Tuesday, 9 July 2024

MKURUGENZI WA RANJI YA NARCO AELEZA PUNGUZO LA BEI YA NG'OMBE


 Mkurugenzi  wa Ranji ya Narco Mohamed  Mbwana amesma serikali imetenga ardhi ekta 12 elfu lengo kufuga ng'ombe ambao nyama za  ng'ombe hawa zitauzwa nje ya nchi ambako kwa sasa tanzania  kupitia ranji Narko wanauza nyama ya ng'ombe falme za kiarabu.

Pia ranjit ya Narco inauza ng'ombe wenye ubora kwa bei ya punguzo milioni mbili na lakitano sawa na asilimia 29% ambako mwanzo ilikuwa milioni tatu na lakitano aina ya borani ng'ombe aina ya mitamba milioni moja na lakitano kati ya asilimia 40% ya bei punguzo apo awali ilikuwa inauzwa mitamba milioni mbili na laki tano .

Mkurugenzi  Mohamed Mbwana amesma mikoa ya ranjit ya narco too Rukwa,Karambo,Ruvuma,Morogoro,Mkata na Dodoma Kongwa. Pia amesema bajeti ilioandaliwa kupitia wizara ya mifugo itasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa chanjo,Uwepo wa ng'ombe na maitaji mengine.

Ametoa rai kwa wananchi waitumie ranjit ya narco ili waweze kujiajili kupitia sekta ya mifugo amesema haya kwenye maonyesho ya sabasaba ya 48 jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit. 

No comments:

Post a Comment