Sunday, 9 June 2024

WAFANYA BIASHARA WAMUONYA NA KUMTAADHARISHA KAMISHINA MKUU WA TRA


 Katibu Mkuu wa Umoja wa Wafanyabiashara Peter Mbilinyi anamtaka kamishina mkuu wa tra tanzania aache kuwakumbatia wanasiasa mfano kuna mwanasiasa amegawa majiko ya gesi kwa wafanya biashara ambao awalipi kodi kariakoo pia amewataka viongozi wa Halmashauri ya Ilala waache kuwatumia wafanyabiashara ambao awalipi kodi.

Peter Mbilinyi amewataka wafanya biashara wajitokeze kwa wingi kwenye mkutano utakao fanyika ukumbi wa Anatogo tarehe 13/6/2024 lengo kujadili mambo waliokubaliana na waziri mkuu na kupitia changamoto zilizokuwa zinawakabili wafanya biashara kipindi cha mgomo.

Ameitaka serikali kuwasajili wafanya biashara elfu 20000 waliopo kariakoo ili waweze kulipa kodi, vilevile serikali ikusanye kodi bandarini ili kuondoa usumbufu kwa wafanyabiashara. Umoja wa wafanyabiashara kariakoo unawafanyabiashara elfu 30000 ambao wamesajiliwa .

Habari picha na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment