Saturday, 21 January 2023

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AIMIZA ULIPAJI WA FEDHA


 Naibu Waziri wa Fedha  na Mipango (JMT).Hamad Hassan Chande amewataka wazanzibar kulipa Kodi  kwani ndio maendeleo yatapatikana kama Husuma za Afya ,Elimu na Miundombinu. Amesema kongamano la kikodi litaleta tija Kwa kupanga bajeti yenye Usawa.

Habari na Ally Thabiti

WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA KONGAMANO LA KODI ZANZIBAR

 Dkt Saada Mkuya Salim Waziri wa Fedha Ofisi ya RĂ is Fedha na Mipango amesema Lengo la kongamano la Kodi ni kuboresha mifumo ya Kodi na kuiwezesha Zanzibar kukusanya Fedha za kutosha ivyo amewataka wazanzibar kutoa mawazo yao.

Habari na Ally Thabiti

Thursday, 19 January 2023

MKURUGENZI WAHOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI AIMIZA UWAZI NA UADILIFU KWENYE FEDHA ZA HIMOFILIIA


Prof Mohamed  Janabi amesema Mradi wa Ugonjwa wa Himofilia umesaidia Kwa kiasi kikubwa kuokoa Manisha ya watanzania ,ambako gharama zote za vipimo na matibabu zinatolewa na chama cha Himofilia ambako mgonjwa mmoja dawa zake milioni moja.

Kwa  mwaka zinaitajika milioni 4 Kwa mgonjwa mmoja Mradi huu ulianza tarehe 18/11/2020 ambako mpaka Sasa wagonjwa elfu sita wapi. Pia zimefunguliwa kiliniki mikoa mitano Mbeya ,Morogoro,Bugando,Dodoma na DSM ambako Kwa mwaka Jana watu 20 walifanyiwa tohara.

Prof Mohamed Janabi amekitaka chama cha Himofilia wawe wawazi na wawajibikaji ameo gezea Kwa kusema kuwa hospitali ya taifa ya muhimbili wako mbioni kuajili wataalamu wa Lugha ya Alama.

Habari na Ally Thabiti

Wednesday, 18 January 2023

KONGAMANO LA KODI KULETA MAFANIKIO TANZANIA

 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Lameck Nchemba  amesema kongamano la mabadiliko ya Sera ya Kodi itasaidia Kwa kiasi kikubwa kuongezeka Kwa walipa Kodi Tanzania .

Habari na Ally Thabiti

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA ,BIASHARA NA UWEKEZAJI AKIPONGEZA CHUO KIKUU CHA IFM

 Exaudi Kigae Naibu Waziri WA Viwanda na Biashara. Amesema Chuo Kikuu cha IFM kinatoa elimu ya maswala ya bima ,matumizi ya ICT katika kukuza uchumi wa kidigitali pia inawasaidia wajasiliamali wadogo nanna ya kuendesha na kukuza Biashara zao Kwa kutumia Tehama.

Ametoa wito Kwa kampuni za bima watoe elimu Kwa jamii umuhimu wa kukata bima  pia amekitaka Chuo cha IFM watengeneze wataalam wa ICT ambao watasaidia wawekezaji kuwekeza nchini na kudhibiti utapeli wa Biashara mtandaoni.


Nae Mkuu wa Chuo Kikuu cha IFM Prof Josephat Lotto amesema maadhisho ya miaka 50 ya Chuo Chao wanajivunia Kwa kuweza kutoa elimu Kwa wajasiliamali na kuwafundisha watu namna ya kukuza uchumi wao kidigitali, Pia Wana mpango wa kutoa elimu Kwa watu wenye ulemavu kuusiana na ujasilia mali.

Walikuwa wanatoa program mbili Chuo kilipoa za na Sasa zipo program 34 za masomo .

Habari na Ally Thabiti


Sunday, 15 January 2023


Picha 1 na b: Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.

Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wapya 57 (hawapo pichani) walioajiriwa na

Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kutoa huduma katika Taasisi hiyo

wakati akifungua mafunzo yaliyofanyika  leo katika ukumbi wa JKCI jijini Dar es Salaam.

 

Picha 2 & 2b: Baadhi ya Wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia

Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kituo cha kazi katika Taasisi ya Moyo Jakaya

Kikwete (JKCI) wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa mafunzo elekezi kwa

 wafanyakazi hao yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

 

Picha 3: Daktari bingwa wa upasuaji Alex Msoka akitoa neno la shukrani kwa niaba ya

wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira ambao

wamepangiwa kituo cha kazi katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa

mafunzo elekezi kwa  wafanyakazi yaliyofanyika  leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo

iliyopo jijini Dar es Salaam.

 

Picha 4: Afisa Utumishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kelvin Manyanga

akiwafundisha wajibu wa mtumishi wa umma wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na

Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kutoa huduma katika Taasisi hiyo

iliyopo jijini Dar es Salaam.

Picha na: Ally Thabith


HIZI HAPA HATUA ZILIZOFIKIWA NA BENKI KUU YA TANZANIA (BoT) KUHUSU FEDHA YA KIDIJITALI YA BENKI KUU

 


Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la ubunifu katika mifumo ya uendeshaji wa shughuli za kifedha duniani kote kutokana na maendeleo ya teknolojia. Mojawapo ya ubunifu unaotawala katika mijadala ya kisasa ya kisera ni fedha ya kidijitali ya benki kuu (Central Bank Digital Currency [CBDC]).

Ijapokuwa inafafanuliwa kwa njia mbalimbali, CBDC ni aina ya fedha ya kidijitali katika nchi inayotolewa na kudhibitiwa na benki kuu. Kwa hiyo, inapotolewa, CBDC inakuwa fedha halali, sawa na fedha ya kawaida inayoshikika. Kulingana na maandiko mbalimbali ya kitaalamu, CBDC inaelezwa kuwa na faida nyingi kwa uchumi.

Kwa kuzingatia ukweli kwamba CBDC inaweza tu kutolewa na benki kuu, hivyo, kuwa chini ya mamlaka yake, Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikitafiti uwezekano wa kutoa CBDC yake. Katika hatua hii ya utafiti, Benki Kuu ya Tanzania iliunda timu ya wataalamu wa fani mbalimbali kuchunguza vipengele vya kiutendaji vya CBDC na kuijengea uwezo timu hiyo kwa njia mbalimbali.

 Pia, katika kuongeza uelewa wa CBDC kwa umma, Benki Kuu ya Tanzania iliandaa Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha nchini Tanzania mwaka 2021 ukiwa na mada kuhusu CBDC na fedha za kidijitali (crypto). Aidha, Benki Kuu ya Tanzania ilikutana na wadau wa sekta ya fedha nchini ili kupata maoni yao kuhusu suala hili. 

Pia, Benki Kuu imenufaika na mikutano mbalimbali ya kimataifa kama vile ya Kamati ya Magavana wa Benki Kuu ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Kamati ya Masuala ya Fedha ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) kupitia Kituo cha IMF cha kanda (IMF AFRITAC), na Muungano wa Benki Kuu za Afrika. Benki Kuu ya Tanzania pia ilifanya vikao kadhaa na kampuni binafsi za kimataifa zinazotoa miundombinu na ufundi kwa CBDC.

Mambo muhimu yaliyozingatiwa wakati wa hatua hii ya utafiti ambayo Benki Kuu ya Tanzania inaendelea nayo ni kuchagua namna inayofaa katika kutumia CBDC
 

kulingana na muktadha wa Tanzania. Hii inahusisha aina ya CBDC itakayotolewa (jumla, rejareja au mchanganyiko wa zote mbili), miundo ya utoaji na usimamizi (ya moja kwa moja, isiyo ya moja kwa moja, au ya mseto), aina ya CBDC (token-based au account based), muundo (remunerated au non-remunerated) na kiwango cha uwazi au ufuatiliaji. Aina itakayochaguliwa inapaswa kuzingatia vihatarishi vya utoaji wa fedha ya kidijitali ya benki kuu na njia za kudhibiti hivyo vitahatarishi katika utoaji na utumiaji wa fedha hiyo.

Matokeo ya utafiti uliofanywa na Benki Kuu ya Tanzania yalibainisha kuwa zaidi ya nchi 100 duniani ziko katika hatua tofauti za kutaka kutumia fedha ya kidijitali ya benki kuu, 88 zikiwa katika utafiti, 20 katika uthibitisho wa dhana, 13 katika majaribio na 3 katika uzinduzi. Uchambuzi wa matokeo haya unaonyesha kuwa benki kuu nyingi duniani zinakwenda kwa tahadhari katika utekelezaji wa mpango wao wa kutaka kutumia fedha ya kidijitali ya benki kuu (CBDC) ili kuepuka hatari zozote zinazoweza kuvuruga utulivu na usalama wa uchumi wao.

Pia, ilionekana kuwa, nchi 6 zilighairi kutumia CBDC hasa kutokana na changamoto za kimuundo na teknolojia katika awamu ya utekelezaji. Changamoto za kimuundo ni pamoja na kutumia fedha taslimu katika kufanya miamala, kuwepo kwa mifumo isiyofaa ya malipo, gharama kubwa ya utekelezaji na viashiria vya hatari vya mfumo wa utoaji wa fedha uliopo.

Katika kuzingatia hili, Benki Kuu ya Tanzania imeamua kutumia mbinu ya kwenda hatua kwa hatua, ikichukua tahadhari na kuzingatia vihatarishi katika kutumia fedha ya kidijitali ya benki kuu. Benki Kuu ya Tanzania itaendelea kufuatilia, kutafiti na kushirikiana na wadau, zikiwemo benki kuu nyingine, katika jitihada za kufikia matumizi ya fedha ya kidijitali ya benki kuu na kuchagua teknolojia stahiki kwa ajili ya utoaji wa

shilingi ya Tanzania katika mfumo wa kidijitali. Baada ya kuhitimisha awamu ya utafiti, Benki Kuu ya Tanzania itatoa taarifa kwa umma kwa ujumla juu ya namna ya kusonga mbele. Taarifa hiyo inaweza kujumuisha mpangokazi katika kuanzisha fedha ya kidijitali ya benki kuu (CBDC) nchini.