Friday, 28 July 2023

STELLA REZAULA AELEZEA IMOPHIRIA



Raisi wa imophiria nchini Tanzania Stella Rezaula amesema kati ya watu elfu kumi moja mmoja ana imophiria amesema pia mpaka sasa hospitali saba zinatoa huduma za imophiria tena bure kuanzia vipimo mpaka matibabu ambapo ni hospital ya rufaa ya mbeya KCMC hospitali ya benjamini mkapa Dodoma, Muhimbili, Kigoma mawenzi na zinginezo.

Stella Rezaula amesema asilimia ya 70% ya imophiria ni wakurithi pia amesema kuna utofauti wa kati imophiria na selimundu ametoa wito kwa serikali waendelee kusaidia matibabu ya ugonjwa huu pia ameitaka jamii kujitokeza kwa wingi kupima imophiria.

habari picha na Ally Thabiti

TANESCO YAWAKIKISHIA WATEJA WAO UMEME WA UHAKIKA





Naibu mkurugenzi wa uzalishaji umeme TANESCO mwandisi Pakaya amesema shirika la umeme nchini Tanzania (TANESCO) linafanya kazi kubwa ya kuzalisha umeme wa kutosha kwa wateja wao ambapo asilimia 35% umeme unazalishwa na maji na asimilia 65% umeme unazalishwa na gesi hivyo amesema bwawa la mwalimu nyerere likikamilika uzalishaji wa umeme utakuwa mkubwa sana naye kwa upande wake mkurugenzi wa huduma EXPERIENCE Bw. Martin Mwambene Amesema Tanesco sasa hivi inatatua changamoto za watu kwa haraka zaidi kwa kutumia namba za simu lakini pia imesambaza watendaji kazi wao wa pikipiki, Bajaji kwa maeneo ambayo magari hayafiki amesema haya Serena Hotel wakati wakiwa na wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari huku mwenyekiti wa baraza la wahariri ndugu Barire amelipongeza shiurika la Tanesco kwa ufanisi wao mzuri pia kwakuweza kutekeleza miradi yao kwa wakati.

Habari picha na Ally Thabith

TANESCO YAZINDUA MPANGO WA JINSIA (GENDER WORK PROGRAM) WA MIAKA MINNE

 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kupitia mradi wa kusafirisha umeme mkubwa kutoka Tanzania hadi Zambia (TAZA).

 

Progamu hii imezinduliwa na Mgeni Rasmi na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato ukiwa na lengo la kutatua changamoto wanazokutana nazo wafanyakazi wanawake katika maeneo yao ya kazi na kuongeza uwiano wa utendaji kazi baina ya wanawake na wanaume kati ya mwaka 2023 hadi 2026.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Mhe. Byabato alisema TANESCO imejizatiti kwa kiasi kikubwa kwenye usawa wa kijinsia na kuitaka menejimenti ya Shirika hilo kuhakikisha inaanzisha kitengo maalumu cha jinsia ili kuwepo na uwanja mpana wa kujadili masuala ya kijinsia.

 

“Naiagiza menejimenti ya TANESCO kupitia mradi wa TAZA kuhakikisha wanawake wanapewa kipaumbele sawa na wanaume na kuongeza fursa zaidi kwa wanafunzi wa vyuo ambao wanajiandaa kuajiriwa kwenye ajira rasmi”.

 

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Maharage Chande alisema, “Sisi kama TANESCO swala la kijinsia lipo juu kabisa katika agenda zetu. Wakati tunaanda mkakati wa Shirika, tuliainisha vipaumbele saba na katika kipaumbele cha kwanza kilikuwa ni kipaumbele cha watu na tuliweka masuala ya usawa wa kijinsia na hususani tuliweka mikakati ya kuhakikisha tunaongeza  viongozi wanawake katika Shirika letu”.

 

Ameyataja maeneo ya kipaumbele kuwa ni pamoja na sera ya Shirika kutoa kipaumbele kwenye masuala ya jinsia, upatikanaji wa taarifa sahihi za masuala ya jinsia kwenye taasisi na kuwepo kwa nafasi za mafunzo ya ukuzaji taaluma kwa wafanyakazi wanawake hasa wanaofanya kazi za kiufundi ili kuwajengea uwezo kupitia mpango wa mafunzo kazini.

 

Akifunga uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Fedha wa TANESCO, CPA Renata Ndege alisema nafasi za wanawake kwenye Shirika zipo nyingi isipokuwa wengi wao wanakosa ujasiri wa kupambanania nafasi husika na wanafanyakazi wanaume.

 

Aidha, amepongeza hatua ya uanzishwaji wa kitengo maalum cha kushughulikia mambo ya jinsia kwani kitendo hiki kitaongeza kasi kwa wafanyakazi wanawake kuwepo kwenye nafasi mbalimbali za uongozi.

 

Mradi wa upanuzi wa njia ya kusafirisha umeme mkubwa wa kilovoti 400 kutoka kituo cha kupokea, kupoza na kusairisha umeme cha Tagamenda Iringa nchini Tanzania kwenda Zambia (TAZA) na nchi nyingine zilizopo Kusini mwa Tanzania kupitia Kisada Iringa, Iganjo Mbeya na Nkangamo Tunduma Songwe unatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia mkopo wa Jumuiya ya  Maendeleo ya Kimataifa (IDA) ya Benki ya Dunia, mkopo wa Mfuko wa Maendeleo wa Ufaransa (AfD), Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


habari kamili na Ally Thabith

Wednesday, 19 July 2023

WAZIRI WA MADINI AKUTANA NA CHEMBA YA MADINI

Waziri Dr Doto Biteko amesema lengo lakukutana na chema ya madini ili kutatuwa kero zinazo wakabiri wanachama wa chema hii ya madini, kero hizo ni wingi wa kodi, tozo, mwingiliano wa Sheria mfano mizara ya Mali asiri na utalii ambapo wanazuia uchimbaji wa madini kwenye hifadhi na mbuga  hata hivyo Dr Doto Biteko amempongeza na kumshukuru mwenyekiti wa chema ya madini pamoja na wajumbe wake kwa namana wanavyotoa ushirikiano kwenye serikali yao mpaka kupelekea secta hii kukua kwa kiwango kikubwa na kuongezeka kwa mapato.Waziri Dr Doto Biteko ametoa wito kwa jamii na kwa wachimba madini  kulinda na kuhifadhi Maliasiri za Tanzania. pia amewatoa hofu chemba ya wachimba madini kuwa sheria zenye mwingiliano zitafanyiwa kazi.Naye kwa upande wake mwenyekiti wa chemba ya wachimba madini amempongeza serikali na kuishukuru  kwa kutatua kero za wachimba madini kwa kazi kubwa. 


Habari picha na Ally Thabiti. 

Sunday, 16 July 2023

BILL NAS KUPAGAWISHA SIKU YA MWANANCHI

 




Msanii wa kizazi kipya Bilnasi amesema tarehe 22/07/2023 atafanya show ya kibabe katika uwanja wa benjamini mkapa ambako TIMU ya YANGA itacheza na Kaizer Chiefs hivyo amewataka watu wajitokeze kwa wingi.

Habari picha na Ally Thabit



LATRA CCC YAJA KIVINGINE MAONYESHO YA 47


 


Bi Fatuma Kiongozi amesema kwenye maonyesho ya sabasaba ya 47 wanatoa elimu kwa watu wenye ulemavu pia wametoa vitabu vya maandishi ya nukta nundu kwaajili ya wasio ona vilevile LATRA CCC inatoa elimu shule msingi, secondari na vyuo vikuu lengo kupunguza ajari barabarani kwa wanafunzi na hili wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa .

Amesema haya Jiji Dar es Salaam kwenye maonyeso ya Sabasaba ambayo ya 47 kwenye jengo la Jakaya Kikwete.


Habari kamili na Ally Thabit

STEVE NYERERE HAIMIZA MICHANGO YA MADAFTARI

 Steven Nyerere mwenyekiti wa taasisi ya mama ongea na mwanao kwa kushirikiana na taasisi ya yoge wanawataka watu kujitokeza kwa wingi kuchangia madaftari kwaajili ya wanafunzi.

Habari kamili na Ally Thabith

MKURUGENZI WA BANDARI AELEZA FAIDA ZA UJIO WA DP WORD

 


Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) amesema faida zitakazopatikana kupitia mwekezaji wa DP word kwenye bandari nchini Tanzania tutaweza kusafirisha mazao ya kilimo mfano mbogamboga, matunda, pamoja na mifugo hivyo amewataka watanzania kuunga mkono ujio wa muekezaji DP WORD kwani sekta ya uchukuzi na usafirishaji wa majini na nchi kavu utakuwa wa kiwango kikubwa na ajira zitaongezeka kwa kasi zaidi.

Amesema haya jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano kati ya wahariri wa vyombo vya habari pamoja na timu iliyopewa mamlaka ya kusimamia mkataba ambapo chini wa waziri Prof. Makame Mbarawa 


Habari Kamili na Ally Thabit

Thursday, 6 July 2023

SIDO YAJA NA MASHINE ZA KUTENGENEZEA JUISI YA MIWA BORA ZAIDI



 Sido imeamua kuja na mashine za kutengenezea juisi ya Miwa zenye ubora na bei nafuu lengo kuwakwamua watu kiuchumi ili wajiajili na waajiliwe kama inavyoonekana picha kwenye banda la SIDO ndani ya viwanja vya sabasaba kwenye maonyesho ya sabasaba  yanayofanyika jiji Dar es Salaam SIDO inawakalibisha.

Habari Picha na Ally Thabiti

SIDO YAWAKUZA WANAWAKE KIUCHUMI


Sara Kijacho ni Kampuni ya Kitanzania ambayo inatengeza bidha za vipodozi ambako kampuni hii imepata mafunzo kupitia SIDO na kutafutiwa masoko ya kitaifa na Kimataifa.

Asema haya kwenye maonesho ya 47  ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.



 Habari Picha na Ally Thabiti

SIDO YAWAFUTA MACHOZI WANAWAKE

Kupitia kampuni ya Uhuru Sanitary Pads imeshilikiana na SIDO katika kutengeneza pads za kike zenye bora na gharama nafuu lengo kumsadia mwanamke kipindi cha hedhi kujistili. Mwanakiputi amesema anaishukuru sido kwa kuwatafutia masoko pamoja na wateja amesema pads zao wanatengeneza kibaha mkoani pwani.

Asema haya kwenye maonesho ya 47  ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na Ally Thabiti


 

TANFOAM YAJA NA BIZAA BORA VIWANJA VYA SABASABA


Bi Glorious Temu  mkuu wa masoko na mauzo Kampuni ya Tanfoam iliyopo Arusha amesema kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 47 Kampuni yao imekuja na magodoro bora na imala, mito pamoja na folonya zake vitanda springi ambazo avimuumizi mtu pia amesema wanapatikana Arusha, Mbeya, Shinyanga, Mwanza, Musoma na Dar es Salaam. Tanfoam ilianza mwaka 1966 ambako kaulimbiu ina sema ambako alinunua babu na mjukuu anatumia. 

Asema haya kwenye maonesho ya 47  ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na Ally Thabiti



 

DIASPORA WAIMIZWA KUWEKEZA ZANZIBAR


Afisa anayesimamia Wazanzibari waishio nje ya nchi (Diaspora) amewataka waendelee kuwekeza ndani ya Zanzibar katika sekta ya Afya, Elimu na zinginezo pia amewapongeza wana Daispora kwa kuweza kutoa michango ya fedha kwa serikali ya Zanzaibar, ametoa lai kwa wanadaispora kuweza kujisajili kwa wingi hili wajue database. Asema haya kwenye maonesho ya 47  ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na Ally Thabiti

 

RAIS MWINYI HAAMUA KUWASILIKIZA WANANCHI WAKE





Afisa Msaidizi wa Mladi wa sema na Rais Mwinyi amesema lengo la kuja na mradi huu kutoka ofisi ya Rais Mwinyi ni kukusanya kelo na maoni zinazowakabili wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara, wanatoa eleimu kupitia TV, Redio na Njia Zinginezo. Asema haya kwenye maonesho ya 47  ya SABASABA Jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na Ally Thabiti





 

SIDO YAJA KUWAGOMBOA WAJASILIA MALI


 

Technician kutoka SIDO Bwana Onest Mwegi amesema lengo la SIDO kuja na mashine mbalimbali kwaajili ya kuwauzia watu kwa bei nafuu ili wajikwamue na uchumi, amesema haya kwenye maonyesho la 47 ya SABASABA jijini Dar es Salaam.

Habri Picha na Ally Thatbiti

Tuesday, 4 July 2023

KINANA ATUNUKIWA NISHANI YA UONGOZI.

 MWENYEKITI aliyemaliza muda wa uongozi katika Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Ndg. Abdulrahman Kinana, ametunukiwa nishani ya uongozi bora wa kipindi cha mwaka mmoja alipokuwa mwenyekiti wa taasisi hiyo.

Nishani hiyo imekabidhiwa  kwa niaba ya Viongozi wakuu wa Vyama wanachama Wa TCD na Mwenyekiti mpya wa TCD, Profesa Ibrahim Lipumba, katika mkutano wa viongozi wakuu wa vyama wanachama wa TCD, uliofanyika Julai 3, 2023, katika ofisi za TCD, Dar es Salaam.

Kabla ya kumkabidhi nishani hiyo, Profesa Lipumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, alisema kuimarika kwa TCD kwa sasa kunatokana na mchango wa kipekee wa Ndg. Kinana ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.

“Kwa niaba ya wakuu wenzangu wa vyama vya siasa wanachama wa TCD, uongozi Ndg. Kinana umetuwezesha kutuunganisha sisi wote, tunakukabidhi nishani hii iwe kumbukumbu kwa kazi yako nzuri, asante sana,” alisema Profesa Lipumba.

Viongozi wengine wa vyama vya siasa ambavyo ni wanachama wa TCD waliohudhuria mkutano huo na kushuhudia Ndg. Kinana akitunukiwa nishani hiyo ni Mwenyekiti wa Chadema, Ndg. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Haji Ambar, Mwenyekiti wa CHAUMMA, Ndg. Hashim Rungwe, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Juma Duni Haji pamoja na Makatibu Wa Kuu wa Vyama hivyo.

Ndg. Kinana alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TCD, Aprili mwaka 2022 kwa kipindi cha miezi sita, na baadaye wakuu hao wa vyama walimuongezea muda wa uongozi kwa kipindi kingine cha miezi sita baada ya kufanyika marekebisho ya katiba ya TCD. 

habari kamili Ally Thabit

MGOMO WA MADEREVA WA DALADALA WASABABISHA KUKWAMA KWA SHUGULI JIJINI ARUSHA.

 


Katika picha ni wakazi wa jiji la Arusha wakisubiri nakuona namna rahisi ya kuwafikisha makazini na kwenye shughuli mbalimbali za kiwaoatia riziki

NA. VERO IGNATUS, ARUSHA

Madereva wa Magari ya kubeba abiria katikia Jiji la Arusha maarufu kama Daladala wametangaza kusitisha huduma hiyo wakidai shughuli zao kuingiliwa na Watoa huduma za Usafiri wa Pikipiki za Magurudumu Matatu maarufu kama Bajaji.

Aidha Madereva hao wamedai kwamba hawatotoa huduma hiyo hadi pale Mamlaka za Jiji la Arusha zitakapopata ufumbuzi wa suala hilo,

Mgomo huo umeshuhudiwa katika Siku ya leo Jumatatu na kuonekana kuathiri huduma za Usafiri hususani kw Wafanyakazi,Wafanyabiashara pamoja na Wanafunzi ambao wamefungua Shule.

Akizungumzia mgomo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro, Locken Adolf amesema kuwa utitiri wa bajaji umeathiri biashara ya daladala hivyo wanaiomba serikali kuzipunguza.

“Ukubwa wa eneo la Arusha, hazitakiwi kuzidi zaidi ya 100 lakini sasa zimekuwa nyingi na zimekuwa kero sana na zimeteka ruti zote za daladala. Pia zinafanya biashara ya kupakia abiria kama wanavyofanya wenzao jambo ambalo siyo makubaliano wakati zinaingia mjini,” amesema

Akitoa dukuduku lake mmoja abiria, Maria Pallagyo amesema mgomo huo umeanza leo asubuhi umesababisha shida kwao pampja na wanafunzi ambao wanatakiwa kwenda mashuleni,pampja na wafanyakazi,wafanyabiashara amabao wanawahi masokoni

“Tunaamini kuwa serikali yetu ni sikivu,na sidhani kama itaacha wananchi wake wateseke namna hii ,tunaiomba itafute suluhu ya jambo hili kwani tunaoteseka ni kwa suala la daladala kugoma imekuwa siyo mara moja,yaani kwetu ni mateso tu amesema Maria.

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra), Mkoa wa Arusha, Amani Mwakalebela amesema kuwa wamesikia mgomo huo na wanaendelea na taratibu za kushughulika na madai ya madereva hao wa daladala, kuona namna gani watataua changamoto hiyo .

Mwakalebela amesema kumekuwa na ongezeko la bajaji ndani ya Jiji la Arusha hasa ruti za Sombetini-Ngusero, pia njia ya Majengo, pamoja na ile ya Uswahilini -Dampo ambapo wameanza kuchukua hatua kuona ni namna gani wataweka mambo yakae sawa

“Kutokana na ongezeko la bajaji ambapo katika 350 zilizosajiliwa na zoezi kufungwa lakini zipo zaidi ya bajaji 2,000 ambazo zinafanya kazi na kugeuka kero, hivyo tulichoamua ni kuomba oda ya mahakama kuzipiga mnada bajaji ambazo tutazikamata hazina usajili . Alisema Mwakalebela

Mgomo huo umemuibua Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro, Locken Adolf ambapo amesema kuwa kumekuwa na utitiri wa bajaji umeathiri biashara ya daladala hivyo wanaiomba serikali kuzipunguza, ili daladala nazo ziweze kuingiza kipato.

habari picha na Ally Thabith

SIDO YAUNGA MKONO MRADI WA VIJANA NAHODHA


 Binti anawataka watanzania kununua viatu vyake ambako yeye ameshikwa mkono na mradi wa vijana nahodha pia anawapongeza SIDO kwa kuwatafutia masoko.

Habari picha na Ally Thabith

VETA YAJA NA BIDHAA YA NGOZI MAONYESHO YA SABABA


Hamadi ni mwalimu wa veta amewataka watu kutumia bidhaa zake za ngozi kwani zinaubora pia amewataka watu kutembelea viwanja vya sabasaba ili wanunue viatu vya ngozi, mabegi na bidhaa zinginezo wanazo uza.

Habari picha na Ally Thabith


VETA YAJA NAMASHINE ZA KUBADILI MAZIWA

 


Mwalimu wa maswala ya umeme kutoka chuo cha VETA kilichopo chang'ombe Dar es salaam amewataka watu kutumia mashine zao ambazo zinabadili maziwa ya maji kuwa ya unga pia amewataka kutembelea bando lao lililopo viwanja vya sababa.

habari kamili na Ally Thabit

Monday, 3 July 2023

Papa Francis alaani kuchomwa kwa Quran nchini Uswidi

 Papa Francis alisema kuchomwa kwa kitabu kitakatifu cha Waislamu, Koran, kumemkasirisha na kuchukizwa na kwamba alilaani na kukataa kuruhusu kitendo hicho kama aina ya uhuru wa kujieleza.

“Kitabu chochote kinachochukuliwa kuwa kitakatifu kinapaswa kuheshimiwa kuheshimu wale wanaokiamini,” Papa alisema katika mahojiano katika gazeti la Umoja wa Falme za Kiarabu la Al Ittihad, lililochapishwa Jumatatu. “Ninahisi hasira na kuchukizwa na vitendo hivi.

“Uhuru wa kujieleza haupaswi kamwe kutumika kama njia ya kuwadharau wengine na kuruhusu hilo kukataliwa na kulaaniwa.”

Mwanamume mmoja aliirarua na kuichoma moto Koran katika mji mkuu wa Uswidi Stockholm wiki iliyopita, na kusababisha kulaaniwa vikali na mataifa kadhaa, ikiwa ni pamoja na Uturuki ambayo uungaji mkono wake Uswidi unahitaji kuingia katika muungano wa kijeshi wa NATO.

Wakati polisi wa Uswidi wamekataa maombi kadhaa ya hivi karibuni ya maandamano dhidi ya Koran, mahakama zimepinga maamuzi hayo, ikisema kuwa yanakiuka uhuru wa kujieleza.

Siku ya Jumapili, kundi la Kiislamu la majimbo 57 lilisema hatua za pamoja zinahitajika ili kuzuia vitendo vya kunajisi Koran na sheria ya kimataifa inapaswa kutumika kukomesha chuki ya kidini.

habari picha na Ally Thabit

JOPO LA KUPITIA MAAMUZI YA LATRA LAZINDULIWA

 



Jopo la kupitia maamuzi ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) linaloundwa na wajumbe wa nne (4) limezinduliwa rasmi leo Juni 2, 2023 katika ofisi za LATRA Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jopo hilo, Mkurugenzi Mkuu LATRA CPA Habibu J. Suluo amesema kuwa, Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA kupitia kikao chake maalum kilichofanyika Dodoma tarehe 7 Februari, 2023, iliwateua wajumbe wa nne (4) wa Jopo hilo ambao ni Bw. Mohamed R. A. Mpinga, Mhandisi John Ngaraguza, Wakili Theresia Michael Clemence, pamoja na Wakili Asma Selemani Mohamed.

Aidha, CPA Suluo amesema, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi LATRA Prof. Ahmed Mohamed Ame, alimteua Bw. Mohamed R. A. Mpinga kuwa Mwenyekiti wa Jopo la Mapitio. Bw. Mpinga ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mstaafu.

Vilevile amesema, Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA kwa mujibu wa kifungu cha 26 (1) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413 inapaswa kuunda Jopo la kupitia maamuzi ya Mamlaka linalohusisha watu wawili (2) wenye uzoefu wa masuala ya Sheria na waliofanya kazi kwa angalau miaka kumi (10) pamoja na watu wawili (2) wenye uzoefu wa angalau miaka kumi (10) kwenye masuala ya Uchumi, Fedha, Uhandisi au Usimamizi wa Usafiri.

CPA Suluo ameongeza kuwa, maamuzi yatakayoshughulikiwa na jopo hilo ni kwa mujibu wa kifungu cha 27(1) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413, kwa mtu yeyote ambaye hatoridhishwa na maamuzi ya Mamlaka anaweza ndani ya siku 14 tangu kutolewa maamuzi hayo, kuomba maamuzi hayo yapitiwe,

CPA Suluo amesema, “Tunaishukuru Bodi yetu kwa kuwateua na tunaamini mtatekeleza majukumu yenu kwa weledi wa hali ya juu kwa kuzingatia kuwa Mamlaka inatoa maamuzi na endapo mtoa huduma hajaridhishwa na maamuzi hayo basi atawasilisha kwenu ili kupitia upya maamuzi tuliyoyafanya na hatimaye jopo litatoa mapendekezo yake kwa Bodi ili iweze kufanya maamuzi kwa jambo husika. Endapo maamuzi hayo hayataridhiwa na mleta maombi, anaweza kukata rufaa kwa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal-FCT) kwa mujibu wa kifungu cha 28 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413,” ameeleza CPA Suluo.

Baada ya uzinduzi huo, wajumbe hao wamepewa semina ya Sheria, Kanuni, wajibu na majukumu ya Mamlaka  ili ziwaongezee uelewa wakati wa kutekeleza majukumu yao.

habari kamili na Ally Thabit

LATRA: ZINGATIENI SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

 


Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewasihi watumiaji wa huduma za usafiri ardhini kufuata Sheria, kanuni na Taratibu za Usalama Barabarani ili kuepuka ajali na madhila mengine yanayoweza kutokea.

Hayo yamesemwa na Bw. Salum Pazzy, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka LATRA  wakati wafanyakazi wa LATRA walipotembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) na kushiriki zoezi la Uchangiaji Damu ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Juni 21, 2023.

Akizungumza baada ya kuchangia damu Bw. Pazzy amesema baadhi ya watumiaji wa huduma za usafiri ardhini wamekuwa na tabia ya kupuuzia Sheria za Usalama Barabarani na wengine kushabikia uvunjifu wa Sheria hizo, hali inayowaweka katika hatari ya kupata ajali na madhila mengine barabarani.

“Ningependa kuwasihi wasafirishaji na watumiaji wengine wa huduma za usafiri ardhini kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Usalama Barabarani, kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kujiepusha na changamoto mbalimbali wawapo safarini kama ambavyo tumeshuhudia wenzetu ambao wapo hapa hospitali kwa sababu ya ajali,  hivyo ni vyema kujiepusha na tabia hatarishi pamoja na kushabikia tabia hizo,” amesema Bw. Pazzy.

Akizungumzia sababu za LATRA kwenda katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Bw. Jonathan Kitururu, Mratibu wa Pikipiki za magurudumu mawili na matatu kutoka LATRA amesema wahanga wengi wa ajali za barabarani wanatibiwa MOI hivyo imekuwa rahisi kuwafikia na kuwapa faraja.

“Asilimia kubwa ya waathirika wa ajali za barabarani ni bodaboda na bajaji, hivyo watu hawa ni wahitaji haswa wa damu na wanatuhusu moja kwa moja, hivyo tukaona ni vyema kuja hapa (MOI) na kushiriki zoezi la kuchangia damu,” amesema BW. Kitururu.

Naye Bw. Patrick Mvungi, Meneja Uhusiano kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) amewashukuru wafanyakazi wa LATRA kwa kufika na kushiriki zoezi la kuchangia damu huku akiwaasa wananchi wengine kujitokeza na kuchangia damu kwani kwa kufanya hivyo wanasaidia kuokoa maisha.

“Tnawashukuru sana ndugu zetu wa LATRA waliotenga muda wao kufika hapa (MOI) na kushiriki zoezi la kuchangia damu kwaajili ya kusaidia wagonjwa wetu. Hapa MOI mahitaji ya damu ni makubwa sana wastani wa chupa 15 hadi 30 kwa siku, ukizingatia kwamba tunapokea idadi kubwa ya majeruhi wanaohitaji kufanyiwa upasuaji na kuongezewa damu, hivyo nitoe wito kwa Taasisi nyingine na Watanzania kwa jumla kujitokeza na kuchangia damu kwani kwa kufanya hivyo tunaokoa maisha ya watu wengi,” amesema Bw. Mvungi.

Akizungumza baada ya kuchangia damu Bi. Lilian Temu, Afisa Huduma kwa Wateja LATRA ameelezea hali aliyoipitia wakati akichangia damu, “Nimefurahi sana kuchangia damu naamini itaokoa maisha ya mtu, hii ni mara yangu ya kwanza kuchangia damu, mwanzoni nilikuwa na hofu sana, niliwaza labda nitapata kizunguzungu au nitadondoka au hata kuugua, lakini baada ya kuchangia damu hofu yote imeondoka na ninajiona ni mzima kabisa, hivyo watu waache uoga na wajitokeze wachangie damuz,” amesema Bi. Lilian.

Asilimia kubwa ya ajali za barabarani zinasababishwa na makosa ya kibinadamu kama vile mwendokasi uliopitiliza na kupuuzia alama za barabarani, madhara ya ajali hizo husababisha kupoteza maisha au kupoteza viungo vya mwili na hivyo kupoteza nguvu kazi ya Taifa. Hivyo ni vyema kwa watumiaji wa huduma za usafiri ardhini kufuata Sheria za Usalama Barabarani na kuacha kushabikia uvunjaji wa Sheria hizo ili kufanya Usafiri Ardhini kuwa salama.

Habari picha na Ally Thabit

MHE MALISA: ZINGATIENI SHERIA NA KANUNI ZA USAFIRISHAJI

 


Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Beno Malisa amewaasa wasafirishaji wa abiria na mizigo Mkoani Mbeya watimize wajibu wao kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za usafirishaji.

Mhe. Malisa amesema hayo Juni 26, 2023 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera katika mkutano wa wadau wa usafirishaji abiria na mizigo ulioitishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kujadili changamoto za usafirishaji.

“Kwa kuwa jukumu hili la kujadili na kutoa maoni ya uboreshaji huduma za usafirishaji lipo kisheria, basi nawasihi kila mmoja wetu kwa kuzingatia umuhimu wa kazi hii atimize wajibu wake kwa umahiri wa hali ya juu,” ameeleza Mhe. Malisa

Pia, ameipongeza LATRA kwa kuandaa mkutano huo na kuwa hatua hiyo inaonesha LATRA inavyowajali watoa huduma wa usafiri ardhini.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA Habibu Suluo amesema sekta ya usafirishaji ni moja kati ya sekta muhimu nchini kwani kila mmoja anahitaji huduma hii ya usafiri ili kutimiza wajibu wake wa kila siku.

“Huduma hii ya usafiri ni ya umuhimu katika jamii yoyote na ina mchango mkubwa katika uchumi na ustawi wa jamii yoyote ile duniani hata kufika hapa wote tumekuja kwa usafiri wa aina mbalimbali,” ameeleza CPA Suluo.

Vile vile amewapogeza wadau wa usafirishaji wa abiria na mizigo mkoani humo kwa kuacha shughuli zao muhimu na kuhudhuria mkutano huo.

Naye Mwenyekiti wa Wasafirishaji mkoa wa Mbeya Bw. Elias Mwanginde amesema kuwa, wasafirishaji wa mkoa huo wameona nuru kupitia uongozi wa sasa wa LATRA, hivyo watashirikiana kwa ukaribu ili kutekeleza mambo waliyokubaliana katika mkutano huo.

“Tunaona LATRA sasa ina uongozi imara na kutakuwa na mabadiliko, tunashukuru kwa elimu na majibu mazuri tuliyopata kwa maswali tuliyowauliza. Kupitia mkutano huu tumejulishwa kuwa Kituo cha LATRA cha Kutahini Madereva kiko tayari, pia leo hii tumetangaziwa fursa na wenzetu wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kuwa wako tayari kuwapiga msasa madereva wetu ili kuwakumbusha mambo ya kuzingatia wakatapoenda kufanya mtihani wa kuthibitishwa,” amesema Bw. Mwanginde

Kwa upande wake, Bw. Muntazir Kassamia, msafirishaji wa mizigo amesema kuwa, mkutano huo umejenga uhusiano mzuri baina ya wasafirishaji na Serikali kwa kuwa baadhi ya changamoto zimeweza kutatuliwa kwa wakati na zingine zinafanyiwa kazi.

“Leo tumefaririjika sana kukutana na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA katika mkoa wetu wa Mbeya na tulikuwa na changamoto zetu ndogo ndogo na tunashukuru kwa uweledi na busara zake kuna mambo mengine ameyapatia ufumbuzi papo kwa papo, baada ya kupewa elimu na uamuzi alioufanya kwa kweli ametengeneza uhusiano mzuri sana baina ya LATRA na wasafirishaji mkoani hapa,” amesisitiza Bw. Kassamia.

Naye Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Mbeya SP Hussein Gawile amesema, “Kikao cha leo kimeleta hamasa kubwa sana kwa wamiliki maana leo wamepata ufumbuzi wa changamoto zao na mengi ambayo yamezungumzwa ni yale yatakayo leta athari chanya  kwenye tasnia hii ya usafirishaji nchini.”

LATRA imekua na utaratibu wa kuandaa mikutano mbalimbali ya wadau wa usafirishaji nchini kwa lengo la kutoa elimu pamoja na kuimarisha uhusiano baina ya Mamlaka na wadau wa usafirishaji ili kuleta maendeleo katika sekta ya usafiri ardhini nchini.

Habari kamili na Ally Thabit

MHE. MWAKIBETE AWAPONGEZA MADEREVA 999 WALIOTHIBITISHWA NA LATRA

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Mhe. Atupele Fredy Mwakibete (MB) amewapongeza madereva 999 waliofanya mtihani na kuthibitishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na amewasihi ambao hawakufaulu kutokata tamaa bali wajikumbushe tena yale waliyojifunza na warudi kufanya mitihani ili wathibitishwe.

Mhe. Mwakibete amesema hayo kwenye ufunguzi wa hafla ya uzinduzi wa Mtaala na Utoaji wa Vyeti kwa Madereva wa Vyombo vya Moto Vinavyotoa Huduma Kibiashara Waliothibitishwa na LATRA iliyofanyika Julai 01, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Arnaoutoglou, Dar es Salaam.

“Ninaamini hata wale ambao hawakufaulu, wamejikumbusha mambo kadhaa na niwasihi wasikate tamaa bali wajikumbushe tena yale waliyojifunza na warudi kufanya mitihani hii ili wathibitishwe na tuje kuwapatia vyeti siku chache zijazo,” ameeleza Mhe. Mwakibete.

Vilevile amesema kuwa, juhudi za LATRA za kuthibitisha madereva zitaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafiri ardhini nchini kwa kubadili tabia za madereva wakiwa barabarani na kutakuwa na tofauti ya dereva aliyethibitishwa na LATRA na yule ambaye hakuthibitishwa na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha usalama wa sekta ya usafirishaji.

Aidha, Mhe. Mwakibete amezungumzia faida za kuwathibitisha madereva, “Serikali inaamini kuwa hadhi ya madereva itaongezeka, wataheshimika zaidi na maslahi yao yataboreshwa na zaidi, taaluma hii ya udereva itarasimishwa na kuwaongezea madereva thamani kwenye masoko ya ajira ya ndani na nje ya nchi, hususan kwenye nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),” amefafanua Mhe. Mwakibete.

Naye Mhe. Jumanne Sagini (Mb), Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani amesema zaidi ya asilimia 76 ya ajali zinazotokea barabarani zinasababishwa na makosa ya kibinadamu na hivyo amewaasa madereva hao kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Usalama Barabarani ili kupunguza na kuondoa kabisa ajali hizo.

Vilevile, ameipongeza LATRA kwa kuendelea kushirikiana na taasisi nyingine za umma ikiwemo Jeshi la Polisi, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na VETA kwa kuandaa kwa pamoja maswali yenye nia njema ya kufahamu uelewa wa madereva wa vyombo vya moto vinavyotoa huduma kibiashara.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA Habibu Suluo amesema Kanuni ya 22(i) ya Leseni za Usafirishaji (Magari ya Abiria), 2020 inaainisha moja ya masharti ya leseni zinazotolewa na LATRA ambapo inawataka wenye vyombo vya moto vinavyotoa huduma za usafiri kibiashara, kuhakikisha kila dereva anayeendesha vyombo hivyo wanakuwa na Cheti cha Uthibitisho kinachotolewa na Mamlaka baada ya kufanya mtihani na kufaulu,

Vilevile amesema kuwa, kabla ya kuanza kutahini madereva, Mamlaka kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, ilipitia maswali ya mtihani yanayotumika kwenye vyuo vinavyozalisha madereva nchini kulingana na mitaala inayotumika na kuyaweka katika mfumo wa Kutahini Madereva (DTS).

Aidha, CPA Suluo ameeleza kuwa, maswali hayo yanawapima madereva kuhusu uelewa wao kwenye maeneo ya alama na miongozo mbalimbali inayowasaidia kuendesha vyombo vya moto kwa usalama, “Baada ya maswali kupitishwa na kuwekwa kwenye mfumo, tarehe 1 Juni, 2022 Mamlaka ilianza rasmi kutumia mfumo wa DTS kutahini madereva ambapo hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2023 jumla ya madereva 1,744 walikuwa wamefanya mtihani na madereva 999 walifaulu.” 

“Kwa kuwa tunawajali madereva wetu na tunataka wafaulu kwa wingi, LATRA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, tumeandaa video mbalimbali zinazoelimisha kuhusu masuala ya msingi ya kuzingatia ukiwa barabarani ikiwemo suala la alama. Video hizi zinapatikana katika Online TV ya Mamlaka inayopatikana kwa jina la latraTV kwenye mtandao wa YouTube, hivyo ninawasihi wakatazame ili kujielimisha zaidi kabla ya kuja kufanya mtihani,” amesema CPA Suluo

Habari picha na Ally Thabit

Saturday, 1 July 2023

MKUU WA WILAYA YA ILALA AIPONGEZA NBS NAKUTOA NENOKWA WATENDAJI

 Edward Mpogolo amewapongeza NBS kwa kuweza kufanya vizuri katika Sensa kwani matokeo ya sensa yatasaidia katika kupanga maendeleo kwa jamii pia amewataka watendaji na wenye viti wa serikali wa mitaa kwenye wilaya ya ilala wayatumie matokeo ya sensa kwaajili ya kutatua changamoto za elimu, afya, maji mazingira na ulinzi. Amesema haya kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee wakati NBS wakitoa mafunzo kwa wenye viti na watendaji wa kata za ilala.

Habari kamili na Ally Thabit