Thursday, 25 July 2024

MAENDELEO BANK YATOA GAWIO KWA WANAHISA WAKE

 Ndugu waandishi wa Habari,Mtakumbuka  Kwamba Mnmo tarehe 17 Aprill 2024,uongozi wa maendeleo bank uliongea na uma kupitia waandishi wa habari na kutangaza kwamba bank yao ya maendeleo Bank Plc ikiwa ni bank ya kwanza  nchini kuorodhoshwa Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE) wakati wa kuanzishwa kwake  kupitia dirisha la dogo  la EGM, imewekwa historia ya kuwa bank yenye faida kwa miaka 9 mfululizo kuanzia mwaka  wake wa piliwa kuanzishwa kwake  yaani mwaka 2015.

Aidha umma ulitaarifiwa kwamba matokeo ya kifedha ya mwaka 2023 yanaonesha uimara na ukuaji thabiti wa Maendeleo Bank katika soko la mabenki hapa nchini. Katika mwaka huo,bank ilikuza faida kwa 66% baada ya kodi. Ambapofaidabaada ya kodiiliongezeka hadi shilingi za kitanzania bilioni2.3 kutoka shilingi bilioni1.4 mwaka 2022.

Ukuaji huo wa kuvutia  faida ulichangiwa zaidi na mikakati mizuri ambayo bank imejiwekea na inayosimamiwa vyema na uongozi wa bank pamoja na ushirikiano mzuri wa  wateja na wadau mbalimbali. Uongozi wa bank umeainisha baadhi ya vichocheo vya mafanikio haya makubwa ambavyo ni pamoja na 

;1 Ukuajiwa faida baada ya kodi kwa asilimia 66 kutoka shilingi za kutanzania bilioni1.4 mwaka 2022 hadi shilingi bilioni2.3 kwa mwaka 2023.

2. Kuongezeka kwa Amana  za wateja kwa asilimia 15 kutoka shilingi za kitanzania bilioni78.0 mwaka 2022 hadi shilingi za kitanzania  bilioni 90.0  mwaka 2023.

3. Kuimarika kwa ubora wa mikopo kutoka mikopo chechefu ya asilimia 5.2 mwaka wa 2022 hadi asilimia 4.95 mwaka wa 2023- hiiimechangiwa na kuimarika  kwa hali ya uchumi na kuwafanya wateja walipe mikopo kwa wakati.

4.Kuongezeka kwa mikopo kwa wateja kwa asilimia 21 kutoka shilingi za kitanzania bilioni 61.0 hadi shilingi za kitanzania bilioni 74.0 mwaka 2023.

5.Kuongezeka kwa jumla ya Mali za bank kwa asilimia 17 kutoka shilingi za kitanzania bilioni 107.0 mwaka 2022 hadishilingi bilioni 125.0 mwaka 2023.

6.Kuimarika kwa mtaji wa bank kwa asilimia 12 kutoka shilingi za kitanzania bilioni 17.0 mwaka 2022 hadi shilingi za kitanzania bilioni 19.0 mwaka 2023.

Hivyo basi kutokana na sera ambayo bank imejiwekea  kuhusu ugawaji wa sehemu ya faida kwa wanahisa 'Gawio' ambapo bank  hutoa asilimia 50 ya faida yake kwa wanahisa wake . Hivyo kwafaida ya mwaka 2023 shilingi bilioni 2.35 jumla ya gawio ni shilingi  bilioni 1.17 . Hii ni sawa na  shilingi 44 kwa kila hisa. Mwaka jana gawio lilikuwa sawa na shilingi 26 kwa hisa. Sawa na ongezeko la asilimia 69.

Bank Kuu ya Tanzania  imeruhusu gawio hili kutokewa na pia  Mkutano wa wanahisa uluofanyika tarehe 22 Juni2024, ukumbi wa msasani tower ulipendekeza gawio hilo liwe kwa mfumo wa hisa badala ya fedha taslimu. Hivyo basi kila mwanahisa atapewa hisa za ziada kwa thamani halisi ya gawio analo stahili kupewa. Maamuzi haya yalifikiwa ili kuowezesha bank kuimarisha zaidi mtaji wake hasa kipindi hiki ambapo bank imepata kibali cha kutanuwa na kufanya kazi nchi nzima .

Nipende kutumia fursa hii kuwataarifu waandishi wa habari kwamba Maendeleo  Bank imepata kibali rasmicha kupanda hadhi na kuwa bank inayofanya kazi nchi nzima  ikiwa ni pamoja na kufunguwa matawi nje ya Der es salaam.  Mafanikio haya yalisubiriwa kwa hamu kubwa kwa miaka  mingi kutokana  na kigezo cha mtaji ambao bank ilikuwa na hadhi ya kikanda. Kwa sasa  Bank imefikisha mtaji wa bilioni 19 ambao unakidhi kuiwezesha  bank kufanya kazi nchini kote. Ili bank iruhusiwe kufanya kazi nchini kote ni lazima mtaji wake uwe zaidi ya shilingi bilioni 15.

Mwisho nipende kuwakumbusha ndugu waandishi wa habari na uma  mzima  wa watanzania kwamba bank inaendelea kuwekeza  kwenye teknolojia na sasa tuko hatua  za mwisho katika kuanzisha  huduma mpya  za kidigitali kama bank ya mtandao ( Internet banking), mfumo wa ukusanyaji wa malipo ikiwemo ada za shule (PCS) na mikopo kwa njia ya simu, hii itaeezesha  bank kuongeza faida  kwa fedha za wanahisa kwa mwaka 2024 na  kuboresha njia mbadala za upatikanaji wa huduma  kwa wateja  wetu.

Katika juhudi za kuboresha  huduma , mwaka huu 2024,tumefungua tawi jipya  Mbagala ambalo ni tawi letu la tano tukiwa na lengo la kuwasogezea huduma  wateja wao na wakazi wa Mbagala na maeneo jirani. Haya yamesemwa  na kiongozi wa Bank ya Maendeleo jijini dar es salaam  Ofisini kwao.

Habari na Ally Thabit 



No comments:

Post a Comment