Thursday, 9 May 2019

FORUM CC YAJA NA MWAROBAINI WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI


Mkurugenzi mtendaji wa FURUM CC Rebeka Muna amesema ilituwe kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ni vyema serikali iweke sela mazubuti kwa kila wizara zitazohusu juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi pia asasi mbalimbali za kiraia na zisizo za kiraia zisisite kupaza sauti na kutoa elimu kwa jamii ya vijijini na mijini juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Pia amezungumzia swala la Nishati ya mkaa na ameitaka serikali kutekeleza kwa vitendo mkataba wa makubaliano juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi uliosainiwa mwaka 2015 nchini Ufarasa na serikali ukalizia kutekeleza mkataba huu.

Pia ameitaka serikali itumie tafiti na ripoti zinazotolewa na asasi mbalimbali ikiwemo FORUM CC kwani tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa kukabiliana na kuondoa tatizo la madiliko ya tabia ya nchi hapa nchi pia ametoa wito kwa serikali sela ya mabadiliko ya tabia ya nchi zilizopo wizara ya kilimo na nishati zifanyiwe mabadiliko kwani aziendani na wakati wa sasa na wizara azina sela za mabadiliko ya tabia ya nchi  ziwekewe ndipo tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Amesema haya jijini Dar es salaam kwenye kongamano la wadau wa mabadiliko ya tabia ya nchi.

Habari Picha na
Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment