Dr Tukae Mbegalo Muhadhiri Chuo kikuu Mzumbe amesema Kongamano ili la Africa Evidence Summit litasaidia kupata mbinu za kufanya tafiti na matumizi ya kisasa ya kiteknolojia ya kufanyia tafiti '' amesema tafiti zinawezesha kufanya mabadiliko ya kisera,sheria ,kanuni taratibu na miongozo.
Pia tafiti zinaongeza uelewa kwa makundi maalum ususani kwa watu wenye usonji na tafiti zinaonesha fursa mbalimbali katika jamii mfano kwenye kilimo na maeneo mengineyo. Tafiti zinakuza na kiboresha huduma za kijamii kama huduma za afya .
Chuo Kikuu cha Mzumbe kinafanya tafiti kwenye sekta ya Afya,Kilimo, Elimu,Utawala, Biashara,Sayansi na Teknolojia kwa upande wake muhadhiri Dr Tukae Mbegalo anafanya tafiti kuhusu elimu kwa watoto waliopo shule za awali lengo kuwaandaa watoto mapema ili kupata watu wenye uweredi na elimu pamoja na ujuzi wa kutosha ambao utasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na tanzania kwa ujumla .
Muhadhiri Dr Tukae Mbegalo amewapongeza na kuwashukuru waandaaji wa kongamano lilowajumuisha watafiti na wadau mbalimbali kutoka ulimwenguni na bara la Africa amesema haya kwenye kongamano la siku mbili jijini dar es. salaam.
Habari picha na Ally Thabit
Asanteni sana habari nzuri zenye kujenga.pia napenda sana namna mnavyoandika habari za uhakika
ReplyDelete