Friday, 12 March 2021

WAZIRI WA MADINI ATOA CHOZI ZITO

 Doto Biteku Waziri wa  Madini ameitaka TEITI kuweza kuwasaidia wachimbaji wadogo wa Madini kwa kutoa ripoti za kuwakwamuwa wachimbaji wadogo kuwa wakati na wakubwa

Waziri Doto Biteku ameitaka TEITI kuweza kujitangaza zaidi na kujenga mahusiano mazuri na taasisi zingine amesema haya kwenye Ofisi za Bunge posta jijini Dsm 

Habari na Victoria Stanslaus


Thursday, 11 March 2021

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE AIPONGEZA TRA

 Mkuu wa Wilaya yaTemeke Godwini Gondwe amesema kampeni ya TRA ya Mlango kwa Mlango kwaajili ya kutoa elimu ya kuamasisha watu kulipa kodi ni mzuri  kwani itasaidia kwa kiwango kikubwa kuwepo kwa mazingira wezeshi na rafiki  kwa wawekezaji na wafanya biashara wadogo,wakati na wakubwa kuenddelea kufanya shughuri zao ndani ya Temeke na wengine kuvutiwa kuja  kuwekeza Temeke . Pia kampeni hii ya TRA itasaidia katika ujenzi wa huduma za msingi ndani ya Temeke kutokana na pesa za walipa kodi  mfano barabara,hospitali na miundombinu mingineyo . Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwini Gondwe ametoa wito kuwa TINI namba ni bure na wananchi waTemeke wawape ushirikiano Maafsa wa TRA 


Habari na Victoria Stanslaus


Saturday, 20 February 2021

AFISA VIWANGO WA TBS AWATOA MCHECHETO WADAU WA MABATI NA COILI


 Henry Masawe Afisa viwango wa TBS amesema kuwa wanafanya Operation Mbalimbali kwa ajili ya kukagua Mabati na Coili kwa Wazalishaji, Wauzaji na wasambazaji wa bizaa hizi  lengo kuwepo na biadhaa za Mabati na Coili zenye Viwango bora, Pia hatua kari zikichukuliwa zidi yao kusiwepo na malalamiko ndiyo maana wanawashirikisha kila hatua.

amesema haya jijini Dar es Salaam makao makuu ya TBS huduma walipokutana na wadau wa Mabati na Coili.

Habari na ALLY THABITI

SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS) LAJA NA MIKAKATI MIZITO


 Kaimu mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Davis Mtebalemwa amesema wameamua kukutana na Wazarishaji, Waagizaji na Wasambazaji wa Mabati na Coili kwa ajili ya kujiajili namna ya kutengeneza bizaa bora za Mabati na Coili hii itasaidia kuimalika kwa biashara zao za Mabati na Coili pamoja na kuimalisha afya za watumiaji na kulinda maslahi ya wanunuaji wa bizaa hizo kwani endapo Mabati na Coili zikikosa ubora uchumi wa watu utayumba na Taifa litayumba na afya za watumiaji zitateteleka.

Hivyo amesema ndiyo maana wamekuja na mikakati bora ya viwango vya ubora wa mabati TZS 353 toleo ya mwaka 2020 na TZS 1077 ya Mabati na Coili ambazo zipo kwenye umoja wa jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati amesema haya jijini Dar es Salaam Makao makuu ya Shilika la Viwango Tanzania (TBS) Ubungo walipokutana na Wazalishaji, Waagizaji na Wasambazaji wa Mabati na Coili.

Habari na ALLY THABITI

TPSF YASIKILIZA KILIO CHA UWEKEZAJI


 Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Francis Nanai amesema lengo la kukutana na wawekezaji hapa Nchini kuweza kujadili changamoto zinazowakabili, amesema kodi ya VAT na kodi ya sukari ya viwandani imekuwa ni kilio kikubwa kwa wawekezaji hivyo amesema kupitia taasisi hii watakaa na serikali ili waweze kujadili kwa pamoja jinsi ya kuondoa vikwazo vinavyowakabili wawekezaji.

Amesema haya jijini Dar es Salaam alivyokutana na wawekezaji tofautitofauti.

habari picha na

Ally Thabiti

NANDY AWA BAROZI WA PADS ZA LOWLESS SANITARY


 Msanii Nandy amesema Watanzania na wasio Watanzania watumie pad za LOWLESS SANITARY kwani ni salama na ubora pia zinamfanya mtumiaji ajisikie vizuri, ameishukuru kampuni hii kwa kumchagua yeye awe barozi wao amesema haya jijini Dar es Salaam

Habari picha 

Ally Thabiti

Thursday, 18 February 2021

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ATOA MAAGIZO MAZITO


 

Mashimba ndaki waziri wa mifugo na uvuvi amesema kuanzia tarehe 17 mwezi 12, 2021 kuku watauzwa kwa kilo, pia ameitaka Bodi ya nyama kwasambalatisha mara moja watu wanaouza vifaranga vya kuku eneo la Tazara wawasambaratishe mara moja na kampuni zinazo walazimisha wateja kununua kuku au chakula cha kuku hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na wale ambao wanatotolesha vifaranga vya kuku kienyejienyeji na wanaojifanya mawakala chamtema kuni watakipata maana selikari haiwezi kuwacha uhuni huu ufanyike kwani sector ya kuku ni sector muhimu nchini Tanzania ndio maana Rais Magufuli anaipa kipaumbele ili iweze kuchangia pato la Taifa.

Waziri Mashimba Ndaki amewatoa hofu na mashaka wafugaji wa kuku kuwa changamoto ya kodi na bei elekezi yakuuza kuku amelibeba na kulifanyia kazi.

Mashimba Ndaki amempongeza kaimu msajili wa bodi ya nyama kwa ubunifu wake kwa kuwakutanisha wadau wa sekta ya mifugo kwaajili ya kupata Suruhisho ya changamoto wanazokutananazo wadau hawa kwaajili ya masilahi mapana ya Taifa. Amesema haya jijini Dar es Salaam alivyokutana na wadau Mbalimbali wa Sekta ya mifugo.

Habari picha na Ally Thabith