Tuesday, 30 July 2024

MKURUGENZI WA TRS AWATOA OFU WATANZANIA


 Mkurugenzi  Mkuu  Mtendaji  wa Shirika la Reli tanzania (TRS) Mwandisi Masanja Kadogosa amesema usafiri wa treni ya umeme (SGR) imezingatia makundi yote wakiwemo watu wenye ulemavu  kwenye vituo vya kupandia treni ya mwendo kasi (SGR) kwani miundombinu ni rafiki na wezeshi na kwenye mabehewa kuna viti mwendo kwaajili ya watu wenye ulemavu wa viungo. Kwa upande wa watu wasioona mlangoni pindi anapoingia kwenye mabehewa mazingira rafiki na wezeshi. 

Mwandisi Masanja Kadogosa amempongeza rais Dr Samia  kwa kutoa fedha kwaajili ya kukamilisha mradi wa SGR anaamini kuwa tarehe 1 /8/2024 uzinduzi wa safari za dar es salaam mpaka Dodoma utasaidia kukuwa kwa uchumi wa tanzania na mtu mmoja mmoja .

Pia amempongeza Waziri wa Usafirishaji na Uchukuzi  Prof Makame Mbarawa kwa kazi kubwa anayoifanya katika kusimaia ujenzi wa SGR pamoja manunuzi ya vichwa vya treni na mabehewa yake . Mwandisi Kadogosa amewataka watanzania kuitumia treni yao ya umeme kwani bei nafuu usafiri wake wa haraka na yeye amewaakikishia watanzania safari zao zitakuwa za uwakika na usalama  amesema haya makao makuu ya trs jijini dar es salaam  wakati akizungumza na wanahabari.

Habari na Ally Thabit 


No comments:

Post a Comment