Tuesday, 28 June 2022

ABDULMALIKI MOLLEL ATETA NA WAZIRI WA ELIMU ZANZIBAR




Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education amesema wanawapa fulsa wanafunzi wa Zanzibar kwenda kusoma vyuo vya nje amemueleza Waziri wa Elimu wa Zanzibar waitumie Global Link Education katika kuwaunganisha na vyuo vya nje kwani awatajuta. Nae waziri wa Elimu wa Zanzibar amempongeza na kumshukuru mkurugenzi wa Global Link Education Abdulmalik Mollel kwa kuwapa fulsa na kuwafungulia milango kwakwenda kusoma nje ya nchi watu wa Zanzibar.

Habari Picha na 

Ally Thabiti

GLOBAL EDUCATION KUTEKELEZA PLOGRAME HEET PROJECT KWA VITENDO


 
Mkurugenzi Mtendaji wa Blogal Link Education Abdulmalik Mollel ameitoa hofu Serikali kwenye HEET Project kwa wahaziri ambao wataenda kusoma nje ya Nchi kwani watatafutiwa vyuo vya gharama nafuu, usalama wa uwakika na ufuatiliwaji wa kozi watakazo maliza.

Abdulmalik Mollel ameiakikishia serikali nafasi za kwenda kusoma wahaziri nje ya nchi wapewe wao Global Link Education kwani ni wazoefu wa masomo kuanzia miaka ya zamani mpaka leo na hawana ubabaishaji hivyo hata kwa elimu za ndani Global Link Education ni wakongwe.

Amesema haya kwenye uzinduzi wa HEET PROJECT uliofaziliwa na Benk ya Dunia kwa miaka mitano yenye samani ya Bilioni 942 fedha za kitanzania.

Habari picha na.

ALLY THABITI

AFISA UHAMIAJI MSAIDIZI AWAPA TANO TANTRADE

Afisa Uhamiaji Msaidizi amempongeza TANTRADE Kwa Kutoa semina elekezi Kwa washiriki Kutoka nje ya nchi,Pia amesema VIsa ni bule Kwa wanachama wa Africa Mashariki 

Amesema haya kwenye maonyesho ya 46 viwanja vya Saba Saba  ambako kauli mbiu inasema TANZANIA NI SEHEMU SAHIHI KWA BIASHARA NA UWEKEZAJI..
Habari na Ally Thabiti 

FORUM CC YAJA NA MIKAKATI YA KUTUNZA MAZINGIRA

 Msololo Onditi Afisa Miradi FORUM CC amesema mikakati Yao ni Kutoa elimu Kwa Jamii namna ya Kutunza mazingira Kwa njia ya upandaji miti. pia wanaenda mashuleni na Wanawatumia mawakala 70 kwenye mikoa yote Tanzania.

Habari picha na Ally Thabiti

Sunday, 26 June 2022

JAMII YAOMBWA KUWATHAMINI WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU.

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam Godwin Gondwe ameitaka jamii kuwathamini watu wenye mahitaji Maalumu ikiwemo Walemavu kwani wanapaswa kupatiwa haki kama watu wengine.


Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe (mwenye Miwani) akiangalia ubunifu wa kazi  za sanaa zilizofanywa na Watoto wenye Mahitaji Maalum.

DC Gondwe ametoa rai hiyo wakati wa tamasha la Watoto wenye Mahitaji Maalumu lililoandaliwa  na Kijiji Cha Makumbusho ya Taifa  lenye ujumbe usemao"Haki Sawa Kwa Wote" lengo ni kuwakutanisha Watoto wenye mahitaji mabalimbali ikiwemo ulemavu wa viungo na walemavu wa ngozi( Albino).

Aidha amesema kwamba Watoto wenye mahitaji maalum wanatakiwa,kutambuliwa, kuthaminiwa na kupatiwa haki zao za msingi ikiwemo elimu ili kuwafanya waweze kuishi katika maisha bora ,huku akikemea jamii kuacha  vitendo vya unyanyapaa kwa Watoto hao.

" Nakipongeza Kijiji Cha Makumbusho ya Taifa  kwa kuandaa tamasha hili ambalo limelenga kutambua thamani ya Watoto wenye ulemavu,natoa wito kwa jamii,taasisi na mashirika mbalimbali kuendelea kuwathamini watu wenye ulemavu" amesema DC Gondwe.

Watoto wenye ulemavu kutoka shule mbalimbali za msingi ikiwemo shule ya Mgabe,Shule ya Msingi mchanganyiko,Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu ,wamekutana kwenye tamasha hilo nakuweza kushiriki Mambo mbalimbali ikiwemo michezo na burudani.

Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Kijiji Cha Makumbusho Bi.Wilhelmina Joseph amesema kwamba Makumbusho ya Taifa itaendelea kuthamini makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo Watoto wenye mahitaji mbalimbali ili kuwafanya wapate haki zao za msingi.
Watoto wenye Mahitaji Maalum wakionyesha burudani kwenye Tamasha la Watoto wenye Mahitaji Maalum lililoandaliwa na Makumbusho ya taifa Mkoani Dar es salaam.
'
"Tumeandaa tamasha hili ili kuthamini haki za Watoto hawa ,hivyo sisi Kama Makumbusho ya Taifa tumeandaa tamasha hili la Watoto wenye mahitaji Maalumu na tukaweka kauli mbiu ya Haki Sawa kwa Wote" ili kuifanya jamii itambue kuwa hata watu wenye ulemavu wana haki sawa na wengine hivyo wasiwafiche majumbani" amesema Bi Wilhelmina.

Akizungumza kwa niaba ya Walimu Wenzake kutoka shule hizo Bw.Emanuel Ibrahim kutoka shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu ( Salvation Army) amesema kwamba ulemavu siyo kushindwa hivyo wameiomba Makumbusho ya Taifa kulifanya tamasha hilo kuwa endelevu.

Habari Picha na Ally Thabiti

HAKIELIMU YAPONGEZA BAJETI YA SERIKALI



 


Habari picha na Ally Thabit

AMOS MAKALA AWATAKA WATUMISHI WALIOKULA BILIONI KUMI WAZITAPIKE


 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ametoa maagizo na maelekezo ndani ya siku saba mkurugenzi wa jiji la Ilala, watumishi kumi na tisa na mawakala wa ukusanyaji taka watoe maelezo ya kiasi cha bilioni kumi zilivyopotea na amewataka ndani ya siku sitini kiasi hicho cha fedha cha bilioni kumi ziwe zimerejeshwa Amos Makala Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amewataka madiwani kusimamia kwa uweredi fedha za serikali nae naibu meya wa jiji la ilala Sadi Kimji amemwahidi mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam watasimamia na kutekeleza maagizo na maelekezo aliyoyatoa.

habari Picha na Ally Thabiti