Richa ya serikali kuingia mikataba mbalimbali ya kitaifa na kimataifa lakini bado wimbi la ajira za watoto zimekuwa kubwa sana kwenye sekta mbalimbali, migodini, kwenye kilimo, masokoni, viwandani na maeneo mengineyo hata hivyo wanaharakati na wadau wanaopinga ajira za watoto wameweza kundi la watoto wenye ulemavu pamoja na wazazi na walezi wenye ulemavu ili nao waondokane na mazira ya ajira kwa watoto.
Executive Director Clemence Mwombeki wa Taasisi ya Door of Hope to Women and Youth Tanzania (DHWYT) ameraani vikali na kukemea vitendo vya utekwaji na ukatwaji wa viungo vya watu wenye Ualbino ameitaka serikali kuwatafuta na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote waliohusika kumteka mtoto mwenye Ualbino miaka miwili na nusu Asimwe Novati wa mkoani Kagera Tanzania pia serikali kupitia vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na jeshi la polisi lifanye jitihada za makusudi za kumtafuta mtoto huyu mwenye Ualbino Asimwe Novati. Amesema haya Jijini Dar es Salaam.
Habari Picha na Ally Thabiti.
No comments:
Post a Comment