Wednesday, 5 June 2024

CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO TANZANIA (TAS) CHA KEMEA VIKALI UTEKWAJI WA WATU WENYE UALBINO

Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Ualbino Taifa Godfrey Molel ameitaka serikali kuwakamata na kuwachukulia hatua kari watu walio mteka mtoto mwenye ualbino mwenye umri wa miaka miwili na nusu anaejulikana kwa jina la Asimwe Novat mkoani Kagera wilia ya Karagwe ambae mpaka sasa mtoto huyo ajulikani alipo.

Hivyo chama cha watu wenye ualbino wanavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha mtoto huyu anapatikana akiwa hai huku chama hiki kikimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Kamilius Wambura waende wakaweke kambi ili wawasake watu waliomteka mtoto Asimwe Novat, hata hivyo chama hiki kinamuomba Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan atoe tamko la kukomesha na kuraani vitendo vya mauaji na ukatwaji wa viungo vya watu wenye Ualbino kwani watu wenye Ualbino wanahaki ya kuishi kama watu wengine mesema haya makao makuu ya chama cha watu wenye Ualbino Taifa jijini Dar es Salaam walivyokutana na wana habari.



Habari picha na Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment