Mwanafunzi wa Chuo cha Baharia cha (DMI) Erasto Aizaki Lamosai amesema Cheti na Zawadi alioipata kwaajili ya ubunifu alioufanya kwa kifaa cha kutambua matatizo yaliopo kwenye boti inavyokuwa inatembea ndani ya maji imemtia moyo na faraja kubwa kwa kutambulika mchango wake kwenye Uchumi wa Bluu anaiomba serikali kifaa hiki kitumike pia ataakikisha anafanya bunifu zingine zenye tija na faida kwa nchi ya tanzania ili lengo na dhamira ya rais Dr Samia la uchumi wa bluu likamilike kwa vitendo .
Amesema haya kwenye kongamano la siku mbili linalojadili uchumi wa bluu lenye kauli mbiu Kuunganisha Usalama Baharini'Utunzaji Utunzaji wa mazingira na Maendeleo ya Teknolojia Kwaajili ya Ukuzaji wa Uchumi wa Bluu jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment