Thursday, 15 February 2024

SUPA JACKPOT YAZIDI KUACHILIA MABILIONI KWA WASHINDI

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas amemtangaza David Mwenge Nyantora kuwa mshindi wa Super Jackpot ya mechi 13 akiwa amejishindia shilingi 265,780,681. ikiwa ni takribani miezi 11 tangu kumtangaza mshindi wa mwisho wa Supa Jackpot mechi hizihizi 13 ambapo hii ni awamu ya pili kupata mshindi wa Supa Jackpot tangu ianzishwe rasmi.

hili ni jambo la kihistoria kwa kampuni ya kubashri kupata zaidi ya washindi wa Jackpot 10 na kuwatangaza kwa miaka 6 mfululizo. Supa Jackpot ya wiki hii imeweza kutoa washindi wa bonasi jumla ya 8708 huku jumla ya bonasi zilizotolewa ikiwa ni zaidi ya milioni 756.

Naye mshindi alikuwa na haya ya kuongea, Akizungumza katika hafla hiyo maalumu iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, Dar es Salaam, David anasema alianza kucheza na SportPesa mwaka 2018, baada ya kuifahamu kupitia usomaji wa magazeti, amewashauli Watanzania waendelee kucheza na SportPesa.

Naye Mkuu wa kitengo cha Uhusiani na Mawasiliano wa SportPesa Sabrina H. Msuya alimpongeza mshindi na kumhimiza kuwa balozi kwa wengine. Anawakumbusha Watanzania Supa Jackpot ipo na itaendelea kuwepo kutegemeaa na matokeo ya kila wiki. endeleeni kutuamini kama ambavyo, David ametuamini na matokeo ya ushindi mtayapata. amesema haya wakati wa kumtangaza mshindi wa Supa Jackpot David Mwenge Nyantora.

Habari Picha na Victoria Stanslaus

Thursday, 8 February 2024

UZINDUZI MAALUMU WA KADI ZA WANACHAMA WA YANGA HII NI YAKIMATAIFA

Mkurugenzi wa Biashara na Wateja Binafsi wa benki ya NMB, Filbert Mponzi amesema wamefungua tawi Sengerema kwa ajili ya kuwaudumia wanachama wa Yanga hivyo amewataka kujisajili kwa wingi kwa kulipa Ada NMB watanufaika na Yanga watanufaika, ameongezea kwa kusema ukiona NMB umeliona tawi la YANGA

Habari na Victoria Stanslaus

UZINDUZI WA KADI MAALUMU ZA WANANACHAMA WA YANGA

 


Rais wa Yanga Eng. Hersi Said amewataka wanachama kujisajili kwenye Benki ya NMB na kufungua Akaunti zao ambapo amesema Ada yake ni shiringi 1,000,000/= ya Kitanzania na mwaka mmoja ukiisha unaweza kuirenew kwa shilingi 25000/= ambapo ameelezea faida zake, kwanza Taasisi zote mbili zitanufaika

1) Jezi sita (6) kila msimu /na VIP Tiket 10 mechi ya nyumbani.

2) Punguzo hadi asilimia kumi ukifanya malipo ya kadi kwa QR.

3) VIP Lounge viwanja vya ndege vya kimataifa bure.

Hizi ndiyo faida ya kadi maalumu za wanachama wa Yanga.

Habari Picha na Victoria Stanslaus

Tuesday, 6 February 2024

TANROADS YAPOKEA MAKAMPUNI MATATU


Eng. Kitainda Hamed Michael meneja wa miradi ya Ubia kati ya Serikali na sekta Binafsi TANROADS amesema mwezi wa tatu walitangaza Tenda wamejitokeza China, Uturuki na wengine kampuni zilizorudisha tenda ni kampuni tatu zote kutoka China wanalipia huduma,katika makampuni matatu inahitajika kampuni moja tu. Serikali ikishindwa kutoa huduma wanatumia sekta binafsi kuchangia.

amesema changamoto ipo barabra ya morogoro road kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro wanatumia masaa sita na ajari za kila siku hivyo zitakoma itakapojengwa Barabra ya express, itakuwa barabara ya viwango vya juu na manufaa yake kuokoa mafuata, vipuli vya magari na afya za waendeshaji ambapo itapelekea mwananchi kupata huduma iliyo bora na uchumi kuongezeka.

TANROADS imefungua Tenda ya Barabara kutoka Kibaha hadi Chalinze, Tender inasehemu tatu na watapokea Proposal. katika sekta binafsi wamewekeza 100% katika kuchangia huduma ya barabara, serikali kupata mitaji sekta binafsi ili kujenga barabara hii inasaidia kukuza uchumi wa nchi.

Habari na Victoria Stanslaus

Friday, 2 February 2024

AZAM TV YAFUNGUA MIRANGO KWA WASANII WA FILAMU NCHINI

Bi Sophia amesema Filamu ya Toboa Tobo imekuja kipekee kwenye soko ambayo itaanza kuonyeshwa kuanzia tarehe 09/02/2024 saa 1:30 usiku. Pia ametoa nafasi kwa Watanzania kupeleke Filamu zao walizoandaa, kwani taasisi yao ni ya kizalendo popote ulipo unaweza kuwasilisha kazi yako Azam ili kuleta ushindani.

Kwenye kutuma Tamthili video ziwe fupi wakumbuke sizidi iwe chini ya dakika 90 mbayo utawasilisha nyaraka kama vyeti, na demo, kuandika majina na nafasi zao kwenye filamu amesema haya kwenye uzinduzi wa filamu ya Toboa tobo.

Habari na Victoria Stanslaus

FILAMU YA TOBOA TOBO YAJA KIVINGINE

Muandaaji wa Filamu ya Toboa Tobo Devota Mayunga ameishukuru familia yake kwa kumuunga mkono katika kazi yake ya uhandishi hatimae kuandaa tamsria hiitayo Toboa Tobo filamu iliyojaa visa, vituko na mambo kemkem pia amewashukuru AZAM TV kwa kuikubali kazi yake kwa mara ya kwanza ambako mwaka 2016 alipata tunzo ya muandishi bora.

Habari na Victoria Stanslaus

WASANII WA FILAMU CHIPUKIZI KUJA KWA KASI

Dr. Cheni amesema miaka hiyo walifanya sanaa kwa kuipenda, kwa sasa wanafanya kama kazi. amesema mashabiki kwa kuendelea kuwa pamoja nao, Ombi kwa Toboatobo wanawapa nafasi kwa kuwakaribisha kufanya biashara, wakifanya masihara watamyumbisha producer amewaomba kumpa ushirikiano producer, amemuomba producer kutoa taarifa kwa wasanii viburi ambao wakishapata jina wanakuatena majeuri awawezi tena kufanya kazi.

ameomba wasanii kushirikiana vizuri kwenye kazi maana kukosana kupo. amewashukuru Azam Tv kwa kufanya kazi mzuri kama Tamthiria ya Mtaa wa Kaza moyo na bado wanaendelea kupokea filamu nyengine, amewaomba mashabiki wa mtaa wa kaza moyo waendelee kuangalia tamthiria ya Toboatobo kwani ni tamthiria mzuri. 

Wito kwa wasanii kuacha viburi badala yake wafanye kazi hata kama watapata majina makubwa.

Habari na Victoria Stanslaus