Wednesday, 10 July 2024

MKURUGENZI MKUU MTENDAJI WA ESRF AELEZA UMUHIMU WA TAFITI

 

Prof Fotunata  Songora Makene Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji  wa Taasisi ya Utafiti ESRF amesema tafiti ni muhimu  kwani zinasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuleta maendeleo kwenye jamii kwenye sekta mbalimbali mfano Afya, Elimu na Kilimo .

Pia tafiti zinasaidia kwa kiasi kikubwa watu kuondokana na umasikini  ametoa wito kwa watunga sera kutumia tafiti zinazofanywa na watafiti ili serikali iweze kuboresha sheria, Kanuni taratibu na Miongozo ili kuwepo na mabadiliko na maendeleo katika jamii.

Mfano serikali ya tanzania itatoa mafunzo ya Amali kwenye secondary hapa nchini lengo wanafunzi wakimaliza shule ya secondary waweze kujiajili' kwani serikali imeweza kutumia mfumo huu baada ya watafiti kufanya  tafiti kwenye sekta ya elimu amesema haya kwenye mkutano wa Africa Evidence Summit jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment