMA AJA NA BAJETI YA KIMKAKATI

 

Kiasi cha fedha bilioni 43.4 imetengwa kwenye wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na makundi maalum. 

Waziri Dorithy Gwajima amesema kiasi hichi cha fedha kinasaidia katika kupambana na ukatili dhidi ya watoto ambako zaidi ya asilimia 60 watoto wanafanyiwa ukatili majumbani kwao na asilimia 40 mashuleni, waziri Dorithy Gwajima amesema fedha hizi zitaimarisha maafisa ustawi na watendaji wengine.


Habari picha na Ally Thabith