Thursday, 25 July 2024

WAZIRI WA UJENZI AWAPONGEZA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA (TBA)

Inosent  Bashungwa Waziri wa Ujenzi amesema Wakala wa Majengo Nchini Tanzania (TBA) wanatekeleza ujenzi wa miradi kwa vitendo na gharama nafuu . Huku akiwataka watumishi wa serikalini wanapopangishwa  nyumba na wakala wa majengo (TBA) wazilinde na kuzitunza pia walipe kodi kwa wakati.

Waziri Inosent  Bashungwa amewapongeza wakala wa majengo kwa kuweka vitasa janja kwenye nyumba walizo jenga n kuwepo kwa mifumo ya ulipaji wa umeme na maji rafiki na wezeshi amesema haya wakati wa uzinduzi wa nyumba ya ghorofa  yenye uwezo wa kukaa familia 16 na jumla ya gharama zilizotumika kujenga nyumba hii ni bilioni 5 fedha za kitanzania . 

 Na hapa pichani waziri wa ujenzi Inosent  Bashungwa akiwa ameambatana na mkurugenzi mkuu mtendaji wa TBA  Daudi Kandolo huku akiwemo mkui wa mkoa wa da es salaam  na mwenyekiti wa ccm kinondoni . 


Habari picha na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment