Wednesday, 5 June 2024

CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO MKOA WA DAR ES SALAAM KUONANA NA RAIS SAMIA

Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ualbino Mkoa wa Dar es Salaam Gabriel Aluga amesikitishwa vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watu wenye Ualbino na amelaani vikali kutekwa kwa mtoto mwenye Ualbino mwenye miaka miwili na nusu ASIMWE NOVAT wa mkoani Kagera Tanzania.

Hivyo kwa pamoja watu wenye Ualbino wanaomba kuonana na Rais Kdt Samia Suluhu Hasani ili wafikishe kilio chao  na mateso wanayopa watu wenye Ualbino, mwenyekiti amemtaka spika wa bunge la Tanzania pamoja na wabunge kupitia bunge linaloendelea hivi sasa watoe tamko la kuraani na kukemea utekwaji na ukatwaji wa viungo vya watu wenye Ualbino pia mwenye amesema tarehe 12/06/2024 wilaya kibaha mkoani Pwani kutakuwa na kongamano kubwa la watu wenye Ualbino.

Habari Picha na Ally Thabiti

 

No comments:

Post a Comment