Thursday, 23 February 2023

TAASISI YA AG GENERGIES YAWATAKA WANANCHI KUTUMIA BIDHAA ZAO

MUSSA IBRAHIM ni mkurugenzi wa Kampuni ya AG ENERGIES amewataka watanzania na wasio kuwa watanzania kutumia bidhaa zao za Solar na kila mtu anapata solar kulingana na solar yake, pia wanamahospital na mahotesl

Habari kamili na Victor Stanslaus

RISHIT RADIA MKURUGENZI

 Mkurugenzi Rishit Radia Mkurugenzi mkuu wa kiwanda cha kahawa amesema wanafanya kazi na wakulima zaidi ya 800 kiwanda cha kusaga na kusafisha alafu wanapaki kwenye paketi

ujazo milimita 250 wanaweka kwenye gunia kilo 60 kwaajili ya kahwa inaladha tamu, watu wanje wanafurahia pamoja na wakulima wameenea Tanzania nzima na kimataifa zaidi. kiwanda kipo talime

Haya yamesemwa na mkurugenzi wa kiwanda cha NORTHERN HIGHLANDS COFFEE COMPANY

Habri kamili na Victoria Stanslaus

Madaktari bingwa wa MOI wapewa mbinu za kisasa za upasuaji wa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo.

 



Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya  na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) zimeanza kutoa  mafunzo maalum ya upasuaji wa  vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo kwa mbinu za kisasa kwa madaktari bingwa waliohitimu katika chuo hicho ambapo wagonjwa 4 wamefanyiwa upasuaji huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface  amesema mafunzo hayo yanaongozwa na Mkufunzi maalum kutoka hospitali ya St. Luke`s, Ugiriki kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutoa matibabu ya kibobezi.

“Mafunzo haya ni endelevu ambapo wataalam wetu  watafundishwa upasuaji wa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo kwa mbinu za kisasa  ambapo mpaka sasa wagonjwa wanne kati ya saba waliopangwa wameshafanyiwa upasuaji huo” amesema Dkt. Boniface

Aidha,  Dkt. Boniface ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongwa na Rais  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya kwani zaidi ya Millioni 50 zimeokolewa kama wagonjwa hao wangetibiwa nje ya nchi.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa Ubongo  na  Mishipa ya Fahamu Dkt. Nicephorus  Rutabasibwa amesema Madaktari bingwa watatu wa MOI waliohitimu Chuo cha MUHAS watafundishwa mbinu za kisasa za na za kibobezi zakutibu magonjwa ya  mishipa ya damu kwenye ubongo.

“Mafunzo haya yamegawanyika katika sehemu nne ambapo tunalengo la kuwafanyia wagonjwa  40 katika kipindi cha mwaka mmoja kwa ajili ya  kuwajengea uwezo wataalam wetu ili baadae wawafundishe wenzao waliopo katika hospitali mbalimbali nchini” amesema Dkt. Rutabasibwa

Naye, Mtaalamu Bingwa Mbobezi wa Mishipa ya damu kwenye Ubongo kutoka hospitali ya St. Luke`s kutoka Ugiriki Prof. Athanasios Petridis amesema anafuraha kubwa kuwa MOI na kutoa mafunzo ya kibobezi ya upasuaji wa kuzibua vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo na  baada ya mafunzo hayo wataalam hao watakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya upasuaji huo.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa Ubongo Dkt. John Michael Mtei  ameushukuru uongozi wa Taasisi ya MOI kwa mafunzo hayo kwani yamewajengea  uwezo  wa kutibu magonjwa ya mishipa ya damu kwenye ubongo .

habari picha na Victoria Stanslaus

Friday, 17 February 2023

Picha: Rais Samia amewasili Addis Ababa nchini Ethiopia

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)




MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AWATAKA TANROADS NA TARURA KUTEKELEZA MIRADI

Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amewataka TANROADS na TARURA kutekeleza ujenzi wa Barabara zilizopo ndani ya mkoa wa Dar es Salaam kwani mbunge wa Mbagala Chaurembo amesema katika jmbo lake la mbagala kwa kiwango kikubwa barabara bado hazijatengenezwa nae mbunge wa kibamba amelalamikia kutopewa kipaumbele barabara zake. Huku Mbunge Bona Kalua akiwataka TARURA waeleze lini watatengeneza barabara kwenye jimbo lake na wathibitishe kama pesa wanazo nae Mbunge Ndungulile wa Kigamboni akitoa kilio kuhusu ujenzi wa barabara wa mwendo kasi katika jimbo lake la kigamboni.

Meneja TARURA amesema barabara za DMDP zitajengwa katika jiji la Dar es Salaam kwani Benki ya Dunia iko Tayari kutoa hizo fedha na michakato imeanza hivyo ifikapo mwezi 11-2023 miradi ya barabara itatekelezwa kwa vitendo. Amewatoa hofu wabunge na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa TARURA itatekeleza kwa vitendo na sio kwa maneno.

Habari kamili na Ally Thabith

RIDHIWANI AGAWA PIKIPIKI KWA WATENDAJI WA KATA SITA NA KUPOKEA

 


Naibu Waziri wa Ardhi ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amegawa pikipiki kwa watendaji wa kata 6 za Halmashauri ya Chalinze, pamoja na kutembelea kiwanda cha Uzalishaji wa marumaru cha Keda.

Pia, amepokea vifaa tiba kwa ajili ya Vituo Vya Afya kwa ajili ya Vituo Vya Afya Viwili Kata za Kibindu na Msata na Zahanati vijiji 11.

Akigawa Pikipiki hizo, Ridhiwani amewakumbusha Watendaji kutumia vifaa hivyo kwa kuzingatia makusudio ya kutolewa kwa vyombo hivyo vya moto ikiwemo kwenda kusikiliza wananchi na kutoa ufumbuzi wa changamoto zao.

Vilevile akikabidhi vifaa tiba wamehimizwa kuvitunza na kuvitumia kwa makusudio vifaa hivyo.

"Kazi kubwa inaelekezwa kituo cha Afya Miono ambapo kazi ya ujenzi wa miundo mbinu inapaswa kuwa kipaumbele";: Kwa upande wa kiwanda tumewashukuru wawekezaji kwa kutambua mchango wa Raisi Dkt. Samia Suluhu #KaziInaendelea

Habari Picha na Ally Thabith

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AKUTANA NA VIONGOZI WA CCM NA WASERIKALI

 Amos Makala Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam tarehe 15/02/2023 amekutaka na viongozi wa ccm mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam wa ngazi zote pamoja na viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali lengo kuweka mikakati ya maendeleo ya chama cha mapinduzi kwa kuitekeleza kwa vitendo, pia waweze kutambuana kwani ni wapya.

Habari kamili na Ally Thabith