Daud Goodluck Daudi Executive Secretary amesema elimu inayotolewa na Latra ccc dar es salaam inazingatia kwa kiasi kikubwa makundi ya watu wenye ulemavu mbalimbali mfano kuna vipeperushi vya maandishi ya nukta nundu kwaajili ya watu wasio ona pia kwenye usafili wa mabasi ya mwendo kasi kwenye mabasi kuna viti vya watu wenye ulemavu wanawake wajawazito na wazee .
pia kwenye vituo vya mwendo kasi miundombinu ni rafiki na wezeshi kwa makundi yote hata watoa huduma wake wana uwezo wa kuwahudumia watu wenye ulemavu na makundi mengine. LATRA CCC dar es salaam inatoa elimu kwa madereva bodaboda,bajaji na daradara ili kuepukana na ajali .
Amekipongeza chuo cha NIT,CBE kwa mafunzo wanayoyatoa ya udereva kwa madereva pia ameipongeza Hospitali ya taifa muhimbili kwa kuingia makubaliano na chuo cha taifa cha usafilishaji NIT kwani ushirikiano wao utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguwa kwa ajali nchini .
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment