Saturday, 4 November 2017

WAZIRI WA AFYA AWAFUNDA TFDA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA

Waziri wa afya ,jinsia,watoto na wazee  UMMY MWALIMU amewataka watendaji wa mamlaka ya chakula na dawa [TFDA] wasiwe kikwazo cha mafanikio kuelekea Tanzania ya viwanda na badala yake wawe chachu katika kuelekea Tanzania  ya viwanda na uchumi wa kati . kwa kutowa vibari kwa wakati, kuepukana na rushwa na wawe wazarendo amesema haya kwenye makao makuu ya TFDA jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa MAHABARA HAMISHIKA

habari picha na ALLY THABITI

WAGENI WATAKIWA KUTOTUMIA NJIA ZA PANYA

Moja ya viongozi kutoka Burundi  amewataka watu kutoka nje ya nchi pindi wanapoingiza madawa na chakula nchini Tanzania wafike kwanza kwenye mamlaka ya chakula na dawa [TFDA]  kwaajili ya kupata vibari

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

WHO YAAIDI MAZITO TFDA

Mwekiti wa kamati ya ukaguzi na usimamizi wa virutubishi ya bodi ya ushauri ya wizara [MAB] kwa TFDA  bi ZAINA THABITI  ameswema wanaunga mkono jitiada za serikali katika kudhibiti dawa bandia  amesema haya wakati waziri wa afya  UMMY MWALIMU  alipozinduwa MAHABARA HAMISHIKA  kwenye ofisi za TFDA

 habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

TFDA YAMTOA WASIWASI WAZIRI WA AFYA

Mkurugenzi mtendaji wa  mamlaka ya chakula na dawa[TFDA]  HIIT B.SILO  amemwambia waziri wa afya UMMY MWALIMU kuwa wao TFDA watafanya kazi kwa umakini na uweredi zaidi. lengo kumuunga mkono rais  MAGUFULI  katika kuelekea Tanzania ya viwanda. pia ameishukuru serikali kwa kuwapa kibali cha kuajili watumishi 49 kwani wakaguzi 27 wataenda kufanya kaguzi katika kanda na vituo vya forodha na wachunguzi wa mahabara 18.Pia amesema TFDA watapambana katika kudhibiti dawa bandia na wataondowa changamoto ya uchache wa dawa ingawa ni changamoto katika Dunia

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

JUKWAA LA KATIBA KUTINGA MAHAKAMANI

Mwenye kiti wa jukwaa la katiba EDWINI MWAKAGENDA  amesema baada ya kuzuiliwa na jeshi la polisi kutofanya maandamano tarehe 30/10/2017 . wao jukwaa la katiba wanaenda mahakamani kwaajili  ya kudai haki yao ya msingi kwaajili ya kufanya maandamano ambayo yamezuiliwa na jeshi la polisi  Mwwenyekiti wa jukwaa la katiba  EDWINI MWAKAGENDA  amesema sababu tatu zilizotolewa na jeshi la polisi azina mashiko .zikiwemo kutothibitisha kwa mgeni rasmi kushiriki kwenye maandamano, umbali na kuanza kwa mitihani ya Taifa ya kidato cha 4.  hataivyo EDWINI MWAKAGENDA  amesema lengo la jukwaa la katiba kufanya maandano ni kumpongeza rais  MAGUFULI kwa utendaji wake wa kazi na kumfikishia ujumbe wa kufufuwa na kuendeleza mchakato wa katiba mpya

hhabari picha  na  ALLY THABITI

Tuesday, 31 October 2017

WAKAZI WA KINONDONI WATAKIWA KUTII SHERIA ZA MAZINGIRA BILA SHURUTI

Afisa mazingira kutoka halmashauri ya Kinondoni  ARUBATI MGEBUSO  amewataka wananchi wa kinondoni na watanzania kwa ujumla kufuata na kuzitekeleza sheria za utunzaji wa mazingira ili kuwa na mazingira safi , bora na salama kwaajili ya afya zetu . amesema mafunzo alioyapata kutoka baraza la mazingira  [NEMKI]  atayatumia katika kuelimisha jamii

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

UBUNGO YAIPA TANO BARAZA LA MAZINGIRA

Afisa mazingira kutoka halmashauri ya Ubungo EZRA GUYA amesema kutokana na mabadiliko ya kiteknorojia katika uchafuzi wa mazingira mafunzo anayo yapata kutoka baraza la mazingira [NEMKI] yatamuwezesha kukabiliana na uchafuzi wa mazingira waaina yeyote . amesema viwanda vilivyojengwa kwenye makazi ya watu katika halmashauri ya Ubungo ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira katika jamii .Pia maji taka na kelele mbalimbali ni vyanzo vikuu vya uchafuzi wa mazingira

habari picha na  ALLY THABITI