Habari picha na Ally Thabit
Thursday, 6 June 2024
WANAFUNZI WA CHUO CHA UTUMISHI WAAHIDI MAZITO
Wednesday, 5 June 2024
TGNP YAPONGEZWA NA KAMISHNA WA UHAMIAJI TANZANIA
Kamishna wa Uhamiaji wamewatia moyo TGNP kwa kazi yao mzuri wanayoifanya hivyo amewataka wanawake nchini kutokata tamaa na kubweteka na badala yake wachangamkie fursa mbalimbali ikiwemo kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu 2024 na uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwaka 2025 lengo waweze kushika nafasi kubwa za maamuzi ili waweze kutatua changamoto zinazo wakabiri kwani wanawake wanauwezo mkubwa wa kuongoza mfano Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassani ambae ni mchapa kazi mzuri na ameweza kuifungua Tanzania kimataifa na kukuza Diplomasia kiuchumi ametoa wito kwa jamii na wanasiasa kuacha mila na desturi potofu na kandamizi zidi ya wanawake na kuondoa mfumo dume kwenye vyama vya siasa na katika jamii pindi wanawake wanapogombea nafasi za uwongozi na wawepe ruhusa kwa kugombea kwenye uwongozi, amesema haya jijimi Dar es Salaam nilipofanyanae maojiano.
Habari picha na Ally Thabiti
LATRA YATOA VYETI KWA MADEREVA 1518
Pia mkurugenzi mkuu mtendaji wa Latra amesema madereva wanafundishwa kutambua watu wenye ulemavu pamoja na kuheshimu arama zao amesema haya jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji vyeti vya madereva 1518.
Habari Picha na Ally Thabiti.
SCHAOLASTICA PEMBE MRATIBU WA TAASISI TANZANIA COALITION AGAINST CHILD LABOUR APIGA VITA UTEKWAJI NA UKATWAJI WA VIUNGO VYA WATU WENYE ULEMAVU
Pia Jeshi la Polisi lifanye jitihada za makusudi za kumtafuta mpaka wampate mtoto mwenye Ualbino mtoto huyu Asimwe Novati. Scholastica Pembe Mratibu wa Taasisi Tanzania Coalition Against Child Labour ametoa wito kwa jamii wahache mila na desturi potofo na kandamizi zidi ya watu wenye Ualbino pia ametoa rai kwa waganga wa kienyeji kuacha ramli chonganishi.
Habari Picha na Victoria Stanslaus.
EXECUTIVE DIRECTOR CLEMENCE MWOMBEKI WA TAASISI YA DOOR OF HOPE TO WOMEN AND YOUTH TANZANIA (DHWYT) ABAINISHA MIKAKATI YA KUTOKOMEZA AJIRA KWA WATOTO
Richa ya serikali kuingia mikataba mbalimbali ya kitaifa na kimataifa lakini bado wimbi la ajira za watoto zimekuwa kubwa sana kwenye sekta mbalimbali, migodini, kwenye kilimo, masokoni, viwandani na maeneo mengineyo hata hivyo wanaharakati na wadau wanaopinga ajira za watoto wameweza kundi la watoto wenye ulemavu pamoja na wazazi na walezi wenye ulemavu ili nao waondokane na mazira ya ajira kwa watoto.
Executive Director Clemence Mwombeki wa Taasisi ya Door of Hope to Women and Youth Tanzania (DHWYT) ameraani vikali na kukemea vitendo vya utekwaji na ukatwaji wa viungo vya watu wenye Ualbino ameitaka serikali kuwatafuta na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote waliohusika kumteka mtoto mwenye Ualbino miaka miwili na nusu Asimwe Novati wa mkoani Kagera Tanzania pia serikali kupitia vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na jeshi la polisi lifanye jitihada za makusudi za kumtafuta mtoto huyu mwenye Ualbino Asimwe Novati. Amesema haya Jijini Dar es Salaam.
Habari Picha na Ally Thabiti.
CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO MKOA WA DAR ES SALAAM KUONANA NA RAIS SAMIA
Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ualbino Mkoa wa Dar es Salaam Gabriel Aluga amesikitishwa vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watu wenye Ualbino na amelaani vikali kutekwa kwa mtoto mwenye Ualbino mwenye miaka miwili na nusu ASIMWE NOVAT wa mkoani Kagera Tanzania.
Hivyo kwa pamoja watu wenye Ualbino wanaomba kuonana na Rais Kdt Samia Suluhu Hasani ili wafikishe kilio chao na mateso wanayopa watu wenye Ualbino, mwenyekiti amemtaka spika wa bunge la Tanzania pamoja na wabunge kupitia bunge linaloendelea hivi sasa watoe tamko la kuraani na kukemea utekwaji na ukatwaji wa viungo vya watu wenye Ualbino pia mwenye amesema tarehe 12/06/2024 wilaya kibaha mkoani Pwani kutakuwa na kongamano kubwa la watu wenye Ualbino.
Habari Picha na Ally Thabiti
CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO TANZANIA (TAS) CHA KEMEA VIKALI UTEKWAJI WA WATU WENYE UALBINO
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Ualbino Taifa Godfrey Molel ameitaka serikali kuwakamata na kuwachukulia hatua kari watu walio mteka mtoto mwenye ualbino mwenye umri wa miaka miwili na nusu anaejulikana kwa jina la Asimwe Novat mkoani Kagera wilia ya Karagwe ambae mpaka sasa mtoto huyo ajulikani alipo.
Hivyo chama cha watu wenye ualbino wanavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha mtoto huyu anapatikana akiwa hai huku chama hiki kikimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Kamilius Wambura waende wakaweke kambi ili wawasake watu waliomteka mtoto Asimwe Novat, hata hivyo chama hiki kinamuomba Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan atoe tamko la kukomesha na kuraani vitendo vya mauaji na ukatwaji wa viungo vya watu wenye Ualbino kwani watu wenye Ualbino wanahaki ya kuishi kama watu wengine mesema haya makao makuu ya chama cha watu wenye Ualbino Taifa jijini Dar es Salaam walivyokutana na wana habari.
Habari picha na Ally Thabiti






