Thursday, 4 July 2024

NAIBU WAZIRI MKUU AKIPONGEZA CHUO CHA BAHARIA DMI

 Dr Dotto Mashaka  Biteko Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati amepongeza kazi nzuri na kubwa inayofanywa na chuo cha baharia (DMI) kwa kuandaa wataalam ambao watasaidia kukuza na kuomarisha uchumi wa bluu nchini tanzania pia amewataka wanafunzi wa chuo hichi kuzingatia wanayofundishwa na watafasiri kwa vitendo dhana ya uchumi wa bluu. 

Huku akiwataka washiriki wa kongamano la uchumi wa bluu watoe mawazo'ushauri'mipango na mikakati yakufikia uchumi wa bluu....amesema haya kwenye kongamano la siku mbili lenye kauli mbiu Kuunganisha Usalama Baharini'Utunzaji wa Mazingira na Maendeleo  ya Teknolojia Kwaajili ya Ukuzaji wa Uchumi wa Bluu  linalofanyika jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

MKURUGENZI WA AZAM MALRINE APONGEZA UCHUMI WA BLUU


 Abubakari Azizi Mkurugenzi  wa Azam Marine amesema Uchumi wa Bluu utasaidia kwa kiasi kikubwa kukuwa kwa uchumi wa tanzania kwa mtu mmoja mmoja  na taifa kwa ujumla anawataka watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kwenye bahari 'maziwa 'mito na mabwawa kwani wakifanya ivyo uchumi wao utaimarika .

Amekipongeza chuo cha  Mabaharia kwa kuunga mkono juhudi na jitihada za serikali katika kuelekea uchumi wa bluu kwa vitendo kwa kuandaa wataalamu kupitia chuo cha mabaharia (DMI) ....amesema haya kwenye kongamano la siku mbili  jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

ERASTO AIZAKI MWANAFUNZI CHUO CHA BAHARIA (DMI) AAHIIDI MAZITO TANZANIA KUELEKEA UCHUMI WA BLUU


 Mwanafunzi wa Chuo cha Baharia  cha (DMI) Erasto Aizaki Lamosai amesema Cheti na Zawadi alioipata kwaajili ya ubunifu alioufanya kwa kifaa cha kutambua matatizo yaliopo kwenye boti inavyokuwa inatembea ndani ya maji imemtia moyo na faraja kubwa  kwa kutambulika mchango wake kwenye Uchumi wa Bluu anaiomba serikali kifaa hiki kitumike pia ataakikisha anafanya bunifu zingine zenye tija na faida kwa nchi ya tanzania ili lengo na dhamira ya rais Dr Samia la uchumi wa bluu likamilike kwa vitendo .

Amesema haya kwenye kongamano la siku mbili linalojadili uchumi wa bluu  lenye kauli mbiu Kuunganisha Usalama Baharini'Utunzaji  Utunzaji wa mazingira na Maendeleo ya Teknolojia Kwaajili ya Ukuzaji wa Uchumi wa Bluu jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

MASAKA JULIUS MASAKA MWANAFUNZI WA CHUO CHA BAHARIA (DMI) ABUNI TEKNOLOJIA


 Mwanafunzi wa Chuo cha Baharia (DMI) Masaka Julius Masaka amebuni kifaa cha kubeba mizigo bandarini ivyo anaiomba serikali wamuunge mkono kwa teknolojia alioibuni kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za kununua vifaa vya kubeba mizigo nje ya nchi kwani kifaa shake kinauwezo wa kubeba content zenye mizigo.

Masaka Julius Masaka ameupongeza uongozi wa chuo cha baharia DMI  kwa elimu wanayoitoa yenye Ubora  amesema haya kwenye kongamano la siku mbili jijini dar es salaam  lenye kauli mbiu Kuunganisha Usalama Baharini'Utunzaji wa Mazingira  na Maendeleo ya Teknolojia Kwaajili ya Ukuzaji wa Uchumi wa Bluu. 

Habari picha na Ally Thabit 

MWANAFUNZI WA CHUO CHA BAHARIA (DMI) AUNGA MKONO UCHUMI WA BLUU


 Hamadi Mussa Hamadi Mwaanafunzi wa Chuo cha Baharia(DMI) amesema katika kuunga mkono juhudi na jitihada za serikali katika kuelekea uchumi wa bluu  yeye amefanya ubunifu wa limondi kwaajili ya kuwasha taa kwenye meli hii inasaidia kama kuna dhalura imetokea ndani ya meli unatumia limont kuwasha taa bila kufika eneo la tukio amesema haya kwenye kongamano la siku mbili  linalojadili uchumi wa bluu kwenye ukumbi wa mwalimu nyerere jijini dar es salaam. 

Ambako chuo cha baharia (DMI) kimeandaa kongamano ili la tatu lenye kauli mbiu Kuunganisha Usalama Baharini'Utunzaji wa Mazingira na Maendeleo ya Teknolojia Kwaajili  ya Ukuzaji wa Uchumi wa Bluu.

Habari picha na Ally Thabit 

TBS YAELEZA MIKAKATI YAO


 Emanuel wa Tbs  akiwa na Espekta  Maganga wa Ukaguzi wa Tbs  katika viwanja vya sabasaba  wamesema Tbs wanatoa elimu kwa jamii namna ya kutambua bidhaa feki na zilizoisha muda wakewa kutumika Tb imeimarisha mifumo na wametoa wito kwa jamii wafike kwenye viwanja vya sabasaba na watembelee banda la tbs ili wajifunze mambo mazuri kutoka Tbs  wamesema haya kwenye maonyesho ya 49 .

Habari  picha na Ally Thabit 

JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA LAWATOA OFU WATANZANIA

 LuteniKanali Gadetius Ilonda  amesema Jeshi la wananchi litaazimisha miaka 60 tangu lianzishwe mwaka 1964 katika maazimisho haya kutakuwa na shunguri mbalimbali za utoaji huduma za tibambalimbali kwa wananchi kwa magonjwa yote kwa wananchi ni bule ambako mikoa ya dar es salaam'Pwani'Tanga'Ruvuma'Mbeya 'Tabora'Zanzibar'Mwanza'Tabora pia kutakuwa na maonyesho ya tamad0uni lengo la maonyesho haya kuonesha mira na desturi  za watanzania .

Pia kutakuwa na Ujio wa Jeshi la Watu wa China ambako jeshi ili litatoa huduma za tiba kwenye meri yao ...lengo la ujio wachina kukuza demokrasia ya kijeshi nakukuza uchumi wa watanzania ametoa wito kwa wananchi kutokuwa na wasiwasi wala ofu watapokuwa wakiona vifaa vya kivita vya kijeshi kwenye maeneo  yao na miungurumo ya silaa nzito kwani maazimisho haya ya miaka60 ya jeshi la wananchi wa  tanzania litaendana na uchangiaji wa dam ivyo wanajeshi watachangia damu na wananchi wanaombwa kuchangia damu.

Lengo la uchangiaji wa dam ni kusambaza kwenye hospitali zote mchini kwaajili ya kuokoa maisha ya kinamama waojifungua na majerui.

Habari picha na Ally Thabit