Waziri Dr Doto Biteko amesema lengo lakukutana na chema ya madini ili kutatuwa kero zinazo wakabiri wanachama wa chema hii ya madini, kero hizo ni wingi wa kodi, tozo, mwingiliano wa Sheria mfano mizara ya Mali asiri na utalii ambapo wanazuia uchimbaji wa madini kwenye hifadhi na mbuga hata hivyo Dr Doto Biteko amempongeza na kumshukuru mwenyekiti wa chema ya madini pamoja na wajumbe wake kwa namana wanavyotoa ushirikiano kwenye serikali yao mpaka kupelekea secta hii kukua kwa kiwango kikubwa na kuongezeka kwa mapato.Waziri Dr Doto Biteko ametoa wito kwa jamii na kwa wachimba madini kulinda na kuhifadhi Maliasiri za Tanzania. pia amewatoa hofu chemba ya wachimba madini kuwa sheria zenye mwingiliano zitafanyiwa kazi.Naye kwa upande wake mwenyekiti wa chemba ya wachimba madini amempongeza serikali na kuishukuru kwa kutatua kero za wachimba madini kwa kazi kubwa.
Habari picha na Ally Thabiti.
No comments:
Post a Comment