NA. VERO IGNATUS, ARUSHA
Madereva wa Magari ya kubeba abiria katikia Jiji la Arusha maarufu kama Daladala wametangaza kusitisha huduma hiyo wakidai shughuli zao kuingiliwa na Watoa huduma za Usafiri wa Pikipiki za Magurudumu Matatu maarufu kama Bajaji.
Aidha Madereva hao wamedai kwamba hawatotoa huduma hiyo hadi pale Mamlaka za Jiji la Arusha zitakapopata ufumbuzi wa suala hilo,
Mgomo huo umeshuhudiwa katika Siku ya leo Jumatatu na kuonekana kuathiri huduma za Usafiri hususani kw Wafanyakazi,Wafanyabiashara pamoja na Wanafunzi ambao wamefungua Shule.
Akizungumzia mgomo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro, Locken Adolf amesema kuwa utitiri wa bajaji umeathiri biashara ya daladala hivyo wanaiomba serikali kuzipunguza.
“Ukubwa wa eneo la Arusha, hazitakiwi kuzidi zaidi ya 100 lakini sasa zimekuwa nyingi na zimekuwa kero sana na zimeteka ruti zote za daladala. Pia zinafanya biashara ya kupakia abiria kama wanavyofanya wenzao jambo ambalo siyo makubaliano wakati zinaingia mjini,” amesema
Akitoa dukuduku lake mmoja abiria, Maria Pallagyo amesema mgomo huo umeanza leo asubuhi umesababisha shida kwao pampja na wanafunzi ambao wanatakiwa kwenda mashuleni,pampja na wafanyakazi,wafanyabiashara amabao wanawahi masokoni
“Tunaamini kuwa serikali yetu ni sikivu,na sidhani kama itaacha wananchi wake wateseke namna hii ,tunaiomba itafute suluhu ya jambo hili kwani tunaoteseka ni kwa suala la daladala kugoma imekuwa siyo mara moja,yaani kwetu ni mateso tu amesema Maria.
Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra), Mkoa wa Arusha, Amani Mwakalebela amesema kuwa wamesikia mgomo huo na wanaendelea na taratibu za kushughulika na madai ya madereva hao wa daladala, kuona namna gani watataua changamoto hiyo .
Mwakalebela amesema kumekuwa na ongezeko la bajaji ndani ya Jiji la Arusha hasa ruti za Sombetini-Ngusero, pia njia ya Majengo, pamoja na ile ya Uswahilini -Dampo ambapo wameanza kuchukua hatua kuona ni namna gani wataweka mambo yakae sawa
“Kutokana na ongezeko la bajaji ambapo katika 350 zilizosajiliwa na zoezi kufungwa lakini zipo zaidi ya bajaji 2,000 ambazo zinafanya kazi na kugeuka kero, hivyo tulichoamua ni kuomba oda ya mahakama kuzipiga mnada bajaji ambazo tutazikamata hazina usajili . Alisema Mwakalebela
Mgomo huo umemuibua Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro, Locken Adolf ambapo amesema kuwa kumekuwa na utitiri wa bajaji umeathiri biashara ya daladala hivyo wanaiomba serikali kuzipunguza, ili daladala nazo ziweze kuingiza kipato.
habari picha na Ally Thabith
No comments:
Post a Comment