Sunday, 15 October 2023

Watanzania wametakiwa waweze kuchangamkia kujiunga na huduma za bima kwani zinasaidia kutatua changamoto wanazoweza kukumbana nazo wakati wanapokubwa na majanga ya aina mbali mbali.

Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam  wakati wa uzinduzi wa TAKAFUL inayotolewa kupitia kampuni ya uwakala ya GALCO Insurance kwa kushirikiana na kampuni mama ya ZIC TAKAFUL LTD ambayo ni huduma ya bima yenye misingi na Sheria za kiislam .

Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Bima nchini  (TIRA) Bi.Khadija Said  aliyasema hayo alipo fika kwenye hafla hiyo kumwakilisha Kamishina wa bima wa TIRA nchini Dkt.Baghayo A.Saqware ambapo  amezitaka wakala zinazotoa huduma za bima kutoa huduma hiyo kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizotolewa na mamlaka hiyo.

Bi . Khadija amesema kuwa kampuni zote za uwakala wa bima zinapaswa kuzingatia kanunu na sheria zilizowekwa na TIRA  iliwaweze kitoa huduma kwa wateja wao kwa kiwango na ubora unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Aidha ameendelea kufafanua kuwa kwa mujibu wa mpango wa kuendeleza sekta ya fedha hadi kufikia mwaka 2030 matumizi ya bima yamelengwa kufikia asilimia 50 lakini mpaka sasa matumizi hayo ni asilimia kumi na tano pekee nakwamba uelewa wa matumizi ya bima umelengwa kufikia asilimia 80 mwaka 2030 ambapo kwa sasa .

Hata hivyo Bi. Khadija amezisisitiza kampuni na wakala za bima kuendelea kutoa elimu kwa watanzania waweze kuchangamkia.


"Huduma hii ya Bima ya  Takaful  mchakato wake umeanza rasmi mwaka 2008 kupitia kampuni ya ZIC Insuarance na imezinduliwa  rasmi  miezi mitatu iliyopita na Rais wa  serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein  Mwinyi,hatua hii ni kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya Bima ya Misingi ya hesheria ya kislam TAKIFUL lakini huduma hii inatolewa kwa waislam na wakristo kwa ujumla"amesema

Takaful ambayo inasimama kama nguzo katika jamii na inasimama katika misingi ya kushirikiana pale ambapo kutakuwa na majanga au faida.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa makampuni ya GSM  Group yanayomiliki kampuni ya Galco Insuarance Ltd ,Benson Mahenya amesema huduma zao za bima ya Takaful sio sera ila ni ahadi ya kuwa wapo karibu na watu katika kutatua changamoto za kibiashara na kimaisha kiujumla .

"Tunafanya kazi katika misingi ya kweli na uwazi na kuhakikisha usawa katika utoaji wa huduma,tuna uzoefu wa miaka mitano sokoni na katika kipindi hiki tumeweza kutoa huduma kwa watu binafsi zaidi ya mia tano na makampuni zaidi ya kumi ,"amesema Mahenya .

Naye meneja Biashara  Emmanuel Bugabu  amesema kuwa Galco Insurance Brokers inashirikiana na makampuni mbali mbali ya kiwemo MAYZUH COMPAZNY LIMITED ilikutoa mafunzo kwa wafanyakazi  na kuhakikisha wana uelewa na huduma ya Takaful na wanashirikiana na pia na ZIC TAKAFUL LTD katika utoaji huduma hiyo ya bima ya misingi ya kiislam TAKAFUL.

"Nia yetu ni kukuza mwamvuli wetu wa huduma  za bima kwa watu wote wakiwemo mtu mmoja mmoja , wanafamilia,wafanyabiashara na makampuni  au taasisi mbali mbali,nakusisitiza kuwa wafanyakazi wa Galco Insuarance wamepata elimu ya kutosha kutoa huduma kwa wateja" amesema Bugabu

 Kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Israel na maeneo mengine ya jirani, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa mpango wa kuwarejesha nchini Watanzania waliopo nchini humo na maeneo mengine ya karibu.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema, Serikali imefikia uamuzi huo baada va kufanya tathmini na kujiridhisha kwamba mazingira ya sasa yanaruhusu zoezi hilo kufanyika.

“Hivyo, Watanzania walio tayari kurejea nyumbani wanashauriwa kujiandikisha kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Tel Aviv, Israel kupitia barua pepe: telaviv@nie.go.tz au simu namba: +972 533 044 978 na +972 507 650 072, kabla ya tarehe 15 Oktoba 2023, saa
6 usiku”

 

Mfanyabiashara maarufu wa maduka ya simu jijini Arusha aliyefahamika kwa jila moja la Mallya amekutwa amefariki kwenye gari yake katika eneo la Maegesho ya Magari (CITY CAR WASH)huku mwili wake ukiwa umeharibika.

Tukio la kugundulika kwa mwili wa marehemu limetokea mapema leo baada ya waosha magari kusikia harufu kali iliyokuwa ikitoka ndani yagari hilo Askari polisi walifika eneo la tukio na kuukuta mwili huo uliokuwa kwenye gari aina ya SCUDO lenye namba T 466 AUB lililokuwa limeegeshwa katika eneo hilo.

Baadhi ya mashuhuda walidai kuwa marehemu Malya amekuwa na desturi ya kufika eneo hilo na kuegesha gari lake na kisha kwenda bar iliyopo eneo hilo kwa ajali ya kula chakula na kunywa.

Mwenyekiti wa eneo hilo maarufu kwa wauzaji wa magari (madalali) ,Alex Kahel alisema alipata taarifa asubuhi ya leo oktoba 13, kuhusiana na tukio hilo na baada ya kufika aliweza kulitambua gari hilo kuwa ni mali ya mfanyabiashara huyo.


 WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muuungano na Mazingira, Seleman Jaffo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe mkoani Pwani, amekabidhi mifuko 600 ya sarufi kwa  madiwani wa kata za wilaya hiyo kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Shikizi.

Aidha Waziri Jaffo ametoa mitungi ya gesi 126 kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya na mkoa ikiwa ni jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kutunza  mazingira.

Waziri Jaffo amekabidhi  mifuko ya saruji na mitungi ya gesi kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya kilichohudhuriwa  na Katibu wa Chama hicho Mkoa Waziri Jaffo alisema lengo ni kuunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira mazuri.

Amesema tayari katika Jimbo la Kisarawe Shule zimejengwa katika maeneo mbalimbali na ni shule nzuri,ila kwa baadhi ya vitongoji bado hivyo wanaendelea na mchakato huo kuhakikisha kila kitongoji kinakuwa na shule shikizi.

“Leo nimetoa mifuko ya cement kwa shule 4 ambapo kila moja imepata matofali 150 yatasaidia kufyatulia matofali na kuanza ujenzi wa madarasa hata mawili mawili,”amesema na kuongeza

“Hii ni kuonesha Wananchi ni namna gani Chama cha Mapunduzi kinavyotekeleza ilani zake na kuhakikisha kila kitongoji kinapata shule hata vile vitongoji vya mbali kama cha Kimelemeta,”amesema.

Katika kikao hicho, hoja mbalimbali ziliibuliwa zenye lengo la kuboresha huduma kwa wananchi likiwemo suala la maji  katika kata sita, Katibu wa CCM mkoa, Bernard Ghaty anatoa maelekezo.

Kwa upande wake Katibu wa CCM mkoa wa Pwani,Bernard Ghaty amesema kipindi wanatoa ahadi katika ilani ya CCM waliwaambia Wananchi watadhibiti ukataji wa miti hovyo na kutengeneza mazingira ambayo ni Suluhu.

Alisema kwa vitendo Waziri Jaffo ameweza kutekeleza agizo hilo kwa kuhakikisha amegawa majiko ya gesi kwa watendaji wa CCM pamoja na wadau wengine ili wakawe mifano kwa watu wengine kuhakikisha wanatunza mazingira.

“Ni jambo la heshima,msingi na kuigwa kw akufata mfano wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha nchi inatunza mazingira na kuiga mfano wa Waziri Jaffo katika kuhakikisha

 Mtaalamu wa Maabara wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Bw. Peter Mwevila amesema swala la mawasiliano baina ya watoa huduma za afya ni muhimu katika kupata vipimo sahihi vya mgonjwa.

Bw. Mwavila ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo katika majengo ya Taasisi ya Saratani Ocean Road alipokuwa akiwasilisha mada inayosema “Sample Collection” katika uwasilishaji wa “Continues Medical Education” (CME).

Aidha Bw. Mwevila ameongeza kuwa katika uchukuaji wa “sample” kutoka kwa mgonjwa ni lazima kuzingatia maelekezo ya kila kipimo kinachohitajika kwa kuwa kila kipimo kina utaratibu wake.

Pamoja na hayo Bw. Mwevila ameongeza kuwa iwapo sample imecheleweshwa kufikishwa kwenye maabara au “sample” imehifadhiwa katika kifaa kisicho sahihi, itabidi kuchukuliwa “sample” nyingine ili kupata vipimo hitajika.

Taasisi ya Saratani Ocean Road imekuwa ikitoa fursa kwa idara na vitengo vya ndani na nje ya Taasisi katika kuwasilisha mada mbalimbali kwa watumishi wake, ili waweze kujenga uelewa wa pamoja.

 Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo ametembelea Taasisi ya Saratani Ocean Road na kuzungumza na baadhi ya watumishi, huku akiupongeza uongozi wa Taasisi hiyo kwa kusimamia vizuri pesa zinazotolewa na serikali kwaajili ya miradi mbalimbali.

Dkt. Mollel amesisitiza kuwa ujenzi wa jengo mfano la Cyclotron ukiliangalia kwa nje unaweza Sema limegharimu kiasi kidogo sana cha pesa ila kwa ndani ndio utagundua thamani ya pesa iliyotumika kuwa inaendana na ubora na umadhubuti wa jengo lenyewe.

Dkt. Mollel ameomba uharaka wa umaliziaji wa jengo hilo ufanyike kwani watanzania wanahitaji huduma zake mapema iwezekanavyo huku serikali ikitaka uwekezaji wake uanze kuleta tija kwa wananchi.

Nae mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt Julius Mwaiselage, amemhakikishia Dkt. Mollel kumalizika mapema kwa ujenzi huo kwani kwa upande wa jengo limekamilika kwa Asilimia tisini na nane wakati mashine tayari zimekwishasimikwa kwa asilimia Mia moja huku ukisubiriwa utaratibu wa kuunganisha umeme pekee ili mashine hizo zianze kutumika kama inavyotakiwa.

Jengo hilo limekusanya mashine mbili kubwa ambazo ni PET-CT SCAN pamoja na CYCLOTRON (kiwanda cha kutengeneza mionzi) ambapo kwa sasa kwa Tanzania nzima kitakuwa ni kimoja tu, ambacho kitakuwa kikitengeneza mionzi ambayo itatumika kwa Taasisi huku mingine ikipelekwa kwenye hospitali nyingine kwaajili ya kusaidia wahanga wa huko. Kwa sasa Taasisi inanunua mionzi hiyo kutoka Afrika ya Kusini huku gharama zake zikiwa kubwa mno ukilinganisha na uwezo wa watanzania wenyewe, hivyo kukamilika kwa usimikaji huo kutakuwa msaada mkubwa sana kwa Tanzania na Afrika mashariki na kati kwa ujumla.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wananchi kufanya uchunguzi wa awali wa kupima Saratani ya Matiti ili kujua hali zao na kupata matibabu mapema kwa wenye changamoto hiyo

Waziri Ummy ameyasema hayo Octoba Mosi, 2023 wakati akimuwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kwenye Maadhimisho ya Mwezi wa Saratani ya Matiti yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi ya Saratani Ocean Road Jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy amesema Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa Saratani takribani Elfu Arobaini na Mbili (42,000) kila Mwaka ndio wanafika katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

Pia, Waziri Ummy amesema taarifa ya mwaka 2022/2023, inaonesha kuwa Taasisi ya Saratani Ocean Road ilihudumia wagonjwa wapya takriban 8,779 na asilimia 13 ya wagonjwa hao sawa na wagonjwa 1,141 walikuwa na Saratani ya Matiti.

Sambamba na hayo, Waziri Ummy amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Wizara ya Afya kufunga mashine za CT-Scan katika Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na mashine za Ultrasound katika Hospitali zote za Halmashauri nchini.

Nae mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha matibabu kwa kutuletea vifaa tiba vya kutosha kwaajili ya uchunguzi wa Saratani mbalimbali ikiwamo PET-CT huku maahine ya Cyclotron ikiwepo kwaajili ya kuzalisha mionzi tiba itakayo tumika hapa kwenye Taasisi huku bakaa ikipangwa kupelekwa kwenye maeneo mengine kwaajili ya kusaidia watanzania wengine.

Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka ifikapo mwezi wa kumia mabapo watu duniani kote huungana kupingana na ushambulizi wa aina yoyote wa Saratani hii huku ikiwasaidia wananchi waliokwisha athirika na ugonjwa huo kupata matibabu