Rais Mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya nne 4 Dr Kikwete anawapongoza waandaaji wa mbio za Msoga Marathon kwani ubunifu huu ni mzuri na unatija kubwa kwenye sekta ya Afya ambako fedha zilizopatikana zitawezesha kwa kiwango kikubwa kupunguza vifo kwa kinamama wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua Na kununua vifaa vya kuwawezesha watoto wanaozaliwa kabla ya miezi tisa kutimia .
Rais Dr Kikwete anawatia moyo waandaaji na kuwataka kutokata tamaa na mbio hizi za Msoga Marathon ziwe endelevu ma zifanyike kila mwaka ''amempongeza mbunge wa Chalinze Riziwani Kikwete na wenzake kuamasisha watu kujitokeza kwa wingi kwenye mbio za Msoga Marathon.
Ametoa wito kwa watu wote wawe namoyo wa kuwasaidia watu wenye uhitaji amesema haya wilayani Chalinze kata ya Msoga kijiji cha Msoga mkoani pwani kwenye mbio za Msoga Marathon.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment