Tuesday, 11 June 2024

TGNP WAITAKA SERIKALI KUTENGA BAJETI YENYE MLENGO WA KIJINSIA

WILFRED KULWA Afisa mtafiti na mchambuzi wa maswala ya kiuchumi na jinsia TGNP amesema serikali itenge majeti yenye mlengo wa kijinsia kwenye wizara zote ili kuondoa ombwe kwenye maswala ya kijinsia  pia TGNP inaofu kuwa bajeti ya mwaka huu kiasi kikubwa cha fedha kitaelekezwa kwenye maswala ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao hivyo wanaitaka serikali fedha zielekezwe katika kutoa elimu kwa wanawake ili wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi za uwongozi wa wenyekiti wa serikali za Mitaa, Ubunge, Udiwani na Urais ili wawe na fursa ya kufanya maamuzi makubwa vilevile bajeti hii pesa nyingi zitaelekeza kwenye maandalizi ya dira mpya ya maendeleo ya Taifa ya miaka 50 ijayo.

TGNP yaitaka serikali ihusishe makundi maalumu katika utowaji wa maoni ya dira mpya ijayo kwani dira tuliyonayo aijazingatia makundi maalumu na mlengo wa kijinsia Wilfred Kulwa ameipongeza serikali kwenye wizara ya afya kwa kuweza kununua Ambulance kwani zitaokoa maisha ya mama na mtoto kipindi wanavyokwenda hospitali kujifungua swala la kuongeza muda wa mapunziko wakati anapojifungua mtumishi wa serikali ni jambo zuri na serikali kutenga fedha kwaajili ya bima za afya kwa wote ni jambo zuri.

Kwa upande wa wizara ya elimu serikali ifanye maboresho kwenye sera ya elimu kwenye upande wa matundu ya vyoo kwani sera iliyopo aioneshi mlengo na maitaji ya kijinsia kwenye matundu ya vyoo ambapo kuna ombwe kubwa kwa wanafunzi wa kike kupata idadi chache kwa matundu ya choo ikilinganisha na wanafunzi wa kiume, swala ya elimu ya amali ni muhimu ila serikali itenge fedha nyingi kwa ajili ya mafunzo kwa walimu ili kuwepo na mlengo na maitaji ya kijinsia kati ya mwalimu na mwanafunzi, huku TGNP wakiipongeza serikali kwa kuweza kuongeza fedha ya mikopo kwan elimu ya juu.

Bwana Wilfred Kulwa amesema wizara ya kilimo iyakikishe mladi wa BBT iweke mgawanyo wa kijinsia katika utoaji wa mbegu yatilifu na mikopo ya kilimo iwafikie wanawake, ametoa wito kwa serikali kuhakikisha mikopo inayokopwa na serikali iwe ya masharti nafuu na isiwe na vikwazo vigumu ili isituletee matatizo kama mikopo ya miaka ya nyuma japokuwa deni la taifa ni imilivu.

Amesema haya makao makuu ya TGNP Mabibo jiji Dar es Salaam nilipofanyanae maojiano.


Habari Picha na Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment