Habari picha na Ally Thabiti
Waziri wa Maliasili ANJERA KAILUKI amesema lengo la kufungua USHOROBA 61 ili Wanyama waweze kupita kwenye njia zao za Asili ambako wizara itaanza na kufungua USHOROBA 42 lakini USHOROBA 20 zipo kwenye mkakati wa kufunguliwa, ambako USAID wamenza kushughulikia USHOROBA 7 Tanzania inashughulikia USHOROBA 2.
Waziri AJENLA KAILUKI ametoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano zoezi la kufungua USHOROBA likianza nae kwa upande wake PROF wa Chuo Kikuu cha Dodoma JULIUS amesema sekta ya utalii inachangia pato la Taifa kwa asilimia 20% na inasaidia kuwezesha vijana wengi kujiajili na kuajiliwa ameipongeza Serikali kwa kuamua kufungua USHOROBA hapa nchini.
Habari na ALLY THABITI
Mwenyekiti wa Chama cha CUF Prof Ibrahim Lipumba amesema ofisi ya Taifa ya Takwimu imefanya kazi mzuri kwenye zoezi la sensa kwani matokeo haya yatasaidia kupanga mipango ya nchi nae kwa pande wake naibu katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Zanzibar SALUM MWALIMU ameitaka NBS kuweza kuboresha mifumo ya namna ya kupata taarifa ya matokeo ya sensa.
Habari na VICTORIA STANSLAUS
Kamisaa wa sensa na pia alikuwa spika wa Bunge la Tanzania ANNA MAKINDA amewataka wanasiasa nchini Tanzania kuyatumia matokeo ya sensa kwenye kazi zao, nae Mkurugenzi wa Sensa DEVOTHA MINJA amesema wanaenelea kutoa matokeo ya sensa kwa awamu tofauti tofauti kuanzia ngazi ya kata mtaa, wilaya, mkoa na Kitaifa amewataka wananchi kutumia matokeo ya sensa pamoja na viongozi wa kiasa.
Habari na Ally Thabiti
LHRC na wadau wa haki za binadamu wameamua kuweka mikakati yakupigania usawa wa haki za binadamu kwa makundi yote kuanzia ngazi za chini hadi za juu, wamesema haya katika maazimisho ya miaka 75 ya tamko za haki za binadamu
Habari kamili na Victoria Stanslaus Gaitan
Mkurugenzi mkuu mtendaji wa LHRC Dr. Anna Enga amesema kupitia miaka 75 ya tamko la haki za binadamu zimetolewa na umoja wa mataifa Tanzania imeweza kupiga hatua kwa kiasi kikubwa ikiwemo uhuru wa kujieleza haki ya kuchagua au kuchaguliwa uwemo wa mfumo wa vyama vyingi vya siasa Dr. Anna Enga amemtaka Rais wa Jamuhuri ya muungano ya Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassani kuweza kufanya maboresho kwenye sera na sheria ambazo kandamizi nchini Tanzania Mfano wa Sheria ya ndoa.
Dr Anna Enga amesema miaka 75 hii imefanya kundi la watu wenye ulemavu kupata haki mbalimbali ikiwemo haki ya Ajira, Elimu na zinginezo.
Habari picha na Ally Thabit
Mkurungezi wa Global Leadership Mbutho amesema mikakati yao kuweza kuyafikia makundi yote kwaajili ya kuwajengea uwezo wakuwa viongozi bora kundi la watu wenye ulemavu ni miongoni mwa mikakati yakuwapa elimu ya uongozi katika nchi 128 nchi 70 zinatoa mafunzo kwakutumia lugha za alama wenye uziwi kwa upande wasio ona wanamipango yakuweka maandishi ya nukta nundu.
habari picha na Ally Thabit
Naibu katibu mkuu wa wizara ya Ardhi, nyumba maendeleo na makazi Dr. Pendo Makokolo amesema Liberty Sparks utafiti walioufanya ni mzuri kwani serikali itatumia report hii walioizindua kwaajili ya kuboresha sera, sheria, kanuni na taratibu ambazo zinamnyima mwanamke haki ya kumiliki ardhi.
Dr. Pendo amepongeza kwa kusema kuwa watafanya maboresho na kwenye mabaraza ya ardhi lengo kuweza kuweka mifumo thabit ili mwanamke aondokane na manyanyaso na matesho anapodai haki ya kumiliki ardhi.
Habari kamili na Ally Thabit
Mwenyekit i wa Liberty Sparks ni vyema Serikali kuwapa elimu na uelewa wanawake waweze kumliki ardhi pia bunge litenge bajeti ya kutosha nakuweka mifumo rafiki kwenye mabaraza ya ardhi pamoja na mahakamaza. Yote haya yatafanyika migogoro ya Ardhi itapungua kwa kiasi kikubwa na wanawake watapa fursa yakuweza kumiliki ardhi
Mwenyekiti wa bodi wa taasisi ya LIBERTY SPAERK Dr Tumsifu amesema utafiti unaonesha kwenye ripoti yao asilimia 10% ya watanzania wanahati za Ardhi.
habari kamili na Ally Thabit
Evans ni mkurugenzi wa Liberty Sparks amesema wamefanya utafiti na kugundua kuwa wanawake wanakosa haki ya kumiliki ardhi nchini Tanzania hii yote kutokana na mila na desturi dhidi ya wanawake pia sheria ya mwaka 1967 haimpi haki mwanamke kumiliki ardhi hivyo upitia utafiti yaiomba serikali kuweka mazingira wezeshi ili mwanamke kumiliki ardhi ambapo mwanamke huyu itamsaidia kwa kiasi kikubwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi ikiwemo kulima na shughuli zinginezo.
habari kamili na Victoria Stanslaus
Dr. Samwel ni mshauri na mtafiti wa taasisi Liberty Sparks amesema wameamua kufanya utafiti kwa namna wanawake wanavyopata changamoto kwenye kumiliki Ardhi nchini Tanzania ambako kwa vijijini imekuwa ni tatizo kubwa sana ndio maana wameamua kufanya utafiti huu lengo serikali iweze kubadili sela, sheria, kanuni na taratibu kandamizi dhidi ya wanawake katika kumiliki ardhi.
Habari kamili na Ally Thabith
Mwakirishi kutoka Uganda John Samwel amesema mkutano ulioandaliwa na mtandao wa elimu nchini Tanzania utasaidia kwa kiasi kikubwa kukua kwa elimu Tanzania na Africa kiujumla.
Habari picha na Ally Thabith
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Dar es Salaam umeanza zoezi la kuwaondoa wapangaji waliolimbikiza madeni ya kodi ya pango.
Mkurugenzi wa TAMWA Dr Rose Rubein Amesema baada ya uzinduzi wa report TAMWA inamipango yakutoa elimu kwa wamiliki na wakurugenzi wa vyombo vya habari pamoja na mameneja lengo kuondoa maswala ya ukatili dhidi ya wanahabari wanawake kwenye vyombo hivyo pia TAMWA inawataka wanahabari wanawake kupaza sauti na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa.
Habari picha na Ally Thabit
Naibu waziri wa habari na teknolojia amesema TAMWA iongeze kasi kubwa katika kupambania kundoa ukatili vya habari kwa wanawake ambako ripoti waliotoa tamwa inaonesha asilimia 64% ya wanahabari ya wanaume wamepewa mikataba kwenye vyombo vya habari na wanawake asilimia 36% wamepewa mikataba huku asilimia 74% ya wanahabar wanawake wanafanyiwa ukatili wa kinondo kwenye vyombo vya habari.
anaipongeza tamwa kwa kazi kubwa wanayoifanya ikiwepo kushiriki kwenye mabadiliko ya sera, sheria, kanuni na taratibu na kuishauri serikali ya Tanzania ameitaka kuongeza idadi ya wanachama wao ambako kwa kipindi ambacho wanatimia miaka 36 wana wanachama 250.
Habari picha na Ally Thabith
Raisi mstaafu wa awamu ya nne Dr Jakaya Kikwete amepongeza mtandao wa elimu Tanzania kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kukuza elimu nchini naye kwa upande wake katibu mkuu wa wizara ya elimu Dr Charles Msonde amesema inashirikiana na mtandao wa elimu katika kuboresha miundo mbinu na kuwa jengea uzoefu walimu, naye mwenyekiti wa mtandao wa elimu Tanzania nae Dr Faraja Nyarandu amesema wameamua kuumpa tuzo Raisi Mstaafu Dr Jakaya Kikwete kwakuweza kukuza sekta ya elimu wakati akiwa Raisi na baada ya kustaafu nae mkurugenzi mtandao wa elimu amesema wanagusa makundi yote wakiwemo wenye ulemavu kwenye sekta ya elimu mfano ujenzi wa vyoo kutoa vifaa vya kujifundishia kwa wasioona.
Haya yote yamesemwa tarehe 27.11.2023 wakati wa ufunguzi wakongamano linalohusu maswala ya elimu ambako nchi saa zimeshiriki chini ya waaandaaji mndao wa elimu Tanzania.
Habari kamili na Ally Thabit
Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Dkt. Said A. Mohamed amesema kiwango cha ufanyaji mitihani kwa watu wenye ulemavu wa darasa la saba imeongezeka kupita wanafunzi 4583 kwa 2023 ambako kwa mwaka jana walikuwa 4221 pia amesema ufahuru wao umeongezeka kwa kiasi kikubwa hii yote ni kwaajili ya juhudi na jitihada zinazofanywa na Rais Dkt Samia Suluh Hassan kwa kujenga miundo mbinu rafiki na bora pamoja na vifaa kwa wanafunzi wenye uhitaji maarumu.
Ametoa wito kwa jamii kutowafungia ndani watu wenye uremavu wawapeleke shule ili wapate elimu.
Habari na Ally Thabiti
Mratibu wa THRDC Onesmo Eli Ngurumo amesema wataendelea kufanya kazi ya kuwatetea watetezi wa haki za binaadamu katika maadhimisho ya miaka 75 wameamua kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wanachuo kwa ajili ya kuweka nguvu katika kueondoa maswala ya ukatili wa kijinsia katika Tanzania. Nae kwa upande wake mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation Joseph Butiku amewataka wanaharakati kurudi nyuma katika kupaza sauti zidi wanaowakandamiza watu.
Habari na Victoria Stanslaus
Mtendaji Mkuu Daudi Kandolo wa Wakala wa Majengo Tanzania amesema tarehe 01/12/2023 watakusanya madeni kwa watumishi wanaoishi kwenye nyumba za wakala wa majengo ambao wanao daiwa kodi amesema kupitia kampuni ya Dalali ambako imepata mmlaka ya mahakama itakusanya madeni kwa watumishi wote ambao wamepanga na wanao daiwa kodi kwenye nyumba za TBA Tanzania nzima watakao shindwa kulipa watafukuzwa kwenye nyumba hizo na watapelekwa mahakamani ili waweze kulipa mikoa inayoongozwa kwa kudaiwa kodi na TBA Dodoma, Arusha na Mbeya.
Mtendaji Mkuu Daud Kandolo wa TBA amewataka wapangaji wote kutoa ushilikiano na zoezi hili litakuwa ndani ya mwezi mmoja ambako kiasi cha Bilioni 7.8 zitakusanywa na ile mikoa kinara inayodaiwa kodi Dodoma, Arusha na Mbeya itakusanywa Bilioni 1.4.
Habari na Ally Thabiti
Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa mfuko wa sawa kwa wote Justina wameweza kuwapa elimu wasichana 954 kwa kuwapa mafunzo ya tehama pia wameweza kutoa vifaa vya tehama kwa shule mbalimbali ikiwemo na shule za watu wenye ulemavu. mfuko wa mawasiliano sawa kwa wote imeweza kujenga minara 758 kwa Zanzibar wameshajenga minara 42 huku wakijenga miundo mbinu kwenye hospitali kwa ajili ya tiba mtandao, amesema lengo ni kujenga minara Tanzania nzima ambako mnara mmoja unajengwa kwa kiasi cha Milioni 350.
Habari na Ally Thabiti
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi amewataka mawaziri wa fedha wa afrika kuweza kuwawezesha wanawake fedha ili waweze kujikwamua kiuchumi
Pia amewataka mawaziri wa Afrika wa wizara ya maendeleo ya jamii kuwatafutia wanawake fursa za uwekezaji kwenye sekta mbalimbali ili wajikwamue kiuchumi waondokane na maswala ya ukatili wa kijinsia huku wakizitaka nchi hizo kupitia kwenye mabunge yao kutenga bajeti wenye usawa wa kijinsia na kuweka sera bora kwaajili ya wanawake naye waziri wa Mwigulu Mchemba amesema kupitia mkutano huu Tanzania itajifunza namna ya kuwainua wanawake kiuchumi pia nitahamasisha nchi nyingine zitenge bajeti zenye usawa wa kijinsia kama ilivyo Tanzania kwaupande wake waziri wa maendeleo ya jamii Dr. Doris Gwajima amempongeza Rais Dr. Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kuwainua wanawake kiuchumi, watu wenye ulemavu vijana, wazee na makundi mengineyo na kwakuweza kutenga bajeti yenye mlengo wa kijinsia na kuwepo kwa sera na sheria rafiki kwa wanawake na makundi mengineyo.
habari kamili na Ally Thabit
Mwanaharakati Anna Kipya amesema TGNP imefanya kazi katika kuleta uchechemuzi wa mabadiriko ya usawa wa kijinsia mpaka ukatiri umepungua Tanzania.
Habari kamili na Ally Thabith
Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengelo amesema wakazi wanaoishi mbonde mto msimbazi, jangwani na magomeni mtaa wa sunaa watapewa kiasi cha milioni nne ikiwa ni fidia kwaajili ya kupisha mradi wa bonde la mto msimbazi.
habari kamili na Ally Thabith
Mwenyekiti wa Bodi TGNP kushirikiana na ASAS za kiraia waitaka serikali kuweza kulejesha mchakato wa katiba mpya, kutenga bajeti yenye mlengo wa kijinsia kutoa sheria za ndoa za utotoni aya yametolewa kwenye kilele la tamasha la kinsia mabibo jijini Dar es Salaam 10/11/2023.
Habari na Ally Thabiti
Program Maneja wa Magonjwa yasiyoambukiza wa wizara ya Afya Dr. Varelia Milinga amewataka watu kujitokeza kwa wingi vinjwa vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupima afya zao bure na kupewa matibabu pamoja na elimu namna ya kukabiliana na magonjwa yasio ambukiza kwa upande wao NHIF wamesema magonjwa yasiombukiza yanatumia fedha nyingi sana katika matibabu kwa mwaka 2021 - 2022 kiasi cha fedha ya Kitanzania Bilioni 32.4 zimetumika kutibu magonjwa ya Kansa ukilinganisha na nyuma kiasi kilikuwa kidogo, kwa upande wa magonjwa ya fido zimetumika Bilioni 35.4 ukilinganisha na miaka ya nyuma NHIF wametoa witoa wito kwa jamii wajiunge na bima za afya.
Habari na Ally Thabiti
Waziri wa Maendeleo ya jamii Doris Gwajima amesema tarehe 15 - 17 /11/2023 mawaziri 22 kutoka nchi za Rwanda, Zambia, Uganda na zinginezo wanakutana jiji Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili maswala ya usawa kijinsia pamoja na kuweka mikakati ya uwekezaji katika maswala ya kijinsia, nae Waziri wa Fedha Mwigulu Mchemba amesema kwenye mkutano huu mawaziri wa fedha watajadili namna gani ya kutenga bajeti zenye usawa wa kijinsia kwenye nchi zao.
Habari Ally Thabiti
Omary Kumbilamoto Mstahiki mea wa Jiji la Dar es Salaam amewataka wananchi wote wa Dar es Salaam na mikoa jirani wajitokeze kwa wingi kupima afya zao na kupata huduma bure kwa magonjwa yasioambukiza viwanja vya mnazi mmoja kuanzia tarehe 14/11/2023 mwisho tarehe 18/11/2023 pia kutakuwepo na utoaji wa elimu wanamna kukabiliano na magonjwa yasiyoambukiza mfano kansa, Figo, Kisukali, Presha na mengineyo.
Omary Kumbilamoto ameshukulu wizala ya afya kwa kutoa huduma hii bure kwani wataokoa maisha ya watu wengi pia amemshukuru mweshimiwa Rais Dr. Samia Saluhu Hassan kwa kuweka kutoa vifaa tiba kwa wizara ya afya.
Habari picha na Ally Thabiti
Aliyekuwa Makamo wa Rais nchini Afrika Kusini mwaka 2005 na mkurugenzi mkuu wa UN Woman mstaafu Bi. Phumzile Mlamdongeuka amesema TGNP Mtandao katika kuhazimisha miaka 30 tangu iazishwe mwaka 1993 imeweza kuwakomboa wanawake zidi ya ukatili wa kijinsia pia imewezeshe mabadiliko ya sera, sheria na miongozo iliyokuwa kandamizi nchini Tanzania zidi ya wanawake kufutwa pia imewajengea uwezo wanawake kugombea nafasi mbalimbali na kuwa viongozi nchini Tanzania pia ameutaka uwongozi wa TGNP Mtandao nchini Tanzania kwenye tamasha lao la 15 liendelee kupaza sauti zidi ya mila na destuli potofu na kandamizi kwa wanawake.
kwa upandewake mkurugenzi mkuu mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi amesema wameweza kupaza sauti ya pamoja katika kupinga ubaguzi, ukatili, na unyanyaswaji wanawake nchini Tanzania, tamasha la TGNP Mtandao limeweza kuwafikia watu elfu 35 Tanzania nzima na watu elfu 7 kwenye wilaya 32, kwenye kanda zote sita watu 1500 wamefikiwa kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi wa TGNP Mtandao gema akilimali amewataka watanzania na wasio watanzania kuweka nguvu za pamoja katika kumkomboa mwanamke nae mkurugenzi mkuu mtandaji wa Woman Found Bi. Rose Malando ametaka asasi mbalimbali kuweza kutumia na kuzitafuta fedha kwa ajili ya kuweza kumkomboa mwanamke kielimu, afya, ardhi na maji. Ambako kiasi cha dola za kimarekani bilioni tano nukta sita ziliweza kutolewa kwaajili ya kufanya harakati ya kumkomboa mwanamke.
Habari na Ally Thabiti
Mkurugenzi Mkuu wa Elimu kwa Uma na mawasiliano TRA Richard Kayombo amesema tarehe 24/11/2023 watatoa tuzo kwa walipa kodi nchini Tanzania mgeni rasmi Naibu Waziri Mkuu Dr. Dotto Biteko tuzo hizi zitatolewa Mlimani City lengo la kutoa tuzo hizi ni kuwamasisha watu kulipa kodi kwa hiari. Kauli mbiu inasema Kodi kwa maendeleo tuwajibike, Richard Kayombo amesema tarehe 09/11/2023 jumla ya shule hamsini na tisa (59) zitafanya mjadala kuhusu maswala ya kodi kwenye chuo cha kodi lengo la kuwashilikisha wanafunzi kuwajengea uwezo na uwelewa ili wawe walipakodi wazuri baadae, Tarehe 18/11/2023 kutakuwa na mbio za kilometa 5 na 10 ambako zitafanyika katika viwanja vya Jimkana bule.
TRA imetoa wito kwa wadau wote kushiriki kwenye mbio hizi
habari na: Ally Thabiti
Kaimu mtendaji mkuu wa benki ya TIB ametoa wito kwa wanahabari pamoja na wahariri wa vyombo vya habari kuitangaza vyema benki ya TIB kwani inawezesha katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania mfano wakulima elfu kumi wamepata ajila kupitia benki ya TIB amesema haya wakatika akizungumza na wanahabari pamoja na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Habari picha na Ally Thabiti
Mr. William Batambi mkuu wa kitengo idara ya mawasiliano na mahusiano kwa huma DART amesema ifikapo tarehe 20/10/2023 Dala Dala zinazoenda feri eneo la kivukoni azitoruhusiwa kufika eneo hilo ila mabasi yaendayo haraka ndiyo yatakayo ruhusiwa tu pamoja na bajaji maelekezo haya yametolewa kwa sababu kuna maboresho ya kituo cha mabasi yaendayo haraka kwa ajiri ya hawamu ya pili ya mladi ya mabasi ya Mbagala, awamu ya tatu mabasi ya Gongo la mboto, awamu ya nne mabasi ya Tegeta.
Habari picha na Ally Thabiti
Dr ameitaka jamii kuzingatia matibabu ya tiba Shufaapia ameeleza Magonjwa pia amesema seratani ya shingo ya kizazi ndio inaongoza kwa wanawake kwa asilimia 95 saratani ya matiti 15 , saratani ya Ngozi asilimia 10, watu wajitokeze kupata tiba shufaa Dr julius ameongeza na kusema anampongeza sana Mh Rais Dr Samia Suruhu Hassani kwa kuweza kuweka fedha nyingi kwenye sekta ya Afya .
Ametoa wito kwa jamii kuweza kupima Afya zao mara kwa mara pia wawe na Bima za Afyan kwani matibabu ni Gharama mno.
Tiba Shufaa iliaza kuazimishwa 2005 kila ifikapo mwezi wa kumi wiki mbili za mwazo , Dunia uwazimisha huduma za tiba shufaa., kwa tanzania imeazimishwa 14/10/2023 Hospital ya Ocean road.
Habari Picha na Ally Thabiti.
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Dunstan Kitandula ameutaka uongozi wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kuwa na mikakati ya kusambaza miche ya miti ya matunda katika maeneo ya shule za Msingi na Sekondari nchini.
Wizara ya Ardhi Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema inahakikisha inatatua kero ya migogoro ya Urasmishaji wa ardhi inayowakumba wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam inamalizika katika kipindi kifupi.
Hayo yamesemwa leo na Waziri huyo wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mkoani Dar es salaam Jerry Slaa ambaye aliitwa jijini humo na Kamati Tendaji ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Dar es Salaam.
Katika kikao hicho kilichohudhuliwa na wataalamu wa ardhi kutoka halamshauri za Mkoa huo,kwa lengo la kujadili namna ya kuondoa tatizo la kero za urasmishaji wa ardhi zinazofanywa na baadhi ya makampuni binafsi ambayo yanakusanya fedha kutoka kwa wananchi huku yakishindwa kutekeleza majukumu yake.
"Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Watendaji wake kushughukia kero ya Urasmishaji wa ardhi inayowakumba wananchi wa Mkoa huo,"amesema Slaa.
Amsema Serikali imepanga kupima na kutoa hati za ardhi milioni mbili na laki tano(2.5 milioni) kufikia 2025,hivyo lengo la serikali ni kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi,kwa mikoa yote ishirini na sita(mikoa 26) nchini na kuna makamishna wa ardhi wanaotoa hati ,hatua hiyo inayosaidia wananchi kupata hati zao bila usumbufu.
Waziri Slaa ametoa muda wa siku saba kwa watendaji wa Wizara ya Ardhi kuhakikisha wanatatua kero hiyo kwa mkoa wa Dar es Salaam nakwamba baada ya hapo warejeshe majibu kwa viongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Dar es salaam.
"Maelekezo yangu ya utatuzi wa kero ya Urasmishaji ni kuwa ,Naibu katibu Mkuu na Watendaji wenzako mlete taarifa kwa viongozi wa chama,kama kuna tatizo la fedha niambie ili tuone tunapata wapi fedha ili muweze kukamilisha kazi hii" amesema Waziri Slaa.
Aidha Waziri Slaa amesisitiza kwamba hataki kuskia kero za urasmishaji wa ardhi zinaendelea kujitokeza katika uongozi wake ambapo amesisitiza makampuni yanayojihusisha na urasmishaji huo yanapaswa kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na yale yatakayoenda kinyume yachukuliwe hatua za kisheria .
Ameongeza kusema kwamba "Urasmishaji umekua tatizo kubwa katika simu kumi anazopigiwa na wananchi simu saba hadi nane zinahusu malalamiko ya urasmishaji wa ardhi.
"Nimekuja na timu yangu inayohusika na mambo ya ardhi napenda kuagiza kuhakikisha kero hizi zinashughulikiwa haraka sana".
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam Abass Mtemvu katika kikao hicho cha kamati tendaji cha CCM amesema kwamba Mkoa wa Dar es salaam umekua na tatizo la urasmishaji kutokana na kazi hizo kupewa makampuni binafsi ambayo yanakusanya fedha za wananchi nakutokomea nazo bila kufanya kazi hiyo kwa wakati.
Amesema kuwa kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa waliona kumwita mheshimiwa Waziri wa Ardhi kuzungumzia tatizo hilo.
Katika kikao hicho madiwani,wakuu wa wilaya na wataalamu wa ardha walifika tayari , kupokea maelekezo ili kuondoa tatizo hilo.
Kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Israel na maeneo mengine ya jirani, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa mpango wa kuwarejesha nchini Watanzania waliopo nchini humo na maeneo mengine ya karibu.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema, Serikali imefikia uamuzi huo baada va kufanya tathmini na kujiridhisha kwamba mazingira ya sasa yanaruhusu zoezi hilo kufanyika.
“Hivyo, Watanzania walio tayari kurejea nyumbani wanashauriwa kujiandikisha kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Tel Aviv, Israel kupitia barua pepe: telaviv@nie.go.tz au simu namba: +972 533 044 978 na +972 507 650 072, kabla ya tarehe 15 Oktoba 2023, saa
6 usiku”
Mfanyabiashara maarufu wa maduka ya simu jijini Arusha aliyefahamika kwa jila moja la Mallya amekutwa amefariki kwenye gari yake katika eneo la Maegesho ya Magari (CITY CAR WASH)huku mwili wake ukiwa umeharibika.
Tukio la kugundulika kwa mwili wa marehemu limetokea mapema leo baada ya waosha magari kusikia harufu kali iliyokuwa ikitoka ndani yagari hilo Askari polisi walifika eneo la tukio na kuukuta mwili huo uliokuwa kwenye gari aina ya SCUDO lenye namba T 466 AUB lililokuwa limeegeshwa katika eneo hilo.
Baadhi ya mashuhuda walidai kuwa marehemu Malya amekuwa na desturi ya kufika eneo hilo na kuegesha gari lake na kisha kwenda bar iliyopo eneo hilo kwa ajali ya kula chakula na kunywa.
Mwenyekiti wa eneo hilo maarufu kwa wauzaji wa magari (madalali) ,Alex Kahel alisema alipata taarifa asubuhi ya leo oktoba 13, kuhusiana na tukio hilo na baada ya kufika aliweza kulitambua gari hilo kuwa ni mali ya mfanyabiashara huyo.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muuungano na Mazingira, Seleman Jaffo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe mkoani Pwani, amekabidhi mifuko 600 ya sarufi kwa madiwani wa kata za wilaya hiyo kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Shikizi.
Aidha Waziri Jaffo ametoa mitungi ya gesi 126 kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya na mkoa ikiwa ni jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kutunza mazingira.
Waziri Jaffo amekabidhi mifuko ya saruji na mitungi ya gesi kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya kilichohudhuriwa na Katibu wa Chama hicho Mkoa Waziri Jaffo alisema lengo ni kuunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira mazuri.
Amesema tayari katika Jimbo la Kisarawe Shule zimejengwa katika maeneo mbalimbali na ni shule nzuri,ila kwa baadhi ya vitongoji bado hivyo wanaendelea na mchakato huo kuhakikisha kila kitongoji kinakuwa na shule shikizi.
“Leo nimetoa mifuko ya cement kwa shule 4 ambapo kila moja imepata matofali 150 yatasaidia kufyatulia matofali na kuanza ujenzi wa madarasa hata mawili mawili,”amesema na kuongeza
“Hii ni kuonesha Wananchi ni namna gani Chama cha Mapunduzi kinavyotekeleza ilani zake na kuhakikisha kila kitongoji kinapata shule hata vile vitongoji vya mbali kama cha Kimelemeta,”amesema.
Katika kikao hicho, hoja mbalimbali ziliibuliwa zenye lengo la kuboresha huduma kwa wananchi likiwemo suala la maji katika kata sita, Katibu wa CCM mkoa, Bernard Ghaty anatoa maelekezo.
Kwa upande wake Katibu wa CCM mkoa wa Pwani,Bernard Ghaty amesema kipindi wanatoa ahadi katika ilani ya CCM waliwaambia Wananchi watadhibiti ukataji wa miti hovyo na kutengeneza mazingira ambayo ni Suluhu.
Alisema kwa vitendo Waziri Jaffo ameweza kutekeleza agizo hilo kwa kuhakikisha amegawa majiko ya gesi kwa watendaji wa CCM pamoja na wadau wengine ili wakawe mifano kwa watu wengine kuhakikisha wanatunza mazingira.
“Ni jambo la heshima,msingi na kuigwa kw akufata mfano wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha nchi inatunza mazingira na kuiga mfano wa Waziri Jaffo katika kuhakikisha
Mtaalamu wa Maabara wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Bw. Peter Mwevila amesema swala la mawasiliano baina ya watoa huduma za afya ni muhimu katika kupata vipimo sahihi vya mgonjwa.
Bw. Mwavila ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo katika majengo ya Taasisi ya Saratani Ocean Road alipokuwa akiwasilisha mada inayosema “Sample Collection” katika uwasilishaji wa “Continues Medical Education” (CME).
Aidha Bw. Mwevila ameongeza kuwa katika uchukuaji wa “sample” kutoka kwa mgonjwa ni lazima kuzingatia maelekezo ya kila kipimo kinachohitajika kwa kuwa kila kipimo kina utaratibu wake.
Pamoja na hayo Bw. Mwevila ameongeza kuwa iwapo sample imecheleweshwa kufikishwa kwenye maabara au “sample” imehifadhiwa katika kifaa kisicho sahihi, itabidi kuchukuliwa “sample” nyingine ili kupata vipimo hitajika.
Taasisi ya Saratani Ocean Road imekuwa ikitoa fursa kwa idara na vitengo vya ndani na nje ya Taasisi katika kuwasilisha mada mbalimbali kwa watumishi wake, ili waweze kujenga uelewa wa pamoja.