Tuesday, 1 October 2019
SHIVIAWATA YATOA NENO KWA THRDC
Brandina Sembu katibu wa jumuhia ya wanawake na watoto shirikisho la vyama la watu wenye ulemavu (SHIVIAWATA) amesema kitendo cha THRDC kukusanya ripoti za maswala ya watu wenye ulemavu katika utekelezaji kupeleka umoja wa Mataifa ni jambo la kishujaa tena linatakiwa kuungwa mkono kwani serikali ya Tanzania kwa upande wa watu wenye ulemavu wanawake aiwatendei haki hata kidogo mfano walemavu wa kutosikia wakienda kujifungua mahospitalini hakuna wataaramu wa lugha za alama hivyo upelekea vifo vya watoto na mama wajawazito.
pia ni tatizo kwa vitanda vya kujifungulia kwa wanawake walemavu wa viungo vya miguu ambako vitanda hivi vipo juu zaidi hivyo amewataka THRDC kuwasilisha maswala haya ili yatendewe kazi huko umoja wa Mataifa ili serikali ya Tanzania iwajibishwe.
Habari picha na
Victoria Stanslaus
WATU WENYE ULEMAVU WAIPA TANO THRDC
Mwanasherisa Maduu Cosmas William kutoka under the same sun amesema maswala ya watu wenye ulemavu bado ayajatekelezwa kwa kiwango kikubwa licha ya serikali kulizia mikataba ya kimataifa na kuwepo kwa sheria mfano kuwajiliwa kwa watu wenye ulemavu bado aijatekelezwa kwa kiwango kikubwa hivyo amewapongeza THRDC kwakuwakutanisha kufanya tasmini hii huku akiwaomba THRDC wasisite kuwasilisha maswala yanayowasibu watu wenye ulemavu umoja kwa mataifa.
Hamesema haya kwenye ukumbi wa LAP mkumbusho jijini Dar es Salaam.
Habari picha na
Victoria Stanslaus
WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO WATAKIWA KUFIKISHWA MARA MOJA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE JKCI
Na Mwandishi wetu
1/10/2019 Madaktari nchini wameshauriwa kuwatuma watoto wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mapema iwezekanavyo mara baada ya kuwagundua kuwa na matatizo hayo ili waweze kupata matibabu kwa wakati.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kwa watoto (JKCI) Naiz Majani wakati akizungumzia kuhusu kambi ya matibabu ya magonjwa ya moyo ya ya kuzaliwa nayo kwa watoto ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Taasisi hiyo.
Dkt. Naiz ambaye pia ni msimamizi wa kambi za matibabu ya moyo zinazofanyika katika Taasisi hiyo alizitaja dalili za mtoto mwenye magonjwa ya moyo kuwa ni pamoja na kutokwa na jasho kwa wingi wakati wa kunyonya, kutoongezeka uzito, kupata nimonia, kikohozi cha mara kwa mara , kushindwa kucheza , kuvimba miguu na kubadilika rangi kwenye midomo na kucha kuwa rangi ya bluu.
“Ninawaomba madaktari wanapoona dalili kama hizi kwa mtoto wawalete katika Taasisi yetu kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi kwani kuna baadhi ya matatizo ya moyo ya kuzalliwa nayo mtoto hatakiwi kuzidi umri wa miezi sita hadi mwaka mmoja bila ya kupata matibabu. Mtoto mwenye matatizo hayo akichelewa kupata matibabu akiwa na umri huo hawezi kufanyiwa upasuaji tena”, alisisitiza Dkt. Naiz.
“Katika kambi ya matibabu ya pamoja tuliyoyafanya na wenzetu wa Shirika la Mending Kids International lenye wataalamu wa afya kutoka nchini Italia na Marekani watoto wanne walishindwa kufanyiwa upasuaji kutokana na umri wao kuwa mkubwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu hivyo wataendelea na matibabu ya kawaida”, alisema Dkt. Naiz.
Akizungumzia kuhusu kambi hiyo Dkt. Naiz alisema watoto 40 walifanyiwa upasuaji kati ya hao watoto waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua 17 na upasuaji wa bila kufungua kifua 23 ambapo hali zao zinaendelea vizuri na wengine wamesharuhusiwa kurudi nyumbani.
Dkt. Naiz alisema, “Kambi hii imeenda vizuri, kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama, wakati huduma za upasuaji zinaendelea kwa watoto walijitokeza wasamaria wema wawili na kuchangia matibabu ya watoto wawili ambao wazazi wao hawakuwa na uwezo wa kuwagharamia matibabu. Watoto hao wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri”, alisema Dkt. Naiz.
Kwa upande wa wazazi ambao watoto wao walipata wafadhili wa kulipiwa gharama za matibabu walishukuru kwa huduma ya matibabu ambayo watoto wameipata na kuwaomba wadau wengine wajitokeze kuchangia gharama za matibabu ya moyo kwa watoto.
“Namshukuru mfadhili wa mtoto wangu ambaye amelipa gharama za matibabu ya mtoto ambaye amefanyiwa upasuaji na hali yake inaendelea vizuri. Mara kwa mara amekuwa akinipigia simu na jana amekuja kumuangalia mtoto kujuwa maendeleo yake”, alisema Eva Jacob
MSANII NGULI APINGA VIKALI UZALILISHAJI WA WANAWAKE
Kalajeremaya ni msanii wa mziki wa kizazi kipya amewataka wasanii hapa nchini kuacha kuwatumia wanawake na watoto wa kike hapa nchini kuwazalilisha kwa kuwaweka kwenye video zao huku maongo yao ya sili yakiwa yanaoneka kwani yeye amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwatumia watoto wakike bila maungo yao ya mwili kuonekana.
Hamesema haya kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Habari picha na
Victoria Stanslaus
SANAA YA MZIKI NA FILAM YAINGIZA WATOTO KATIKA VISHAWISHI
Mkurugenzi wa program kwenye tasaisi ya Bright Jamii Inshetiave Godwin Mungi amesema wameweza kufanya tafiti katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Aruha wamebaini kuwa sanaa ya muziki imesababisha watoto wengi kujihusisha na maswala ya unywaji pombe, uvutaji wa bangi na kuacha masomo kwa upande wa filam umesababisha wanawake pamoja na watoto wakike kujihusisha kwenye maswala ya ngono zembe amehiasa jamii, wazazi, walezi,serikali na viongozi wa dini waakikishe wasanii sanaa wanayotoa ilinde utu wa mwanamke na mtoto pamoja na maadili na destuli ya nchi yetu ya Tanzania.
Amesema haya kwenye uzinduzi wa ripoti ya maswala ya sanaa na filam katika hoteli ya Selena jijini Dar es Salaam.
Habari Picha na
Ally Thabiti
RUSHWA YA NGONO YAWATAFUNA WASANII WA KIKE NCHINIAAA
Anna Sangai amesema asasi za kiraia zimeamua kutoa elimu kwa wasanii kuacha kuwazalilisha wanawake na watoto katika kazi zao za sanaa kwani wanawake wengi wanatumika kutoa rushwa ya ngono katika filam na nyimbo .
Hivyo asasi za kiraia zitatoa elimu na pia wameitaka serikali kuweza kutumia sheria katika matumizi ya filam oambazo azina maadili na nyimbo lengo kunsulu watoto waweze kusoma kwa bidii.
amesema haya kwenye uzinduzi wa ripoti ya namna ya sanaa na filam zinavyo wazalilisha wanawake na watoto kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Habari picha na
Victoria Stanslaus
VIONGOZI WA KIDINI WALALAMA JUU YA FILAM
Sheikh Abdallah Kundecha amesema nyimbo zinazoimbwa na wasanii wa kitanzania pamoja na Filam zinamzalilisha mwanamke pamoja na watoto kwani lugha zinazotumika kwenye nyimbo ni zamatusi pia wanawake katika filam wanatumika katika kuonesha maungo yao ya mwili ususani ni sehemu za sili huu ni udhalilishaji.
Nae mkurugenzi wa Bright Jamii Inshetive bibi Irene ambaye yupo kushoto wa Sheikh Abdallah Kundecha amevitaka vyombo vya habari na wasanii kupigavita maswala ya uzalilishaji wa wanawake na watoto kwa wandishi wa habari wasipige nyimbo za matusi na uzalilishaji na wasanii waache kutoa filam za kufedhehesha wanawake na watoto amesema haya Serena Hotel jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti inayohusu wasanii pamoja filam zipozalilisha wanawake na watoto.
habari picha na
Ally Thabiti
Subscribe to:
Posts (Atom)



