Tuesday, 10 July 2018

MHADHILI WA CHUO CHA KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE AWEKA MAMBO HADHARANI

Dkt Fillip Daninga ambaye ni mhadhili wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya mwalimu  nyerere amesema kuwa "lengo la luanzishwa kwa chuo hiki kuandaa vijana kuongoza nchi hii baada ya kupata uhuru wa Tanganyika ambapo waliweza kufundishwa na mpaka sasa wanafundisha maswala ya maadili,uadilifu,nidhamu,siasa na uchumi ili kuweza kupata viongozi bora ambapo lengo hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa"

Dkt Fillip Daninga akizungumza na mwanahabari katika maonyesho ya 42 ya biashara sabasaba Dar es salaam
Pia vilevile hakusita kutaja baadhi ya viongozi nguli ambao walinufaika na elimu hiyo akiwemo raisi mstaafu wa awamu ya nne mh Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,Mzee Kaduma,Mzee Fillip Mangula,mh Nape Nauye ambaye ni mbunge wa jimbo la Mtama Lindi na mh Isaya Mwita ambaye ni meya wa jiji la Dar Es Salaam
Hakusita kusema jinsi chuo kinavyo wafikia jamii kwa njia ya makongamano,matangazo ya radio na televisheni, kwa machapisho mbalimbali kwa njia ya vitabu,majarida na kielectronic pia wamejipanga kutoa elimu ya ngazi ya juu masters, amesemahayo kwenye maonyesho ya biashara 42 sabasaba Dar Es Salaam.habari picha na Ally Thabit

BUNGE YAJA NA MIKAKATI MIZITO MASHULENI


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa mheshimiwa RITA KABATI amesema "kwamba wameamua kuja na mpango maluum wa kutengeneza vyoo kwa kila jimbo moja kwa lengo kuwasaidia wanafunzi wa kike na wanafunzi wenye ulemavu kutopa shida mashuleni pindi wanavyokwenda kujisaidia vyoo"
 
mhs Rita Kabati akizungumza na mwanahabari katika maonyesho ya biashara 42 sabasaba, Dar es salaam.
Pia wameamua kuwatafutia fursa mbalimbali kwa watu wenye ulemavu Bi Rita Kabati amewapongeza wabunge wa Tanzania kwa kuunga mkono hoja za watu wenye ulemavu pamoja na watoto wakike ambao hupitia kwenye changamoto mashuleni amesema hayo kwenye maonyesho ya  biashara ya 42 sabasaba ambayo yanaendelea jijini Dar Es Salaam wilaya ya Temeke. Habari picha na Ally Thabit

Thursday, 5 July 2018

WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOROJIA AWEKA HAZARANI MIKAKATI MIZITO

Wazirin wa elimu sayansi na teknorojia prof JOYCE NDARICHAKO  amesema wamekuja na muongozo wa kuwatambuwa na kuwaweka pamoja wabunifu wadogowadogo na kuwafikia kwa ngazi ya halmashauri pia wameamua kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwenye bajeti ya mwaka huu kiasi cha zaidi ya bilioni30 kwaajili ya utafiti na ubunifu na mambo ya sayansi na teknorojia .Lengo kupata wataalam vifaa pamoja na mashine ili kufikia hazima Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati kama rais Magufuli anavyo elekeza  .Pia ametoa wito kwa tume ya sayansi na teknorojia kutumia fedha hizi kama inavyotakiwa. Pia ameipongeza tume ya sayansi na teknorojia kwa uhadilifu' uzarendo na kwa kwakufanya tafiti zenye tija kwa maslai ya Taifa na kwa kuandaa kongamano la sita la sayansi teknorojia na ubunifu


Habari picha na ALLY THABITI

WADAU WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAUNGA MKONO WABUNIFU

Wadau wa sayansi na teknorojia pichani wakionekana kuunga mkono jitiada zinazofanywa na serikali kwa kuanzisha muongozo wa kuwatambua wabunifu wadogowadogo na kuwafikia kwa ngazi ya halmashauri

habari picha na Ally thabiti

VIJANA WABUNIFU WATOA YA MOYONI KWA WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOROJIA

Mmoja ya kijana mbunifu amemuomba waziri wa elimu sayansi na teknorojia prof JOYCE NDARICHAKO wawawezeshe kwa hali na mali na kitaaluma ili wafikishe malengo yao ya kuwa wabunifu wa kimataifa  hamesema  aya alipotembelewa kwenye banda lake katika ukumbi wa mlimani city katika kongamano la sita la sayansi teknorojia na ubunifu baada ya kutembelewa na waziri wa elimu sayansi na teknorojia prof JOYCE NDARICHAKO

Habari picha na Ally Thabiti

WABUNIFU WAUNGA MKONO HAZIMA YA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA

Pichani mwana mama akimuelezea waziri wa elimu sayansi na teknorojia prof JOYCE NDARICHAKO namna walivyo buni mashine mbalimbali  Lengo ni kumuunga mkono rais Magufuli kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati .amesema haya kwenye kongamano la sita la sayansi teknorojia na ubunifu  kwenye ukumbi wa mlimani city jijini dar es salaam

habari picha na  Ally Thabiti

Saturday, 30 June 2018

WATANZANIA WATAKIWA KUTOKATA TAMAA


Watanzania watakiwa kuto kata taama katika suala la kudai haki kwani haki ni msingi ambao kila mtanzania natakiwa kuipata hayo yamesemwa na Pili Mohammed Kuliwa msaidizi kisheria kutoa mkoa wa Lindi katika semia iliyofanyika Landmark hotel ,Ubungo jijini Dar es salaam , semina ambayo imeandaliwa kituo cha msaada wa kisheria LHRC, Semina hiyo ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kisheria wasaidizi wote wa kisheria nchini.


Habari picha na ALLY THABIT