MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ,AWAONYA NA KUWATADHALISHA WAFANYA BIASHARA
ALBART CHARAMILA , amewataka wafanya biashara wa Kariakoo na Wafanyabiashara kwa Ujumla waache mara moja mpango wao wakutaka kugoma kufungua Maduka kwani kufanya hivyo ni kukiyuka sheria , kanuni , na Taratibu za Nchi kwani madai waliyoyatoa mbele ya Waziri mkuu ,yamefanyiwa kazi kupitia wizara ya fedha , wizara ya viwanda na Biashara na Taasisi zingine za Serekali . swala la kodi ya VAT na Service Review , inafanyiwa kazi kupitia wabunge kila mtumishi wa Serekali anamadai ya serekali kama wao wafanyabiashara lakini hawajachukua maamuzi ya Mgomo .
Pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amewataka wafanya biashara kuwasilisha serekalini fedha za kodi wanazokusanya kwa wezao amewataka wafanya biashara kutokubali kutumika na wana Siasa ili wagome , na badala yake waendelee kufanya biashara zao ,amewatoa hofu wafanya Biashara wote ,
Soko lililoungua la Kariakoo lilojengwa na Rais Dr. Samia suluhu Hassani kwa kiasi cha fedha Bilioni 28, tena fedha za kodi Watanzania , litafunguliwa karibuni na Rais Dr Samia na kila mmoja atapata kizimba au Duka la kuuza Bidhaa zake katika soko hilo.
kikubwa mtu afuate sheria na Taaratibu za kuingia katika Soko hilo ametoa wito kwa wana Dar es salaam kutoshabikia wa kushadadia Mgomo wa wafanya biashara na waache ,kusasmbaza Jumbe za Mgomo
Amesema haya jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari,
No comments:
Post a Comment