Tuesday, 25 June 2024

PROF LADSLAUS MNYENE ATOASIRI NZITO ELIMU KIDIGITALI


 Mkurugenzi wa  Idara ya Sayansi na Teknolojia Wizara ya Elimu Prof Ladslaus Mnyane  amesema Utoaji elimu kwanjia ya kidigitali kuanzia elimu ya Awali ,msingi ,secondary na vyuo vikuu itasidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufundishwa masomo kwa muda mfupi wakiwa wengi,walimu watafundisha wanafunzi kwa uchache wao,itapunguza gharama kwa serikali kwa kutoajili walimu wengi.

Katika mabadiliko ya kiteknolojia duniani tanzania tukiwafundisha wanafunzi kwa njia za kidigitali itawawezesha wanafunzi baada ya kumaliza shule na vyuo vikuu watakuwa wameshabobea katika matumizi ya kidigitali . Hivyo ufanisi utaongezeka kwa kiasi kikubwa katika utendaji kazi kwenye sekta mbalimbali mfano kwenye sekta ya madini,sekita ya kilimo,sekta za maji na sekta zinginezo.

Prof Ladslaus Mnyane amesema lengo la kutoa elimu kwa njia ya kidigitali kuwezesha watanzania kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia ya sasa na ya baadae,pia wanatarajia serikali na watu binaus kutekeleza mpango huu kwa vitendo  ifikapo mwezi7/2025  .Swala la kujumuisha na kushirikisha kundi la watu wenye ulemavu ili wapate elimu kwa nia ya kidigitali ni jambo muhimu na linatija kwa tanzania amesema haya jijini dar es salaam kwenye mjadala wa kupokea maoni kwa wadau wa elimu  kwa namna gani ya kukamilisha mpango wa kutoa elimu kwa njia ya kidigitali.

Habari picha na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment