Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amewataka TANROADS na TARURA kutekeleza ujenzi wa Barabara zilizopo ndani ya mkoa wa Dar es Salaam kwani mbunge wa Mbagala Chaurembo amesema katika jmbo lake la mbagala kwa kiwango kikubwa barabara bado hazijatengenezwa nae mbunge wa kibamba amelalamikia kutopewa kipaumbele barabara zake. Huku Mbunge Bona Kalua akiwataka TARURA waeleze lini watatengeneza barabara kwenye jimbo lake na wathibitishe kama pesa wanazo nae Mbunge Ndungulile wa Kigamboni akitoa kilio kuhusu ujenzi wa barabara wa mwendo kasi katika jimbo lake la kigamboni.
Meneja TARURA amesema barabara za DMDP zitajengwa katika jiji la Dar es Salaam kwani Benki ya Dunia iko Tayari kutoa hizo fedha na michakato imeanza hivyo ifikapo mwezi 11-2023 miradi ya barabara itatekelezwa kwa vitendo. Amewatoa hofu wabunge na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa TARURA itatekeleza kwa vitendo na sio kwa maneno.
Habari kamili na Ally Thabith
No comments:
Post a Comment